Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,
Makamba.jpg
makamba1.PNG


KAULI MBIU YA JANUARI MAKAMBA: TANZANIA MPYA

Ikiwa ni muendelezo wa watangaza nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa ni zamu ya January Makamba kutangaza nia kutokea Mlimani City.

-January Makamba anaomba ridhaa ya chama kusimamishwa kuwa mgombea wa urais kufuatia wana CCM 15 kutangaza nia hiyo ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM.

-Hivi sasa kinachoendelea ni ushuhuda wa watu mbalimbali juu ya uongozi wa Januari Makamba.

-Mmoja wa wananchi wa jimbo la Bumbuli ametamka kuwa, "Januari ana kama Unyerere Unyerere hivi". Hii ana maanisha kuwa kijana ana ufuatiliaji wa hali ya juu na ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia watu.

-Januari ameanza kuongea na amejielekeza moja kwa moja kutanga nia yake ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM, pia amesema kesho kutwa ataenda kuchukua fomu ya urais kutoka kwenye ofisi za CCM, Dodoma.

JANUARI ATATOA HOTUBA HII BILA YA KUSOMA POPOTE. HOTUBA YOTE IPO KICHWANI.[/B




- Januari anasisitiza kuwa Tanzania MPYA itajengwa na viongozi wenye fikra mpya.

Januari ahaidi kuwa na mawaziri wasiozidi 18 tu katika baraza lake la mawaziri endapo chama chake kikimpa ridhaa ya kugombea urais kupitia CCM.

-Januari Makamba anaorodhesha ajenda tano kuu atakazo simamia endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea na hatimae kuunda serikali.

............Update............[/SIZE]

....Januari ahaidi kuwa serikali yake itatoa mikopo maalumu kwa vijana watakaomaliza vyuo vikuu ambao watapata changamoto ya ajira ili na wao waweze kufungua makampuni yao ili waweze kujizalishia kipato.

....Pia amesema katika serikali yake atahakikisha sekta ya nyumba ina mchango wa zaidi ya 25%, wakati sasa hivi ni chini ya 4% ikimaanisha Watanzania wengi hawana makazi. Hivyo katika uongozi wake hilo la makazi atalipa kipaumbele tofauti na ilivyo sasa.

....UVUVI, serikali yake itaanzisha mifuko maaalumu ya kukopesha wavuvi ili waweze kununua vifaa vya uvuvi ili isaidie kuboresha vipato vya wavuvi na pia kukuza sekta hiyo kwa kasi.

....UHABA WA WALIMU, serikali yake itaongeza udahili wa walimu haswa kwa masomo ya sayansi. Pia ameahidi kutatua changamoto za walimu kama vile mishahara yao kuwa duni, kukosa posho na stahiki mbalimbali. Ahaidi serikali yake kutatua kero hizo kwa kukuza na kuboresha maslahi yao.

.... RUSHWA, amesema kuwa kulizungumza na kulipigia kelele tatizo la rushwa sio njia ya kulimaliza tatizo hilo.

...ARDHI, jinsi ya kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Serikali yake itabainisha kisheria maeneo ya kilimo, mifugo na makazi. Pia amesema wakulima na wafugaji watamiliki maeneo yao kisheria. Atatumia teknolojia mpya ya satellite kutekeleza hayo kupitia kituo maalumu kitachoundwa chini ya serikali yake. Lakini pia kituo hicho kitasaidia pia na mambo ya kiusalama.

....AFYA, kila Mtanzania lazima awe na bima ya afya, kila Mtanzania lazima apate huduma bora ya afya bila ya kujali kipato chake.

....MAJI, wakala na mfuko mpya wa maji utaanzishwa vijijini. Hapa kukazia hoja yake, ametolea mfano wa mawakala kama wa barabara (TANROADS) na wakala wa umeme vijijini (RERA) kuwa mafanikio makubwa yamepatikana kupitia uwepo wa mawakala hao. Hivyo sasa kuna haja ya kuwa wna wakala wa maji vijijini. Ahaidi ndani ya miaka kumi kusogeza hudumasafi na salama aya majikwa kaya karibu zote nchini.

....MAPATO YA SERIKALI, hapa anazungumzia namna atakavyopata fedha za kutekeleza ahadi zake. Mambo atayofanya ni yafuatayo:

1. Atahusisha sekta binafsi kwa kina zaidi ambapo serikali haina ulazima kutumia fedha zake yenyewe katika kutekeleza miradi mbalimbali.

2. Kupunguza misamaha ya kodi kufikia 1% ya pato la taifa. Ambapo serikali itaweza kupata kiasi cha kisichopungua bilioni 700 pesa za Tanzania.

