Kutoka Mwanaspoti: Aussems: Nilipogoma kupangiwa kikosi shida ikaanza

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
7,354
13,015
ALISHTUKIA MAPEMA

Alipoulizwa amechukuliaje uamuzi wa
kufutwa kazi, Aussems alisema; “Ni
muda mrefu nilikuwa najua tutafikia
hatua hii kati yangu na Simba. Ni
muda mrefu walikuwa wanataka
kukata shingo yangu, namaanisha
kwamba kuna baadhi ya viongozi kila
mwezi walikuwa na malengo ya kutaka
kuniondoa hapa. Mwezi mpaka mwezi
hakukuwa na zuri ninalolifanya katika
uso wao, daima walikuwa
wakipambana kuhakikisha kazi yangu
hapa inaharibika.

“Unajua mimi sio kocha wa kunipangia
kipi cha kufanya hasa katika ufundi wa
soka, mfano kuniambia mchezaji huyu
anatakiwa kucheza au huyu hatakiwi
kucheza hii ndio ilikuwa akili yao sasa
nilipowakatalia wakatengeneza chuki
kwa muda mrefu, hivyo uamuzi huu
haukunishtua kabisa kwa kuwa
nilikuwa najua kwamba kuna watu
wanapambana kunitoa.”


MAISHA YALIKUWAJE SIMBA?

“Maisha yalikuwa mazuri wakati
tunaanza hapa na kila kitu kilikwenda
sawa. Kidogo maisha yalianza
kubadilika baadaye hasa msimu
uliopita wakati tukipata mafanikio.
Tuwe waungwana, inawezekana Simba
ilikuwa inajulikana hata Ulaya, ila kwa
kazi ya msimu uliopita iliifanya klabu
kujulikana zaidi. Watu walikuwa
wanazijua klabu kubwa za Afrika lakini
Simba haikuwa na jina kubwa.”
“Tulianza kwa kuhakikisha kwanza
tunakuwa na falsafa ya mpira wetu
hapa kwa kutafuta wachezaji
watakaoendana na falsafa hiyo.
Tulifanya kazi kubwa sana msimu
uliopita. Wachezaji walikuwa na ubora
wa juu kwa mchezaji mmoja mmoja
hadi timu nzima. Angalia mchezaji
kama Erasto (Nyoni), Kagere (Medie),
Okwi (Emmanuel), Chama (Clatous)
walifanya kazi kubwa sana, kifupi
tulifanya kitu ambacho kilituingiza
katika historia kubwa ya klabu hii kwa
kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, kuchukua taji la ligi
hapa Tanzania na Ngao ya Jamii.”


ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU

“Tatizo lilianzia wakati tunaanza
kufikiri katika kwenda msimu mpya.
Kuna makosa makubwa tuliyafanya.
Kuna wachezaji mahiri na bora
tuliwaacha. Hapa ndio tulipoanza
kuingiza matatizo. Kuna wachezaji
waliondoka ambao hadi naondoka hapa
sasa sikukubaliana na huu uamuzi wa
kuwaacha. Nafikiri uamuzi huu
ulitokana na baadhi ya watu. Kuna
biashara zao walitaka kuzifanya,
walinishinda nguvu wakafanya uamuzi
wao wanaoujua.
“Sikukubaliana kabisa na kuondoka
kwa wachezaji kama Okwi, Kotei hawa
ni wachezaji waliokuwa na nguvu
kubwa katika mafanikio ya Simba
msimu uliopita. Hata kama kulikuwa
na vitu haviko sawa lakini tulipaswa
kujaribu kuviangalia na kuvifanyia kazi
kama uongozi lakini sio kuwaondoa,
kuwaondoa wachezaji kama Kwasi
(Asante), Haruna (Niyonzima) au hata
Gyan (Nicholas) sikuwa na tatizo lakini
hao wawili nilijua uamuzi huu
ulifanyika wakati ambao tayari
nimeshasaini mkataba mpya. Kama
ingekuwa kabla sijasaini nahisi
ningekuwa na uamuzi tofauti.
“Unajua katika timu hakuna wachezaji
muhimu kama washambuliaji na kila
mmoja alikuwa anajua nguvu ya Okwi
na morali yake ya ushindani. Alikuwa
ni mchezaji ambaye ni mshindani hasa
anapovaa jezi ya Simba. Nilijua
kwamba tutapata shida na tulipoanza
msimu mpya tu washambualiaji wetu
tuliotakiwa kuwategemea wawili
wakaumia Da Silva akaumia na Bocco
akaumia mpaka sasa hawajarudi
tunategemea nguvu ya Kagere peke yake
na hili likawa ndio msingi wa anguko
letu katika Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu huu kwa kutolewa hatua ya
awali.


