Kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa matumaini ya kupata msaada wa elimu

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,685
3,549
Member wa JamiiForums wote nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo aliekufa msalabani kwa ajili ya uovu wangu.

Leo nimependa kushare kidogo kuhusu historia ya maisha yangu inaweza kuwa funzo kwa mwingine pia.

Mara baada ya kumaliza darasa la Saba katika shule moja ya msingi mkoa wa Singida dc nilibahatika kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya wavulana Tabora school, kwa bahati mbaya nilizaliwa katika familia ambayo bado haikuwa inatambua umuhimu wa elimu pamoja na ilikuwa na uwezo wa kunisomesha lakini haikuwa hivyo.

Mimi ni mtoto wa mwisho Kati ya watoto Tisa kutoka kwa baba mmoja na Mama mmoja hivyo nilikuwa napendwa sana kama mtoto wa mwisho na ndugu zangu wengine wapatao wanne walifaulu vizuri kwenye shule nzuri ambazo leo zinaitwa special school lakini wazazi waligoma kabisa kuwasomesha wakiwa na Imani wataenda kupotea, hivyo nami nikaunganishwa kwenye kundi hilo kuwa nitaenda kupotea na hivi ikizingatiwa Mimi ni mtoto wa mwisho na wazee wananipenda sana.

Baada ya kuomba ushauri kwa kaka zangu nao pia waligoma kabisa kunipa ushauri wowote na zaidi ya kuniambia kaa nyumbani wewe ndio utawalea wazazi na kuwatunza, nahisi kwa wale mliokulia Singida mnajua vizuri mtoto wa mwisho ndio mwenye jukumu la kubaki na wazazi kwa kipindi hicho,

Basi baada ya majibu hayo moyoni mwangu palikuwa na wingu zito la mawazo huku nikishuhudia wale tuliosoma wakiwa kwenye haraki za kujiandaa kuripoti shuleni na hasa marafiki tuliokuwa karibu sana na wengine walikuwa wa shule jirani na tulikuwa tukifanya mitihani ya ujirani mwema na kushindana kwa nguvu kubwa, pamoja na yote hayo sikuwa na njia nyingine ya kufanya.

Kuna siku nikiwa nachunga nikajiwa na wazo kwanini nisitafute shule za mashirika ya kidini niende kujieleza naweza pia kupata msaada wa kusomeshwa na ndugu wakiona juhudi zangu wanaweza kuamua kuanza kunipa msaada,
baada ya kupata wazo Hilo huku siku mbili nyuma nilisikia story kuhusu shule moja ya sekondari inamilikiwa kanisa la kilutheri Tanzania na huwa inatoa msaada hasa kwa watoto yatima na washio katika mazingira magumu.

Baada ya kupata wazo Hilo nilipanga safari ya miguu kwenda shule ya sekondari Iambi na mfukoni nikiwa na hela ya kula Kama elfu tatu nilitoka asubuhi bila kuaga kwa mtu yeyote na nilifanikiwa kufika shuleni hapo saa 6 hivi mchana na nikapokelewa na mwalimu Mpuni nikamweleza sababu ya Mimi kuja hapo, akanichukua na kunipeleka kwa mkuu wa shule hiyo Mchungaji Elirehema Nkungu.

Mkuu huyo wa shule alinambia naweza kusaidiwa kwa kulipiwa ada nusu ikiwa nitafanya mtihani wao vizuri, Basi niliomba niufanye na nilipelekwa kwenye chumba Cha darasa nikiwa mwenyewe Somo la kwanza likiwa ni hesabu na baada ya kuuona mtihani kwa sababu hesabu pia ilichangia Mimi kupangiwa Tabora school niliuona mtihani wa kawaida sana nilipewa Lisa na nusu lakini ndani ya dakika 45 nikaufuta , nikaletewa tena wa Lugha nao kidogo nikamaliza nikatolewa nje kupata chakula nikapewa chakula na mwl El huyu ni mdada alikuwa anajitolea.

Baada ya kurudi kwenye paper la maarifa nalo mda kidogo nikalifuta na ikawa mwisho nikaenda kusubiri matokeo na baada ya kuitwa kwanza mkuu wa shule alifurahi sana na kunipongeza nikiwa nimepata hesabu zote pamoja na mitihani wa maarifa nao nimepata zote, Lugha tu ndio Kati ya maswali 50 nilipata 46 nikiwaachia 4 tu.

