Kutoka Uturuki: Friendly Match, Simba SC yaichapa F.C.E Ksaifa mabao 3-1

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mabingwa wa nchi ya Tanzania Simba Sports Club leo Agosti 4, 2018 imechapa bila huruma F.C.E. Ksaifa mabao 3-1 katika mchezo safi wa kirafiki uliofanyika kwenye dimba la Kartepe Green Park.

Simba ikionyesha kandanda safi na la kuvutia kwenye mchezo huo, ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa Emmanuel Okwi katika dakika ya 16' kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Emmanuel Okwi aliipatia tena bao Simba dakika ya 50' ambapo lilidumu kwa dakika 4 tu baada ya F.C.E. Ksaifa kuandika bao lao la kwanza katika dakika 54 kupitia kwa mchezaji Nader Al-krinsui.

Mshambuliaji matata Meddie Kagere alihitimisha ukurasa wa mabao katika dakika ya 87' akifunga bao la tatu, hivyo mchezo huo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 3 dhidi ya bao 1 la F.C.E. Ksaifa.
IMG_20180804_185656_458.jpg
 
Mabingwa wa nchi ya Tanzania Simba Sports Club leo Agosti 4, 2018 imechapa bila huruma F.C.E. Ksaifa mabao 3-1 katika mchezo safi wa kirafiki uliofanyika kwenye dimba la Kartepe Green Park.

Simba ikionyesha kandanda safi na la kuvutia kwenye mchezo huo, ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa Emmanuel Okwi katika dakika ya 16'. Hadi mapumziko Simba ilikuwa mbele ya bao hilo moja.

Emmanuel Okwi aliipatia tena bao Simba dakika ya 50' ambapo lilidumu kwa dakika 4 tu baada ya F.C.E. Ksaifa kuandika bao lao la kwanza katika dakika 54 kupitia kwa mchezaji Nader Al-krinsui.

Mshambuliaji matata Meddie Kagere alihitimisha ukurasa wa mabao katika dakika ya 87' akifunga bao la tatu hivyo mchezo huo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 3 dhidi ya bao 1 la F.C.E. Ksaifa.View attachment 827078
Mkuu, Umemsahau kusema F.C.E Ksaifa ni timu ya Palestine. Siyo club bingwa ya Morroco
 
Kwani kuna sehemu nimesema hivyo. F.C. E. Ksaifa ndo nimeandika. Tukutane kwa machina maana kule hakuna kujitoa
Hatuna wasiwasi kukutana kwa mchina. Ndiyo siku mtaanza kusambaratika. Tayari mmeanza kusema katika imekiukwa. Mashamba ya mkonge ya Mo yanarudi serikalini.
 
Mkuu nipo sana tu.
Zamu yenu hii muitumie vyema.
Exactly mkuu..hii ni fursa yetu. Na Wewe kama hutaingia kwenye mabadiliko na ukategemea michango, yamkini itakuwa kama Ujerumani timu moja tu..!
 
Back
Top Bottom