Kutoka Zanzibar : Tanganyika yakalia Billions za Zanzibar [Climate Change] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka Zanzibar : Tanganyika yakalia Billions za Zanzibar [Climate Change]

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 11, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Kuna pesa zimetolewa na United Nations kuhusu program ya mabadiliko ya Climate Change (siku hizi wanaita mabadiliko ya tabia nchi – climate change).
  Pesa hizi zinafika mabilioni ya shillings za TZ – na madhumuni yake makubwa ni kutoa kwa nchi kama Zanzibar – nchi za visiwa (Island states) ambazo kimaumbile ndio zinazoathirika zaidi. Naam…Zanzibar kweli imeathirika sana katika suala hili la climate change.
  Pesa hizi zinatakiwa wapewa SMZ na zifanyiwe program katika idara kama Mazingira, kilimo, Idara ya hali ya hewa, taasisi kama za viwanda n.k – ni pesa nyingi na zinafika billions.
  Hizi wamzikalia akina Membe, hazina na taasisi za Fedha za Tanganyika.
  Kadhalika, kuna component ya pesa kama hizi kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ziliidhinishwa katika mkutano wa climate change ‘adaptation’ uliofanyika, Kampala Uganda, March-April 2012.
  Katika Mkutano huo, wajumbe kutoka Tanganyika walisema wazi wazi kuwa ‘Zanzibar haina foreign accounts/ na haiwezi kuwa signatory” katika suala hili — so pesa hizi ziingiawe katika account ya Tanganyika – hazina au popote pale. Hizi pia ni bilions.
  Wapo wajumbe kutoka zanzibar waliohudhuria vikao kama hivyo – kutoka mazingira, kilimo na hata idara ya maafa Zanzibar.
  Ukiachilia zile alizozikalia Membe, hizi walizikalia akina Jumanne Maghembe, au nani na nani sijui, wote mafirauna kwa Zanzibar. Hili suala la mambo ya pesa — cabinet ya Zanzibar, SMZ wanalizungumza kila wanapokutana, but no solution na haipatikani aslan abadan.

  source: mtandao wa kizenji Mzalendo.net .
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  [h=1]TETEZI:MEMBE AKALIA 200BN/= ZA ZANZIBAR[/h] Written by CCM-ASP Zanzibar // 05/08/2012 // ZenjiLikiz // 31 Comments

  [​IMG] Kumbe zipo sababu nyingi kuwasikia wajumbe wetu wa BLW wanasema kwa ukali, ghazab na jazba wanapozungumzia haki ya Zanzibar ndani ya Muungano; dhulma inayofanyiwa Zanzibar ndani ya Muungano – na kelele zinapokuwa nyingi, zinaundwa kamati. Mpaka sasa zimeundwa kamati 200 kutatua kero (KARO) za Muungano; karo hazijasafika.
  Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na "Ushirikiano wa Kimataifa" amekalia pesa za Zanzibar zipatazo 200bn/= zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuipa Zanzibar kuendeleza/kufufua specifically zile EPZ, maeneo huru ya kiuchumi Zanzibar.
  Waliotoa pesa hizi wakiwemo UAE/Rasil Khemah – ambao viongozi wetu wote watatu (Shein, Seif-1 na Seif-2) wamekuwa kiguu na njia kutafuta misaada. Imepatikana Membe – laatul laah amezuia, just kutia saini tu ili pesa ziwe released.
  Kipengelea kimoja kinachomfanya Membe ndiye atiwe saini/pesa za misaada, mikopo, zawadi n.k zinapoingia katika foreign currency au misaada kama hiyo – Zanzibar hairuhusiwi kusaini, kwa sababu ‘si nchi' inatakaiwa TZ ndio imwage wino.
  Huu ni mwezi wa pili, Membe amekalia barua yetu na pesa zetu, halali yetu. Baadaye wanakuja Zanzibar eti kujiliza baada ya meli kuzama.
  Hiyo ndio TZ, na huo ndio Muungano wetu uliodumu miaka 48 kwa Bara kuidhulumu Zanzibar.
  * Plus, jana tu Abubakar alikuwa anasema ndani ya BLW kuwa hao hao akina Membe wameinyima Zanzibar fursa ya kuhudhuria vikao muhimu vya kimataifa kwa kuwanyima wajumbe wake visa, just kwa sababu wao watanganyika hawakwenda au hawakutakiwa kuwemo.
  Ushauri wangu: MAMBO YA NCHI Z ANJE IONDOSHWE KABISA KATIKA LIST YA MUUNGANO (GET ME RIGHT PLEASE, SIO SUALA LA KUGAWANA MABALOZI, LA HASHA). ONDOA FOREIGN AFFAIRS KATIKA LIST HIYO FOR GOOD.
  Mbaya zaiid katika sakata hili la Membe kuzuia pesa zetu, naibu wake anaitwa Mahadhi Juma Maalim – mzanzibari wa Muyuni/na Mungoni (huyu ni kambi ya NO vote katika referendum, na ndiye group la akina Samia, Haroun, Shamsi, Perera Ame Silima – wanachochea watu wa kusini wasema NO serikali tatu au muungano wa mkataba). Mahadhi, Kazi ya uzinzi haifai na kutafuta wanawake kuowa. Kuwa na akili wewe, nchi yako inazamishwa.