Baada ya matokeo hayo nikapewa barua yangu ya kuchaguliwa na kuibeba kwa furaha na ahadi ya kulipiwa ada nusu nikijua kiasi kilichobaki naweza kuwashawishi wazazi na kaka zangu kunisaidia, nikarudi home nilifika nyumbani saa 5 usiku pamoja na kupata lifti ya baiskeli baba aliniuliza ulikuwa wapi mpaka mda huu nikamwambia nilikuwa kwa rafiki zangu nikajikuta nimechelewa so sikutaka kumwambia ukweli maana alikuwa ameonja kidogo hivyo nikaona nitamweleza kesho.

Itaendeleaa..........
 
Inaendelea....

Baada ya kulala kesho yake asubuhi nikawahi kumwita Kaka maana yeye ndio anajua kusoma nikamkabidhi barua ile kwa furaha akaisoma mbele ya wazazi na kutoa kwa kilugha ili wazizi waweze kuelewa vizuri, baada kumaliza kuisoma akaniuliza ulienda lini huko nikamwambia Jana nilienda, Baba akadakia nakwambia huyu mdogo wako anataka atufilisi yeye anataka asome ataenda wapi mbona mtoto wa Fulani yupo tu, yeye akae alime alizeti apate hela na tumlipie mahali aoe apate mke.

Baada ya maneno hayo nililia nikaiona dunia imebana kila sehemu, Basi niliamua kwenda kwa Kaka mwingine kumweleza yeye kidogo akanifariji akasema nitakuja home kuongea na wazee,

Baada ya kuja Kaka mwingine home kaja kaongea na wazee sana wazee wakakubali japo kwa shingo upande, wakakubali kuuza ng'ombe wawili nikanunuliwa sare za shule na madaftari na siku ya kufungua shule nami nikafika shuleni hapo, nikasoma kwa bidii kweli kweli Kama mnavyojua kipindi hicho mpaka muanze masomo kamili ni mwezi 3 miezi yote mnafudishwa English course tu na masomo kidgo, baada ya hapo tukafanya mtihani nikafaulu vizuri sana.

Kabla ya kufunga shule kulikuwa na michango sijalipa Sasa natakiwa nilipe huo mchango ndipo niruhusiwe kufanya mitihani wa mwezi wa 4 na kufunga shule, nikaomba ruhusa ya kwenda home kupewa mchango ilikuwa Kama elfu 15000/ hivi nilifika nyumbani nikawaeleza nilichokutana nacho Basi tu.

Kwanza nilipigwa mkwara Mara tulikwambia unataka utufilisi Mara kusoma huwezi na maneno mengi ya kejeli hasa kutoka kwa Kaka zangu ambao ndio niliwategemea kwa asilimia kubwa kuwashauri wazee kwa sababu wao hawajui chochote kinachohusu elimu, mpka kufikia hapa nikakosa matumaini ya kurudi shuleni tena mbaya zaidi baba akienda kunywa anarudi na maneno kibao kuwa nataka kumwibia Mali zake na matusi juu.

Jambo Hilo lilinikera sana niliamua kutoroka nyumbani na kwenda kwa mjomba wangu kukaa huko, kabla sijaondoka nyumbani nikawa nimepata ushauri kwa mama kuwa Kuna binamu yangu aliwahi kusema kuwa huyu kijana akimaliza shule ya msingi aje marerani nitamtafutia kazi anaweza kupata pesa nzuri, baada ya mama kunipa wazo Hilo akanipa na karatasi ya anuani wapi nitafikia na kila kitu.

Baada ya kufika kwa mjomba huku nikiwa na mawazo mengi sana wazo jingine likanijia kuwa Nina binamu yangu mwingine yupo dar ni mwanajeshi yeye na mke wake kwa Nini nisiende huko huyu naona atakuwa mwelewa zaidi nikimwambia anisomeshe anaweza nisaidia, wazo Hilo likapata kibali kwenye moyo wangu nikapanga na siku ya kuianza safari Ila nauli Sina itakuwaje!.



Itaendeleaa......
 
Inaendelea.....

Siku ilitimia na kuanza safari, safari ya kwanza ilianzia Singida mjini baada ya kutoka kijijini kwa msaada wa baiskeli na rafiki yangu huko ujombani, asubuhi saa 12 mbili kamili safari ilianzia stand ya mabasi Singida mjini kujitafuta dar kwa miguu siku hiyo nilitembea Hadi karibu kukaribi kidogo kufika Ikungi Ila nilikuwa nimechoka sana sijala na hata kunywa maji sijanywa.

