Kutoka Uhamiaji: Askofu Kakobe asisitiza yeye ni mtanzania. Ang'aka watu wa Kigoma tu kuhojiwa kuhusu uraia

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
753
3,096
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF),Zachary Kakobe amewasili Uhamiaji Dar baada ya kutakiwa kuripoti katika ofisi hizo.

Muendelezo/Sasisha
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema yeye ni raia wa Tanzania ,"anayesema mimi si raia wa Tanzania aniambie ni raia wa nchi gani."

Askofu Kakobe ametoa kauli hii leo Aprili 9,2018 mara baada ya kutoka kuhojiwa kwa takriban saa tatu kuhusu uraia wake katika Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema uhamiaji wanaweza kuwa na nia njema lakini, "kwa nini sasa, kwa nini wanahojiwa watu wa aina fulani wa kutoka eneo fulani la Kigoma. Mbona hatujasikia kutoka Dodoma, Kaskazini wakihojiwa."

"Mimi ni Mtanzania na kama kuna mtu anasema si raia basi aniambie mimi ni raia wa nchi gani," amesema Askofu Kakobe

Amesema, ametakiwa kuacha hati yake ya kusafiria ili iweze kuwasaidia kupata taarifa zake muhimu huku yeye akisisitiza "hiki wanachokifanya kina tia shaka.

Mahojiano ya kiongozi huyo wa kiroho yaliyoanza Saa 4.53 asubuhi hadi saa 7.55 mchana yamehitimishwa.

Ofisi ya Uhamiaji wamtaka Askofu Zachary Kakobe ataje wapi yalipo makaburi ya baba na mama yake? Naibu Kamishina wa Uhamiaji akataa kuweka wazi sababu za kumuita Askofu huyo.

Pia soma=>Askofu Mkuu Zachary Kakobe aitwa Uhamiaji Jumatatu kuhojiwa juu ya uraia wake


pic+kakobe.jpg


 
Back
Top Bottom