3. Kupanua wigo wa kodi, hasa kwenye sekta isiyo rasmi. Serikali yake itaondoa mfumo wa sasa wa kutoza kodi kabla hata ya biashara kuanza. Pia ataweka adhabu kubwa kwa watakaokwepa kodi.

4. kuongeza ufanisi wa TRA, amenukuu rpoti ya kitaalamu iliyohitimisha kuwa TRA kama ikiongeza ufanisi wa asilimia 10% tu, itaongeza ukusanyaji wa kodi kiasi cha bilion 600 kwa mwaka.

5. Mradi wa makaa ya mawe, serikali itapata kiasi cha bilion 800 kama utafanywa kwa ufanisi zaidi.

6. Kila mwenye ardhi yenye hati atatozwa kodi stahiki, kiasi cha bilion 500 kitapatikana hilo likifanikiwa. Hapa ili afanikiwe atahakikisha kwamba wizara ya ardhi inashirikiana na sekta binafsi kupima ardhi ili kumilikisha watu wengi zaidi ili serikali iweze kupata mapato kutokana na ardhi hiyo iliyopimwa.

7. Sekta ya nyuki itatoa bilion 130 kwa mwaka kama itapewa kipaumbele.

8. Meli nyingi za kimataifa hazilipi kodi, serikali yake itarekebisha sheria ya uvuvi ya bahari kuu ili kuongeza mapata kiasi cha bilion 350 kwa mwaka.

.....Update......


[/CENTER]



...Januari amemaliza kwa kutoa rai kwa wanaCCM wote kuacha kugombana..badala yake amewaomba watangaza nia wote kujikita zaidi katika kuelezea namna gani watapambana na matatizo na changamoto za Watanzania.

......Update.....

Wakati wa maswali:

1. Kuhusu michezo: Ni kwa namna gani atatatua tatizo la michezo kusuasua?

2. Namna gani atatatua changamoto za foleni jijini Dar es salaam?

3. Mkakati gani wa kuwasaidia wanamama waweze kupata mikopo midogo midogo?

4. Landa speculators: Hili swali linahusu wale wenye kuhodhi ardhi kubwa huku hawaiendelezi. Je, ni namna gani atawashughulikia watu wa aina hiyo?

Mhe Januari anaanza kudondosha nondo kujibu maswali yote yaliyoelekezwa kwake!

1. Majibu ya swali la kwanza:

- Kuunda academy za michezo ili watoto wadogo wa miaka 6, 7, 8 waanze kufunzwa michezo katika umri huo mdogo.

- Kuwezesha kifedha timu za daraja la kwanza ili iwe motisha kwao na kuepusha mfumo wa sasa wa kutembeza bakuli ambao unawavunja moyo wana michezo.

2. Katoa nondo nyingi sana ila kubwa ni kwamba atajenga flyovers ili kutanua zaidi njia za kutoka katikati ya jiji na kwenda kwenye zile four ateries (njia nne kuu za kutoa Dar). Hili linafanyika kwa miaka chini ya 10 tu, ila amegoma la kuweka foleni kwa sababu itahitaji miaka 50 ili mradi kukamilika. Hivyo kwa uharaka wa tatizo la foleni, njia ya flyovers ndio nzuri zaidi.


4. Majibu kwa swali la nne:

- Ataweka gharama kubwa kwa speculators. Hili ni jambo la muhimu sana na kiukweli dogo huyu ni kichwa! Ameni-impress.
 
Mimi huwa najiuliza, kwa nini wakina nyerere walikuwa wadogo kuliko hawa vijana watia nia lakini hawa wengi weupe saana. Lawama nyingi tu. Ngoja aje.
 
HAMY-D

Weka update basi wengine hatupo dsm na hatuna access na tv wala radio.
 
Last edited by a moderator:
January kawachukue watu wa Bumbuli watoe ushuhuda sio hao uliowanunua.
 
Tangazo Tangazo!

Nikiwa Kama mwanachama hai wa ccm, nikiwa na haki kikatiba ( katiba ya ccm) , na nikiwa na nia, uwezo , moyo wa kizalendo , na nia ya kuitumikia nchi yangu napenda kutangaza kuwa kesho majira ya saa 4 asubuhi nitatangaza nia yangu ya kugombea urais wa jmt kwa kupitia chama changu makini cha ccm, eneo ni Ukumbi wa Nkurumah hall, udsm.

Watu wanashangazwa na kutangaza nia kwa wana-ccm wengi ila hii ni kuonyesha uthubutu na uwezo wetu.

Challenges begins at home.

Don't plan to miss.

Nb:
1.Hakuna magari ya kuja kuwachukua nyumbani
2. hakuna mgao wa fedha
3. usisahau kuja na mchango wa form yangu ya urais....



Hahahaaaaa.......ccm bhana
 
Back
Top Bottom