Nililala nje kwenye mawe nikajificha mpaka asubuhi kesho yake saa 10 maana nilikuwa na saa nikaanza safari Hadi Isuna saa 11 nikafika nikakuta Gari imemwaga mahindi wanazoa na kuweka kwenye mifuko nikaomba niwasaidie wakakubali nikawasaidia hapo tulifanikiwa kumaliza kazi ya kupakia mpaka saa 2 usiku mzigo ukafungwa vizuri na tayari kwa safari mie nikazunguka kwa dereva nikamwomba lift Hadi Monyoni, akaniuliza Manyoni unaenda kufanya Nini nikamdanganya nimefukuzwa nyumbani kwa sababu ya kugoma kuacha shule dereva alinambia Sasa Manyoni unaenda kwa Nani nikamwambia Nina ndugu hapo mjini.

Baada ya mahojiano hayo dereva aliniuliza kwanza umekula nikamwambia tangu Jana hata maji sijanywa akaniambia mbona hukusema mapema utakuja kufa wewe akanitukana kidogo akanipa mkate na soda nikala na maji kanipa nikanywa haswa nikapata nguvu, safari ikaendelea kumbuka barabara kipindi hicho ni vumbi tupu tukaondoka mpka kesho saa 2 mbili asubuhi ndio tunafika Manyoni mjini dereva akaniuliza kwa ndugu yako ni Manyoni mjini au kijijini nikamwambia kijijini Basi hakuniuliza Kijiji gani maana hapa angeniuliza tu nilikuwa sijui chochote maana Manyoni yenyewe ndio kwanza naijua.

Baadae nikashuka kwenye Gari akanipa elfu 3 Kama nauli yangu wao wakaendelea na safari nami huyo tena kwa miguu kufuata road Hadi kufika Solya pale mlima Saranda ilikuwa jioni mida Kama saa moja hivi nikauliza kwa balozi wapi nikaonyeshwa nikafika bahati nzuri nilimkuta balozi mwenyewe nikamwambia jinsi nilivyotoka nyumbani japo kwa kumdanganya kuwa nimefukuzwa na hapa naenda kwa Kaka yangu ni mwl.shule ya sekondari Mazengo ,niliamua kumdanganya hivyo ili nipate hifadhi na shule naijua tu kwa jina kweli nikapokelewa vizuri nikapewa maji ya kuoga na chakula nikatandikiwa kitanda nikalala hapo.

Kesho yake asubuhi palipokucha nikaambiwa na mwenyeji wangu tuende barabarani tunaweza pata msaada lift ya magari makubwa Hadi dodoma

Itaendeleaa.....
 
Inaendelea....

Baada ya kulala kesho yake asubuhi nikawahi kumwita Kaka maana yeye ndio anajua kusoma nikamkabidhi barua ile kwa furaha akaisoma mbele ya wazazi na kutoa kwa kilugha ili wazizi waweze kuelewa vizuri, baada kumaliza kuisoma akaniuliza ulienda lini huko nikamwambia Jana nilienda, Baba akadakia nakwambia huyu mdogo wako anataka atufilisi yeye anataka asome ataenda wapi mbona mtoto wa Fulani yupo tu, yeye akae alime alizeti apate hela na tumlipie mahali aoe apate mke.
Endelea mkuu
 
Inaendelea.....

Baada kukakaa barabarani na mwenyeji wangu mda kidogo Kama saa 3 hivi nikapata lift na mwenyeji wangu kanipa elefu 2 so kulingana na huu usafiri niliombewa na mwenyeji wangu sikupata kuulizwa maswali na safari ilianza toka Solya kwenye kitovu Cha Tanzania kulipia Hadi dodoma nilifanikiwa kufika Dom saa 12 jioni huku nikiwa nashangaa tu sina hili Wala lile nikashushwa na baadae nikatafuta eneo la kwenda kulala nahisi nililala pale kwenye hosptali Fulani Dom Kuna mlima Fulani Kuna mawe nikala Hadi asubuhi na kesho yake nikatafuta eneo nikanywa chai na kuanza safari mpka njia panda Chamwino Bugiri saa 10 nikapita kwenye mji wa mtu kuomba maji ya kunywa ili niendelee na safari.

Itaendeleaa.............. Jamani samahani kidogo huku ndio Kuna kucha hivi ngoja nianze kujiandaa kwenda job nitarudi mda mwingine
 
Huku ndio kuna kucha kwani upi wapi mkuu?
Singida vijiji ulivyotaja navielewa ngoja tuone mwisho
 
Naomba tuendelee na story.....

