Kutokana na longo longo za tiba za kisasa, je turudi kwenye mitishamba?

ngulukizi

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
510
1,431
Hapo zamani wazee wetu walikuwa hawajui haya mambo ya tiba za kisasa wengi wao wao walikuwa wanajitibia kienyeji sana na wala hawakuwa wanasumbuka. Kama mfano mtu aliyevunjika alitibiwa kienyeji na alipona kabisa kwa wale watoto waliochelewa kutembea kulikuwa na dawa wanaogoshewa kuanzia shingoni kushuka chini na ndani ya siku mbili mtoto mtoto alitembea.

Ila siku hizi mtoto akiwa hivyo ukimpeleka hospitali kuna longo longo kibao mara hivi kipindi cha nyuma mtoto akichelewa kukaa kuna dawa zilitumika za kienyeji ila siku vijana watoto wetu wakichelewa kukaa tunahangaika sana hivi ni wapi tulipokosea au kwa kuwa tumeacha mila zetu ndio mana tumekua hivi siku hizi.

Hebu wadau tushauriane. Je, turudi kwenye tiba zetu, tiba zilizomfanya mama mjamzito ajifungue kwa wepesi pale anaponyeshwa dawa na si kwa operation kama sasa hivi wengi inavyowakuta.
 
Back
Top Bottom