Kutoka mzee wa vijisent hadi mtemi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka mzee wa vijisent hadi mtemi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfred Daud Pigangoma, Jun 18, 2012.

 1. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi!

  Hii inakaaje kwa wabunge wetu wa TZ kwa kujitambulisha kwa majina tofauti kila kukicha. Akimalizia hotuba yake mwenyekiti wa kamati Mh. Andrew J. Chenge amejitambulisha rasmi kuwa ni MTEMI CHENGE....

  Tutasikia majina mengi hivi sasa kama wengine wanajiita Dr. , Prof. ukizingatia hawana elimu ya kuwa hivyo....
   
 2. N

  Njaare JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nahisi ni mtemi maana ya mbabe. Anamaanisha kuwa kazushiwa mengi ila kayamaliza kitemi/kibabe na sasa mmempa uenyekiti wa kamati nyeti.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Wasukuma wa bariadi (Wanyantuzu) wana fursa ya kutuambia ukweli kwani mtemi hajichagui bali anachaguliwa..... kwa suala la chenge kuwa mtemi wa wasukuma bila kujali kuwa utemi na uchifu ulipigwa marufuku na Nyerere sio suala la kitaifa.

  Mtemi Chenge......matamu hapo inalipa kwa mtu anayependa kujikweza.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ametutumia mesage kwamba hatumuwezi...tukae kimya kama hatuoni vile
   
 5. m

  mamajack JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Shibe imemzidia huyo,ngoja mambo yabadilike.
   
 6. Sunday Ngakama

  Sunday Ngakama Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Andrew Chenge anatoka katika familia ya mtemi Ndatulu. hivyo huo utemi wake huenda ukawa ni wa halali kabisaa. ingawa sijawahi kusikia habari za uteuzi wake.
   
 7. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,524
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  ameshiba madaraka amelewa pesa zetu sasa anatutangazia utemi kweli sisi wadanganyika!
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Kazi kwelikweli!INASHANGAZA SANA KUWA WAINGEREZA WANAKUWA NA UCHUNGU NA NCHI YETU KULIKO SISI WENYEWE!yaani wao wametusaidia kukusanya ushahidi wote dhidi ya ufisad wa chenge,sisi tumeishia kumpa kamati ya uchumi!mwache ajiite mtemi,maana ametushinda watz!
   
 9. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ni matusi kwa watanzania-watanganyika kwa huyu mtu kishika nafasi hiyo ya uongozi ni bora ccm wangempa nafasi ya harakati za kujivua gamba ccm.mungu ibariki tanzania.
   
 10. J

  Juma Kilaza Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  makubwa
   
 11. n

  nhassall Senior Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni mtemi haswa maana kila jambo baya juu yake kapangua kuanzia ufisadi mpaka kuua kwa kugonga na gari, nafikiri anatamani tu hata ajiite jina zaidi ya hilo, kwani anafikiri kafanikiwa sana kumbe anajidanganya tu
   
 12. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145

  Ni kweli, ni mmoja wa watoto wa aliyekuwa Mtemi Ndaturu lakini wakati akiwa serikalini (mwanasheria mkuu wa serikali) alikuwa hata haudhulii wala kuchangia vikao mbalimbali vya wanandugu wa kisukuma (Bulabo)
  Uamuzi wa kutaka kuwa mbunge wa Bariadi ndiyo ulimfanya akaanza kujihusisha na maswala mbalimbali ya wanandugu wa kisukuma (Bulabo) ili aonekane kuwa karibu nao ili kutimiza lengo lake la kuwania Ubunge. Kuna tetesi(hazijadhibitiswa) pia kama rushwa ilitumika miongoni mwa wazee wa kabila ili achaguliwe na kutawazwa kuwa mtemi wa Itirima kwa sababu wanandugu wengi walikuwa wanamuona kama hakuwa karibu katika maswala ya kimila.

  Mpambano wa Ubunge kati yake na Isaac Cheyo(mdogo wake na bwana Mapesa) ulikuwa mkali na uliimega jamii ya wanandugu wa kisukuma Bariadi (Bulabo) kwa sababu Isaac Cheyo naye anatoka katika jamii ya wanandugu hao na pia UDP kwa wakati huo kilikuwa ni chama maarufu katika eneo hilo na Mwenyekiti wake(john Cheyo) alionekana miongoni mwa wanandugu kuwa yuko karibu nao ukilinganisha na Mzee wa Vijisenti.

  Kwa habari zaidi soma hii habari kutoka gazeti la Tanzania Daima by Sitta Tumma.

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]Chenge asimikwa utemi


  na Sitta Tumma, Magu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, ametawazwa kuwa mtemi wa kabila la Wasukuma-Bagole, Kanda ya Itilima, wilayani Bariadi.
  Chenge alichaguliwa katika sherehe maarufu za kabila hilo, maarufu kama Bolabo, mwishoni mwa wiki, wilayani hapa, ambazo mbali na viongozi wa kimila, Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro, alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
  Baadhi ya watu waliokuwepo kwenye sherehe hizo, waliuelezea utemi wa Chenge kwa mtazamo tofauti, huku baadhi wakidai kaupata ili kuweka mambo yake sawa, na wengine wakidai anastahili kupata nafasi hiyo kwa kuwa ni miongoni mwa watu wa kabila hilo.
  Mbunge huyo ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri alisema, utemi huo ni karama aliyopewa na Mungu na kwamba wajibu huo ni sawa na daraja la kuunganisha jamii ya kabila husika.
  "Utemi niliopewa naweza kusema ni karama iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu! Kazi hii ya utemi ni nzito kwa sababu ina masuala yake yanayohusiana na mambo ya kimila pamoja na kuunganisha jamii ya kabila husika," alisema Chenge.
  Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Kandoro alitoa onyo kwa wakazi wa Wilaya ya Magu kuwa makini wasije kurubuniwa na kuuza mazao yao ya chakula kwa walanguzi kutoka nchi jirani za Uganda na Kenya.
  RC alisema kuwa ni aibu kwa mtu kuuza mazao yote na kukosa chakula nyumbani, na kwamba hali hiyo isiwepo, badala yake wananchi watunze chakula chao ili wasije kukiuza na baadaye kupatwa na baa la njaa na kuathiri maisha yao.
  "Kuna tabia ya baadhi ya watu kuuza mazao yao kwa walanguzi, kwa hali hii ni hatari kwa maendeleo ya familia.....walanguzi hawa waepukeni watawasababishia njaa kwenye familia zenu," Kandoro alionya.
  Sherehe hizo za kabila la Kisukuma, zilihudhuriwa na watu maarufu akiwemo Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mshauri wa Watemi, Jaji Michael Bomani, Mwenyekiti wa Watemi wa Wasukuma, Kanda ya Mwanza, Charles Kafipa, mmoja wa washauri wa Watemi Bujora, Jaji Thomas Mihayo, na viongozi watemi wengine kutoka mkoani Shinyanga.

  [​IMG]


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 13. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2014
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nimewahi kusikia pia kwamba anauhusiano na mtemi Mwanila'gha wa Lugulu Itilima na kwamba amerithi utemi baada ya mtemi Limbe. Inasemekana aliteuliwa na kusimikwa rasmi.
   
 14. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2014
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,492
  Likes Received: 25,309
  Trophy Points: 280
  hakuna uhalali wowote , chenge ni fisadi mkubwa na wala hana uadilifu wowote , aliwahi kuhukumiwa mahakamani kwa kuendesha gari akiwa njwii vibaya sana , tena bila leseni na kusababisha mauaji ya kimbari .
   
Loading...