Nikiwa Bugiri hapo jioni kabisa nimeenda nyumbani kwa mtu kuomba maji ya kunywa, nilipewa maji ya kunywa nikanywa vizuri nikaaga na kuanza kuondoka, nilipiga hatua Kama 4 hivi mwenye Nyumba akaniita we mtoto nikageuka akaniambia njoo kwa hofu nikarudi huku natetemeka najisemea labda kanifahamu au nimekosea wapi?.

Wakati bado najiuliza maswali hayo kichwani mwangu Basi yule jamaa akaagiza mtoto alete kiti na kumwambia mke wake aangalie Kama Kuna kiporo akipashe atengeneze na mboga alete, nilipewa kiti nikakaa na baada ya mda yule mwenye mji akaniambia kijana Mimi ni mtembeaji sana hivyo najua vizuri mtu mwenye shida kweli najua hata wewe hapa umetoka mbali sana na huenda pia unaenda mbali sana, hivyo naomba uniambie umetoka wapi unaenda wapi, nami bila kuchelewa nilimwambia nimetoka Singida nimefukuzwa nyumbani kwa sababu nilitaka kwenda shule Ila wazazi hawataki na hapa nilipo naenda Morogoro Kuna Kaka yangu ni mwl Mzumbe sec, kumbuka hapa kuwa nadanganya tu ili niwe napata msaada wa kusogea japo kidogo.

Baada ya maelezo hayo yule jamaa alinihurumia sana akaniambia kaa hapa Leo nitaenda kuongea na balozi pia ili Kama ikiwezekana tuchange japo kidogo upate nauli hivyo Leo utalala hapa kwangu, nikweli nililala hapo na kesho yake nikapelekwa kwa balozi nikaulizwa maswali nikajibu vilivyo wakaambizana huyu ni mtoto mdogo hatuwezi kuwa na mashaka nae hivyo apmzike hata week moja hivi tuandae nauli na yeye mchoko uishe theni tumsindikize aende.

Basi nilikaa week nzima hapo ikafika siku nikapewa nauli kutoka hapo Hadi Morogoro na 2000 ya akiba, niliondoka na Basi mpaka Morogoro na baada ya kushuka Moro ilikuwa saa 7 mchana niliulizia Gari za kwenda dar na nauli nikaambiwa Gari zipo na nikiangalia nauli yangu inatosha kabisa hivyo nikaenda kukata ticket kwenye Basi nikatulia , kumbuka hapa Sina kitu chochote zaidi ya nguo nilizovaa tu Sina nguo nyingine, ikafika mda Basi likaondoka safari ikaanza huku nikiwa nashangaa sana njiani kumbuka nimetoka bushi huko nikafika dar Kama saa 1 usiku kwa maana Kuna sehemu Gari ilisimama mda mrefu sana, baada ya kufika dar ubungo hapo nikashushwa hapo kwenye stand ya daladala ya zamani huku nikiwa naona maluwiluwi tu yaani naona Gari nyingi full ushamba yaani ni hatari tupu.

Baada ya hapo nilifanikiwa kuvuka upande wa pili nikatafuta mtu wa makamu hivi kasimama na Gari ndogo nikamuomba naomba unielekeze mabibo jeshini, kumbe yule jamaa ni driver tax akaniambia una sh ngapi hapo nikaduwaa yaani kuuliza tu njia naambiwa unashilingi ngapi? , Basi nikamwambia Sina hela nakuomba tu unielekeze , akaniambia umetoka wapi nikampa story nzima akasikitika hapo alafu Kuna jamaa zake hapo pembeni wakamwambia Sasa Kama analijua jina la ndugu yake ukimfikisha hapo naamini utalipwa na kama hata kulipa Basi labda jamaa awe si muungwana na utakuwa umetoa sadaka kumsaidia huyu mtoto.