  Mbona Meli 39 za Iran wamezikubali na zinapeperusha bendera ya Tz halafu wanapotaka kuwekewa vikwazo wanatukumbuka, hizo ni hulka tu za wakosaji, Membe hana ubavu wa kuzuia hela ya visiwani kwani sio Signatory kwanza angegoma katika meli za mafuta km angekuwa na ubavu huo
   
 3. BWANYEENYE

  BWANYEENYE Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 4. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi ni upeo au nn hasa ndgu zangu? Mwezi wote wa Ramadhan huu then mtu anaamua maksudi kusema uongo tu, kwa staili hii ya kuongopa kiasi hiki then mnapata wafuasi wanaowaamini bila shaka wazanzibar wengi wana tatizo kubwa la 'common sense'. Wizara ya mambo ya nje ya Tz iwanyime visa? Dah!
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280
  ..mimi naunga mkono Tanganyika kuzikalia fedha hizo.

  ..dawa ni kuendelea kuwabana wa-ZNZ mpaka wajitoe moja kwa moja ktk muungano.

  ..wa-Tanganyika hatutaki muungano wa serikali 3, hatutaki mkataba. LET ZNZ GO!!
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  JokaKuu

  Vipi tena Mkuu?

  Misimamo yako inabadilika kwa kasi kwa siku za karibuni.

  Jana ,ya juzi umesema tukubali serikali tatu au Muungano wa mkataba japo kwa shingo upande ili kelele ziishe. Inaonekana tunapenda kusikia kelele.

  Tanganyika kukalia fedha hizo kama ni kweli ni kosa. Ndio UAMSHO hupata hoja yakusema waachiwe wapumue.

  Kama Tanganyika inakalia fedha hizi, hii ni kuongeza kero za muungano au ndio upendeleo wenyewe huo? Kuna baadhi yetu tunasema Znz inapendelewa.

  Kwa nini tujenge tabia ya uchoyo wakati ukarimu ndio tabia njema?

  Kama Znz wamefanya juhudi kupata hela hizi, Tanganyika ilitakiwa ifanye fasta fasta kuona zinafika kule zinakotakiwa ili zitumike katika lengo linalokusudiwa. Tuoneshe upendo au tumeamua kuonesha kwa vitendo kuwa maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana?
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Visa haitolewi na wizara ya mambo ya nje, ila wizara inafanikisha kupatikana kwa visa kutoka balozi za nchi husika. Kuna barua/ hati ambayo wizara huandika pamoja na pasi za wahusika na kuziwasilisha huko ubalozini.Na hapo balozi husika hutoa visa kwa wakati muafaka, sio nenda, uje kesho.

  Huenda wizara ilikalia kutoa hizo barua/ hati za utambulisho.

  Katika Tz yetu haya yanawezekana sana. Roho mbaya, kumkatisha mtu tamaa kwa mzawa/mzalendo ni sera katika Tz.
   
 8. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii introductory letter si yaweza kuandikwa hata na zile ofisi zao za kule kilimani(naamini bado zipo) just na passpt namba zao tu,then mhusika anakata mitaa mwenyewe,amini maneno yangu nonda, muungano ni kero lakini vingine ni uzushi mtupu. Anway, na hizi fedha zilizokaliwa hebu atuambie zimetoka ktk mfuko gani wa dunia,na hizo za Afrika Mashariki zimetoka ktk mfuko/iniative gani?
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Hili la intro letter pengine inawezekana lakini Tz ina utaratibu wa head office, amri ya mkuu/ bosi.

  Kweli habari iliyo hapa haijitoshelezi ila niliifuatilia na kukutana na hii

  Link Zanzibar pushes to join island alliance to confront climate change - AlertNet
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280

  Nonda,

  ..ulichokishuhudia siyo kuyumba ktk msimamo, bali ni hali ya kukata tamaa kwamba muungano uta-survive.

  ..quite frankly, that will b a sad day for me.

  ..option ya mwisho, au "plan z," kwangu mimi ni kwenda kwenye serikali 3, au kwenye "muungano wa mkataba."

  ..hopefully, tukifika huko[serikali 3, au mkataba] watatokea wa-Tanganyika wenye msimamo kama wangu ambao watakataa hii hali inayoendelea sasa hivi ambapo wa-Tanganyika tumekuwa kama "misukule" ya wa-Zanzibar.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Umezipitia hizi?

  Link 1. Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa |
   
Loading...