Kutoka Viwanja vya Karimjee:Baraza la Eid Fitiri live kupitia Star tv

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Mgeni rasimi ni Raisi Magufuli.Leo sijui atasema nini tena nyie fuatilieni.

Raisi ndio anaanza kuhutubia sasa(17:22)

Raisi kasema mengi sana na pia ametoa ahadi za fedha kwa ndugu zetu waislamu.Hata hivyo kilichonishangaza ni kuona raisi amemkabihi Muft msaada wa fedha(cash) kutoka kwenye bag maalumu ikiwa ni mchango wake kugharamia safari ya mahojaji kwenda Hija.

Nachojiuliza ni kwanini hakukabidhi hundi?Je,kwa taratibu za kiislamu isingekuwa halali kukabidhi hundi kwa Mufti?Je,kiusalama ndio imekuwa sababu ya kushindwa hata kutaja kiwango cha fedha alichokabidhi kwasababu ametoa hela cash?Mh.Raisi haoni kuwa ni risk kwa mtu/ofisi kukaa na hela cash mpaka keshokutwa maana Mabenki hayafanyi kazi kwa siku hizi mbili ambazo ni public holiday?
 
image.jpeg
Baraza la Idd linaendelea viwanja vya Karimjee.Mgeni rasmi ni Rais JPM,wapo pia Mkuu wa Mkoa Makonda,Waziri Mkuu Majaliwa,Rais Mstaafu Mwinyi,Sheikh wa Mkoa wa Dsm,RPC Sirro na Mufti Mkuu wa Tanzania.

Baada ya Salamu,Muwakilishi wa BAKWATA anasoma risala kwa Rais.Msoma Hotuba anaelezea mafanikio ya Mufti Zubeir baada ya kuingia madarakani.Moja ya mafanikio yake ni kufungua milango ya BAKWATA na nchi za nje ambapo kuna wakati ilikuwa kama imefungwa,moja ya mafanikio ya kufungua milango hiyo ni safari za nje ya nchi ambazo zina lengo la kufungua milango ya mashirikiano kati ya BAKWATA na Nchi za nje.Safari ya kwanza ya ushirikiano ilianza nchni Morroco ambapo Mufti ameanzisha ushirikiano na Mfalme wa Morroco juu ya kuendeleza maendeleo ya Waislam.

Safari nyingine ilikuwa nchni Uturuki ambapo Mufti alipata nafasi ya kukutana na uongozi wa kiserikali wa Uturuki na kuanzisha mashrikiano katika mambo ya elimu kwa waislamu na maendeleo ya kijamii.Safari nyingine ni nchni Ujerumani ambapo Mufti anakwenda kujifunza namna Waislam wa Ujerumani wanavyowesa kuishi na watu wa dini nyingine bila mfarakano na baadae atakwenda Afrika Kusini kwa ziara ya kutembelea na kujifunza jinsi watu wa dini na nasaba tofauti wanavyoweza kaishi bila mifarakano ya kidini.

Hotuba pia imeelezea kuwa BAKWATA ipo katika mchakato wa kufungua chuo kikuu Mkoani Dodoma ambacho kitatoa elimu Ya dini na Elimu Dunia.Mkazo utakuwa katika elimu ya dini ambapo Waislamu watafundishwa mambo mbalimbali yahusuyo Uislamu na taratibu zake.

Anafuatia Mufti Zuberi,anatoa shukrani kwa Rais JPM kwa kufika,lakini pia anasema ni mara ya kwanza kwa Viongozi wa Kitaifa kama Rais na Waziri Mkuu kuhudhuria kwa pamoja.Anasema JPM ni kama "Mvua yenye manufaa ambayo hunyesha kwa manufaa wakati muafaka unaohitajika".Mufti anasema Waislam wanamuunga mkono JPM katika uongozi wake,anashukuru mshikamano ulioonyeshwa na Madha'habu mengine katika mfungo huu wa Ramadhan.

Mufti anakemea ufisadi,rushwa na mambo yote yasiyompemdeza Mungu.Anasema mwenyezi Mungu anasema amelaaniwa yule mtoa rushwa,mpokea rushwa na hata yule mkaa kati wakati wa kutoa na kupokea rushwa.Mufti pia kaongelea swala la ushoga,kuwa jamii ya Kiislam na BAKWATA kwa ujumla wanapiga vita tabia za ushoga,amekeemea ugaidi na kusisitiza hakuna uislamu unaoshahabiana na ugaidi na hata hao waliolipua Madina karibu na Msikiti wa Mtume si Waislamu bali ni maadui wa Uislam
Sasa inafuata kaswida kabla ya Rais kuhutubia

Rais anatoa hotuba,anawaambia wale wote waliotaifisha mali za Waislamu wazirudishe haraka na waache tabia ya kuingia mikataba inayowakandamiza waislamu,amewaomba Mufti ahakikishe kuwa Mali za Waislam zinarudi.