Baada ya jamaa kupewa maneno hayo na rafiki zake akakubali kunipeleka mpaka mabibo tukafika sijui ndio kulikwa na geti hapo maafande wapo jamaa kasimamishwa hapo na kuulizwa unaenda wapi na kwa Nani dereva kajieleza hapo wakaniuluza vipi dogo una ndugu yako humu anaitwa Nani nikawaambia anaitwa baba Fulani maana ndio jina maarufu kusema tu hivyo wakamwambia dereva huyu kafika tayari we mshushe hapa tunampeleka wenyewe jamaa akalipwa hela yake pale na wale mapoti jamaa kasepa mie nikabaki hapo getini mda kidogo Kuna Gari ya Jeshi ikafika hapo naona jamaa akasema unaiona hii Gari huyu jamaa pia ni mtu wa kwenu hivyo tunakukabidhi kwake maana yule baba Fulani unaemtaka wewe ambae ni ndugu yako hap ameshahama yupo gongolamboto, moyoni nikasema sawa tu kidogo yule mjeda akashuka kwenye Gari na kupigiwa saluti hapo wakamwambia mkubwa Kuna ndugu yenu hapa, jamaa kaniita na kuniuliza unaitwa Nani nikamjibu na kumpa story kidogo akanihurumia kaniambia pole sana karibu nyumbani wewe hapa umefika na huyo mjinga unaemtafuta atakuja kukufuata kesho usijali huyo ndugu yako kwangu ni dogo tu, kumbe ni mtu na rafiki yake hivi.

Itaendeleaa......
 
Inaendelea.....

Nilipokelewa vizuri kabisa, nikapewa huduma zote nikapewa na nguo ili nibadilishe zingine nifue ikawa hivyo kesho yake Kama saa Tisa hivi binamu yangu kaja kunifuata hapo, alipofika tu maswali kibao na mitusi kidogo hapo nikalegea mpka yule jamaa yake akamwambia kumbuka huyu ni mtoto kwa hiyo sio vizuri unavyomfokea kwa sababu katoka Nyumbani kuja kukuomba msaada Bora uongee nae kwa upole tu,
Kumbukeni huyo binamu mwenyewe tangu kuzaliwa hatujawahi kuonana nae hata kidogo nilijipeleka kwa kusikia tu so ndio mwanzo wa kufahamiana na ndio nakutana na hali hiyo kiukweli niliumia sana sana.

Basi akanichukua tukaingia kwenye Gari la kijeshi huyoo mpaka pale karibu na mazizini kwa nyuma kidogo ukiwa unatokea Mombasa janction, tukifika nyumbani mke wa jamaa ni mkarimu kweli nae pia ni mjeda nikapokelewa vizuri nikaonyeshwa na chumba changu Cha kulala siku zikawa zinayoyoma hivyo sioni dira yeyote, mwisho nikavunja ukimya nikamwambia binamu vipi kuhusu ombi langu?

Kiukweli hapo ni Kama nilimchokoza nilipewa mitusi kama yote hivi na kuambiwa kwanzia leo kazi yako ni kulima mchicha hapo na kuutembeza , kweli kesho yake nikaonyeshwa eneo la kulima mchicha nikaanza kulima na mchicha ukawa vizuri nikaanza kuuza natembeza kwenye besen hivi mpaka nikachoka, nilipochoka kubeba beseni hela nakabidhi zote sipewi hata Mia nikaona isiwe tabu wakati nazungusha mchicha wangu nilikutana na jamaa ni fundi viatu na kubrashi viatu ni mtu wa Nyumbani Singida, alinambia ukipenda uje nikufundishe hii kazi kidogo unaweza kuwa unapata hela ,Basi siku moja nilijifanya naumwa hivyo sikwenda kulima shmba langu la mchicha na nipopata chance ya kutoka nilienda moja kwa moja kwa yule jamaa pale mazizini kabla ya lami kwenye Duka la Arawa mbele yake kulikuwa na kibanda Cha kushonea viatu na kuziba pancha baiskeli na kubrashi viatu jamaa mfupi anaitwa Pea kwa wenyeji wa pale nahisi mnamfahamu vizuri.

Baada ya kumwona jamaa nikamweleza Hali halisi ya Mimi kuchoka kuuza mchicha jamaa akaniambia ngoja nikutafutie mtu ambae mtaishi geto moja nae alafu wewe utatoka huko uliko na kwenda jamaa nikaeona atafaa kukaa na wewe alafu utaendelea kuja kujifunza kufanya hii kazi hapa na kwa sababu unajifunza Basi mie nitakuwa nakulipa elfu moja kila jioni chai ya asubuhi na chakula Cha mchana utakula hapa kijiweni kwa gharama zangu.


Itaendeleaa......
 
Inaendelea......

