Kutokana na kusuasua kwa EAC, nashauri EAC ijiunge na SADC, na SADC ijiunge na Sub-Saharan Africa Free Trade Area (SSAFTA)

z12f

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
635
458
Kutokana na kusuasua kwa EAC, nashauri nchi zote za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zijiunge na SADC. Hili lifanyike wakati Tanzania ni Mwenyekiti wa SADC.

Mimi nadhani tuachane kabisa na masuala ya EAC monetary union (masuala ya sarafu moja ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki). Sidhani kama sarafu hiyo itafanikiwa. Mimi nadhani pia tuunde Sub-Saharan Africa Free Trade Area (SSAFTA).

Inaweza kuwa na currency yake ambayo itatumika sambamba na national currencies. Currency ya SSAFTA inaweza kuitwa 'Shaba'.National currencies zisiwe abolished, kama zilivyokuwa abolished huko Euro zone.

Halafu ni vizuri watu wafahamiane zaidi at the cultural and personal level. Halafu watu wa mataifa haya wasihujumiane na wapendane na kushirikiana kiukweli na kindugu. Taifa moja lisi jione bora kuliko taifa jingine.

Makao makuu ya monetary authority ya SADC au na ya monetary authority ya SSAFTA yawe Arusha au Mwanza.

SSAFTA inaweza ikawa mbadala mzuri kwa nchi ambazo zinaogopa kujiunga na African Continental Free Trade Area (AfCFTA).

NB: Zone hii ya SSAFTA ijenge ustawi wa mwafrika mweusi.
 
Dawa nikuwa na wizara ya mambo ya ndani ya pamoja na wizara ya ulinzi tukifakiwa hilo ugomvi utaisha, iwe muungano wa Tanzania na Zanzibar
 
Back
Top Bottom