Rais ametowa zawadi kwa kikundi cha kaswida cha Vijana wa Kiislam shilingi milioni mbili,pia ametoa zawadi hiyo kwa kijana atakayeshiriki mashindano ya dunia ya kuhifadhi Quran huko Urusi na amemzawadia shilingi milioni mbili....Rais pia ametowa kiasi kikubwa cha pesa kwa Mufti ili kuwapa wale wasio na uwezo kwenda kuhiji Macca mwezi wa 8.Japo kiasi hicho hakijatajwa.

Baada ya hapo shukrani ya mwisho na pia duwa'aa kwa waliofika
 
Baraza la Idd linaendelea viwanja vya Karimjee.Mgeni rasmi ni Rais JPM,wapo pia Mkuu wa Mkoa Makonda,Waziri Mkuu Majaliwa,Rais Mstaafu Mwinyi,Sheikh wa Mkoa wa Dsm,RPC Sirro na Mufti Mkuu wa Tanzania.

Baada ya Salamu,Muwakilishi wa BAKWATA anasoma risala kwa Rais.Msoma Hotuba anaelezea mafanikio ya Mufti Zubeir baada ya kuingia madarakani.Moja ya mafanikio yake ni kufungua milango ya BAKWATA na nchi za nje ambapo kuna wakati ilikuwa kama imefungwa,moja ya mafanikio ya kufungua milango hiyo ni safari za nje ya nchi ambazo zina lengo la kufungua milango ya mashirikiano kati ya BAKWATA na Nchi za nje.Safari ya kwanza ya ushirikiano ilianza nchni Morroco ambapo Mufti ameanzisha ushirikiano na Mfalme wa Morroco juu ya kuendeleza maendeleo ya Waislam.

Safari nyingine ilikuwa nchni Uturuki ambapo Mufti alipata nafasi ya kukutana na uongozi wa kiserikali wa Uturuki na kuanzisha mashrikiano katika mambo ya elimu kwa waislamu na maendeleo ya kijamii.Safari nyingine ni nchni Ujerumani ambapo Mufti anakwenda kujifunza namna Waislam wa Ujerumani wanavyowesa kuishi na watu wa dini nyingine bila mfarakano na baadae atakwenda Afrika Kusini kwa ziara ya kutembelea na kujifunza jinsi watu wa dini na nasaba tofauti wanavyoweza kaishi bila mifarakano ya kidini.

Hotuba pia imeelezea kuwa BAKWATA ipo katika mchakato wa kufungua chuo kikuu Mkoani Dodoma ambacho kitatoa elimu Ya dini na Elimu Dunia.Mkazo utakuwa katika elimu ya dini ambapo Waislamu watafundishwa mambo mbalimbali yahusuyo Uislamu na taratibu zake.

Anafuatia Mufti Zuberi,anatoa shukrani kwa Rais JPM kwa kufika,lakini pia anasema ni mara ya kwanza kwa Viongozi wa Kitaifa kama Rais na Waziri Mkuu kuhudhuria kwa pamoja.Anasema JPM ni kama "Mvua yenye manufaa ambayo hunyesha kwa manufaa wakati muafaka unaohitajika".Mufti anasema Waislam wanamuunga mkono JPM katika uongozi wake,anashukuru mshikamano ulioonyeshwa na Madha'habu mengine katika mfungo huu wa Ramadhan.

Mufti anakemea ufisadi,rushwa na mambo yote yasiyompemdeza Mungu.Anasema mwenyezi Mungu anasema amelaaniwa yule mtoa rushwa,mpokea rushwa na hata yule mkaa kati wakati wa kutoa na kupokea rushwa.Mufti pia kaongelea swala la ushoga,kuwa jamii ya Kiislam na BAKWATA kwa ujumla wanapiga vita tabia za ushoga,amekeemea ugaidi na kusisitiza hakuna uislamu unaoshahabiana na ugaidi na hata hao waliolipua Madina karibu na Msikiti wa Mtume si Waislamu bali ni maadui wa Uislam
Sasa inafuata kaswida kabla ya Rais kuhutubia
Mbona ujumbe wa THE BIG SHOW haujafikishwa ?
 
Mgeni rasimi ni Raisi Magufuli.Leo sijui atasema nini tena nyie fuatilieni.

Raisi ndio anaanza kuhutubia sasa(17:22)
Jiandaeni kuandika makala maana bila Rais kuongea hamna uwezo wa kupata cha kuongea au kuandika!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom