Kutoka Selecao mpaka La Albiceleste – yafahamu majina ya maarufu ya timu 32 zitakazocheza Kombe la Dunia 2022

Dibwi Method

Member
Nov 22, 2021
31
28
Na Godian Method

Kombe la Dunia ndiyo michuano mikubwa zaidi ya kimataifa katika mpira wa miguu, ambapo watu, Sanaa na tamaduni za mataifa mbalimbali huungana.Michuano hii ya soka, hudumu kwa muda wa mwezi mmoja, tukishuhudia mataifa bora 32 yakichuana vikali katika jitihada za kuhakikisha zinatwaa kombe hili adhimu zaidi kuliko yote katika ulimwengu wa soka.

Karibu kila timu ya soka huwa na jina la utani ambalo kupitia majina hayo, zinapatikana historia na chimbuko la timu hizo. Kila jina huwa na hadithi Fulani ndani yake na kupitia majina hayo, mashabiki hupata hamasa zaidi kutumia majina hayo ya utani kuliko majina rasmi ya Mataifa yao.

Taifa lenye mafanikio zaidi kisoka (Brazil), lina jumla ya majina ya utani sita. Timu ya taifa ya Argentina hufahamika kama La Albiceleste (anga la kijani na buu) kutokana na rangi za bendera yake ya taifa. Ureno yake Cristiano Ronaldo, hufahamika kama The Navigators (Mabaharia), kutokana na historia yao ya kufikia maeneo mengi duniani kwa njia ya maji. Uingereza hufahamika kama The Three Lions (Simba Watatu) kama ilivyo kwenye nembo ya Taifa hilo.

Australia al-maarufu Socceroos, lilitengenezwa na mwandishi wa habari kutokea Jijini Sydney aitwaye Tony Horstead. Alitaka kuihusisha timu ya Taifa ya Australia na kivutio cha utalii maarufu cha nchi hiyo (Kangaoo). Ili kulifanikisha hilo, neon soccer na kangaroo yaliunganishwa na kutohoa neno soccer-roo.

Iran al-maarufu Melli ni neno la Kipersia lenye maana ya ‘Timu ya Taifa’. Pamoja na hilo kuna majina mengine kama ‘Shiran e Iran’ (Simba wa Iran), ‘Shirdelan’ (Mioyo ya Simba) na ‘Princes of Persia’ (Wana wa Mfalme wa Persia).

Japan al-maarufu Samurai Blue (Mashujaa wa blue), timu ya Taifa ya Japan hufahamika kama Masamurai wa bluu, wakihusishwa na historia ya nchi hiyo.

Qatar al-maarufu The Maroon (Damu ya Mzee), hii ni kutokana na rangi ya bendera ya taifa hilo.

Saudi Arabia al-maarufu Al Akhdar (Wana Kijani), Pia wanafahamika kama ‘as-suqur al-akhdar’ (Kozi-kipanga). Jina lao la tatu ni ‘as-suqur al-araiyyan’ (kozi-kipanga wa Arabuni).

Korea Kusini al-maarufu ‘Taegeuk Warriors’ (Wanajeshi wa Taegeuk), pia hufahamika kama ‘The Reds’ (Wekundu) na ‘Lions of Asia’ (Simba wa Mashariki ya mbali). Taegeuk ni alama inayopatikana kwenye bendera ya taifa hilo.

Cameroon al-maarufu ‘Les Lions Indomtables’ (Simba asiyeshindwa).

Ghana al-maarufu ‘Black Stars’ (Nyota Weusi), jina hili limetokana na nyota nyeusi inayopatikana katikati ya bendera ya taifa hilo.

Morocco al-maarufu ‘The Atlas Lions’, jina hili limetokana na simba waliowahi kupatikana katika taifa hilo ambao pia alikuwa ni mnyama wa taifa hilo. Kwa sasa simba hao wametoweka.

Senegal al-maarufu ‘Lions of Taranga’ (Simba wa Taranga), Taranga ni neno la Kisenegali lenye maana ya ‘Ukarimu’.

Tunisia al-maarufu ‘Eagles of Carthage’, carthage ni jamii ya kale ya taifa hilo na inahusishwa kuwa jamii ya kwanza kustaarabika. Ndege tai yuko kwenye nembo ya shirikisho la soka la Tunisia.

Canada al-maarufu ‘The Reds’ (Wekundu), taifa hili linajulikana kwa jina hili kutokana na rangi ya jezi (ya nyumbani) ya taifa hilo. Wanafahamika pia kama ‘Maple Leafs’ kutokana na bendera ya taifa hilo yenye alama ya jani ndani yake.