Baada ya makubaliano hayo na jamaa ilifika siku nikaamua kuondoka kwa binamu yangu na fundi viatu tayari alinitafutia sehemu ya kulala kwa jamaa mmoja ambae ni mtu wa Nyumbani pia anafanya kazi ya ulinzi kwenye maja ya makampuni ya kimataifa, na jamaa pia alikuwa ametoka kwenye mazingira magumu sana na ndio kaanza kazi hivyo alikuwa anaishi kwa kujibana na kwa malengo makubwa sana, na chumbani hakukuwa na kitu chochote zaidi ya mkeka na shuka na neti tu basi.

Basi tukawa tunafarijiana sana na jamaa alikuwa anaenda lindo la mchana kwa hiyo usiku tupo wote jamaa ni mtu wa maombi sana tukawa Kama mayatima Fulani hivi tunapeana faraja sana, na Mimi kichwa kulikuwa chepesi sana kujifunza kushona viatu na kubrashi vizuri sana hadi nikapendwa na wazee Kama sipo Mimi Basi na wao hawatoi kazi kwa mwingine.

Nilikaa hapo mpaka mwezi wa tano nakumbuka siku moja ilikuwa jmosi akaja mzee mmoja na Landcruicer akaipaki mbali na akaja na viatu nikambrushia vizuri huku akinipiga maswali ya hapa na pale Mara kwenye maisha yako unapenda Nini nikawa nafunguka tu Hadi kumpa historia yangu ya Mimi kutua hapo jijini, Basi mzee alisikitika sana kaniuliza kwa hiyo bado una nia ya kusoma? Nilimjibu Tena bado nia ninayo sana na napenda sana kusoma unaona hata hapa pia Nina vitabu huwa najisomea kidogo kidogo Kama hakuna wateja.

Yule mzee ikafika mda wa jioni akaniaga kaondoka bila hata kunilipa ujira wangu kweli moyo wangu uliumia sana , Ila sikuwa na jinsi baada ya siku mbili tena yule mzee kaja mida ya jioni na kandambili pea tatu zimekatika akaja nikamshonea bila kinyongo na story Kama kawaida tena kwa furaha nikiamini Leo nitalipwa hela nzuri pamoja na ya siku ile, lakini ilipofika mda wa kuondoka aliniaga tu fasta kasepa bila kulipa siku hiyo Hadi machozi yalinitoka lakini nikamwambia Mungu ahsante kwa yote.

Baada tena Kama siku tatu siku ya jmosi mzee yule yule alikuja na viatu pair tatu na ndala zimekatika na viatu vingine ilikuwa ni vya kubrashi tu Basi nami bila kinyongo nilichangamkia kazi yake vizuri tu Tena kwa furaha bila kuonyesha kinyongo, baadae kaniuliza leo utakunywa chai gani nataka tunywe wote nikamwambia nataka supu ya kuku mzee wangu, kumbuka hapa nataja hivyo lengo langu ni kumkomoa huyo mzee, kweli mzee aliagiza supu kwa mama lishe hapo karibu tukanywa wote na story zikaendelea nami napiga kazi Kama kawa , ilifika saa 7 nikamwambia naomba niende nyumbani kidogo akaniuliza kufanya Nini nikamwambia naenda kufanya maombi natamani Mungu wangu asikie kilio changu, Basi yule mzee akaniuliza unasali wapi nikamwambia ni TAG ukonga kwa mchungaji Kimaro ni marehemu kwa Sasa huyu mchungaji, akaniambia sawa nenda akakujibu hitaji la Moyo wako niliondoka nikafika zangu geto nikapiga magoti na kuomba sana Kama Lisaa na nusu hivi baadae nikamaliza nikaanza kurudi kazini kwangu.

Nilipofika kazini nikamkuta mzee yupo ananisubiri nikafika tukaendeleza story kaniuliza hivi ikitokea mtu anakurudisha shuleni pale ulipofaulia unaweza kurudi na kuendelea na masomo nikamwambia ndio naweza na tena nahiidi kufanya vizuri sana kwenye masomo haijalishi mda umepita mwingi, akaniuliza kwa Nini unajiamini hivi nikamwambia kwa sababu napenda sana kusoma, Basi akaniambia leo hapa unaweza kutoka kidogo nikamwambia ndio naweza kutoka mwenzangu si yupo, basi akanichukua mpaka kwa fundi nguo nikapimwa na kurudi kazini kwangu, ukweli ni kwamba hapa kidogo nilijiuliza maswali mengi mno je anataka nishone nguo za kuvaa tu au ndio za shule? Maswali mengi hayakuwa na majibu.


Itaendeleaa........
 
Back
Top Bottom