Ugumu wangu
JF-Expert Member
- May 6, 2021
- 1,685
- 3,549
- Thread starter
- #101
Ahsante mkuu kwa swali hili japo sio mchumi Ila naweza kujibu tu kutumia akili za kawaida,Hongera!
Mwenyezi MUNGU akutie nguvu katika yote unayopitia.
Swali nje ya mada.
Umefanya kazi Mining (GGM) na sasa unafanya na Serikali.
Ni sehemu gani Serikali inapofeli katika sekta ya madini.
Kwa maana hadi sasa Sekta ya madini haijaonekana kuisaidia nchi ktk uchumi.
Lakini pia hata maeneo yote yenye madini wananchi wake bado maisha yao ni taabu. (Afya, Elimu na Miundombinu).
Katika hili Wala sio serikali inakwama Bali Kuna kikundi Cha watu wachahe na tuliowapa dhamana ya nchi na kuwaamini lakini wamejimilikisha wenyewe na familia zao.
Leo hii huwezi kuniambia hata Kama huna utaalamu wa kuchimba madini yako mwenyewe ndio uingie mkataba mibovu inayotuumiza na kuchia Mali zote kuondoka na sisi kubakiwa na mashimo tu, Hebu fikiria Leo bado tunaambiwa hakuna mtanzania anaeweza kuwekeza kwenye secta ya madini maana ni gharama huu ni uongo mkubwa, mzee Mengi tu mwenyewe alikuwa na uwezo Ila basi tu Tanzania hii hakuna wa kuikomboa ni mpaka sisi wenyewe siku moja tuamue ndipo tutapata Uhuru kamili wa nchi hii.
Japo Kuna watanzania wachache waliamua kutoa maisha yao kuisema kweli na mwisho wa Siku watanzania wenyewe tunaishia kuwakatisha tamaa nao Kama binadamu wengine wanachoka na kuamua kuunga juhudi ili nae ale na Familia yake😭😭😭 Mungu alitupa Tanzania nzuri Ila sie wenyewe tumeshindwa kujitambua.
Fikiria leo wanaombeza Lissu na kunitukana matusi yote, ulishawahi jiuliza Leo nchi hii tungeamua kuwatumia watu Kama hao tungekuwa wapi????
Naomba kuishia hapa nikiwaza nashindwa kuelewa daima🤐🤐🤐🤐