Kutoka Ukumbi wa JNICC DSM kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Linking Academia, Tourism & Hospitality

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,544
Wanabodi,

Wewe as mwana JF, be the first to know, niko kwenye ukumbi wa JNICC hapa jijini Dar es Salaam, kwenye ufungaji wa mkutano wa kimataifa wa Linking Academia, Tourism & Hospitality.



IMG-20200209-WA0022.jpg


Karibuni,

Paskali
 
Mgeni rasmi kwenye ufungaji ni Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. William Ole Nasha ambaye ameanza kwa kutoa vyeti vya ushiriki.
P
 
Hivi sasa anazungumza Mwenyekiti wa Bodi ya NCT, Imani Kajula, kumkaribisha mgeni rasmi kufunga.
P
 
Tunajitapa tunakuza Kiswahili kiwe lugha ya kimataifa, hapa ukumbuni tuna washiriki 100, kati ya hao, washiriki 99 ni Waswahili Watanzania, mzungu ni mmoja, lakini tunazungumza Kiingereza!, hii live stream ya Kiingereza kuwatangazia Waswahili, kiukweli haijakaa poa!, ila lugha ya tourism na hospitality ni kizungu zaidi!, hata wadada zetu, ukimwambia "nakupenda" unakataliwa, ukimwambia "I love you" unakubaliwa!. Hata mama, ukimuita "mtoto" anakasirika kuwa umemtukana, ila mijibaba, mijitu mizima na wajukuu, inapoitwa "baby!", inafurahi!.
Kiukweli wakoloni wametufanya vibaya na lugha yao!.
P
 
Back
Top Bottom