Costa Rica al-maarufu ‘Los Ticos’, jina hili limetokana na utofauti wa kimatamshi ya lugha ya Kihispania tofauti na Mataifa mengine yanayozungumza lugha hiyo.

Mexico al-maarufu ‘El Tri’, jina hili linatokana na rangi tatu zilizotawala bendera ya Taifa hilo kutoka Marekani Kaskazini.

Argentina al-maarufu ‘La Albiceleste’, hii ni kutokana na rangi ya mistari ya jezi za timu hiyo (bluu na nyeupe)

Brazil al-maarufu ‘Selecao’, ni neo maarufu la Kireno lenye maana ya wachezaji waliochaguliwa.

Ecuador al-maarufu ‘La Tri’, jina hili limetokana na rangi tatu zinazopatikana kwenye bendera ya taifa hilo.

Uruguay al-maarufu ‘La Celeste’ (Anga la Bluu), jina hili limetokana na rangi ya jezi za timu ya taifa hilo.

Belgium al-maarufu ‘Die Roten Teufel’ (Mashetani Wekundu), jina hili lilipendekezwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pierre Walckiers kutokana na rangi ya jezi za timu hiyo za mwaka 1906.

Croatia al-maarufu ‘Kockasti’, Luka Modric na wenzake wanafahamika kwa jina la ‘Kokhasti’ lenye maana ya ‘nyakati nzuri na mbaya’ kama mpangilio wa rangi ulivyo kwenye bendera ya taifa hilo.

Denmark al-maarufu ‘Da Rod-Hvide’ (rangi nyeupe na nyekundu), hii imetokana na rangi za jezi za kwanza za timu hiyo.

Uingereza al-maarufu ‘Three Lions’ (Simba Watatu), Shirikisho la Mprira wa Miguu la Uingereza hutumia nembo ya simba watatu na hivyo timu ya taifa hilo ikaitwa Simba watatu.

France al-maarufu ‘ Les Blues’ (Wana Bluu), jina hili limetokana na rangi ya bluu ya jezi za taifa hili kutoka Barani Ulaya.

Ujerumani al-maarufu ‘Nationaleif’, jina hili linamaana ‘Kumi na moja wa taifa’.

Uholanzi al-maarufu ‘Oranje’ (Manjano), jina hili limetokana na rangi ya uzizi wao ya nyumbani na nembo ya KNVB, ambayo ni nembo ya shirikisho la soka nchini hapo.

Poland al-maarufu ‘Biato-czerwoni’, hii ni lugha ya Kipolish na maana yake ni ‘Nyekundu na nyeupe’

Portugal al-maarufu ‘Os Navegadores’(Mabaharia), jina hili limetokana na historia maarufu ya taifa hili ya kuwa la kwanza kufika katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa njia ya maji.

Serbia al-maarufu ‘Orlovi’ (Ndege tai), jina hili limetokana na ndege tai mwenye vichwa viwili anayepatikana kwenye nembo ya taifa la nchi hito.

Hispania al-maarufu ‘La Roja’, neno hili humaanisha ‘Mwekundu’. Pia wanafahamika kama ‘La Furia’ (Wenye Hasira).

Switzerland al-maarufu ‘Rossocrociaati’ wakiwa na maana ya ‘Msalaba Mwekundu’. Pia wanafahamika kama ‘Nati’, neno hili ni la Kiswiss na lina maana ya ‘Timu ya Taifa’

Wales al-maarufu ‘The Dragons’ (Joka), wamekuwa wakijiita hivi kutokana na uwepo wa joka linalotema moto kwenye bendera yao ya taifa.

USA al-maarufu ‘Star Stripes’ (Mistari Nyota), Marekani wana jina lisilo na mbwembwe lililopatikana kutokana na bendera la taifa hilo na bendera ya shirikisho la mpira wa miguu la nchi hiyo. Pia wanafahamika kama ‘The Yanks’.

Chanzo: Goal.com
 
Mbona siioni Tanzania au kichwa cha mwendawazimu siyo jina letu la utani?
Hiyo ni kwa timu zinazoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu (Qatar 2022) kaka!
Siku tukikata tiketi ya kushiriki nitaandaa makala itayoijumuisha Tanzania kwa jina lake maarufu, ingawaje sina uhakika kama litafanana na hilo ulilolisema.
 
Hiyo ni kwa timu zinazoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu (Qatar 2022) kaka!
Siku tukikata tiketi ya kushiriki nitaandaa makala itayoijumuisha Tanzania kwa jina lake maarufu, ingawaje sina uhakika kama litafanana na hilo ulilolisema.
Aah kwani jina letu la utani ni lipi mkuu! Maana mi nlikuwa najua ni kichwa cha mwendawazimu nipe data zaidi!
 
Back
Top Bottom