Vipi kuhusu wachezaji waliosajiliwa?

“Kuhusu wachezaji waliosajiliwa
wakati tunafikiria wachezaji gani wa
kuwaongeza, niliwapa majina ya
wachezaji ambao nawahitaji. bahati
mbaya zaidi mpaka sasa naondoka kuna
mchezaji mmoja tu Kahata ndiye
waliyemleta wengine wote
hawakuletwa.


Vipi kuhusu usajili wa Wabrazili?

“Usajili wa wachezaji wa Brazili
nakumbuka MO alinipigia simu akitaka
tushauriane juu ya hawa wachezaji,
sikutaka kumdanganya nilimwambia
wazi kwamba hiki wanachotaka
kufanya ni kama kurusha shilingi
wakati unataka kuamua kitu. Upande
utakaoangukia hauna namna,
unalazimika kukubaliana nao. Unajua
Wabrazil hawa hawajui utamaduni wa
soka la Afrika. Nilimwambia MO
kwamba hii ni kama kamari ngumu.
Walivyokuja mpaka sasa aliwaonaje
“Kila kitu kipo wazi sio lazima mimi
Patrick niseme tunaweza kujiuliza
wamefanya kazi ambayo tuliitarajia?
Nakubaliana na wengi kwamba
mchezaji wa kigeni anayekuja hapa ni
vyema akawa na ubora mkubwa kuliko
mchezaji wa ndani.”


Vipi usajili wake wa Zana Kulibaly?

Wakati Aussems akiwataja viongozi
wake kuhusika katika usajili mbovu
sasa anajibu swali juu ya usajili wa
beki Zana Kulibaly ambaye naye
aliondoshwa akisema: “Ilikuwa hivi
wakati tunaanza msimu uliopita
niliona tatizo la beki wa kulia. Wakati
huo tulikuwa na Kapombe pekee,
nikawaambia viongozi ikatokea
Kapombe akiumia au kukosekana kwa
namna yoyote tutakuwa na shida
tunatakiwa kutafuta beki mbadala wa
kulia.
“Nikashauri tunatakiwa kusajili
mchezaji mwenye uzoefu mkubwa.
Nilipopeleka majina mawili kwa Magori
Crescentius alikubalia kila kitu tena
alishangilia na kunisifia kwamba
nimepata beki mzuri na kuniuliza
nimepata wapi beki mzuri kama huyu?
Tatizo kubwa la Zana lilikuwa alitumia
muda mrefu kuzoea mazingira ya soka
la Tanzania, baadaye alianza kubadilika
na kuonyesha uwezo mkubwa.
“Shida kubwa ambayo ilikuja kumtokea
baadaye ni kitendo cha kuruhusu
kusikiliza watu wanasema nini juu yake
huwezi kucheza vizuri kila siku,
nimecheza mpira pia, alipaswa hata
kama watu wanamlaumu asisikilize
sana nini watu wanasema badala yake
azidi kuongeza juhudi. Hakufanya hayo,
presha ikawa kubwa kwake.
Aussems:Bila MO simba haina lolote


Ushindani wa ligi aliuonaje?

“Unajua bado kuna maeneo nayaona
kuna changamoto, soka la nchi hii
haliwezi kukuwa kama litaendelea
kuwa ubingwa unakuwa mali ya
Simba, Yanga au Azam zinapocheza
timu hizo tatu ndio ushindani mkubwa
unaonekana lakini zikicheza na timu
zingine matokeo yanakuwa ya
kutabirika sana ndio mana timu hizi
tatu zikiwa bingwa na kutoka
kushindana na mabingwa wengine huko
zinapata matokeo mabaya.
“Angalia ligi katika nchi kama Algeria,
Misri, Morocco Kongo na hata Afrika
Kusini kuna mechi nyingi ngumu katika
ligi unaweza kukuta katika ligi kuna
mechi mpaka 10 ngumu kila mwisho
wa wiki unatarajia kukutana na mechi
ngumu. Lakini hapa ni tofauti. Bado
kuna timu nyingi nyepesi. Changamoto
nyingine kubwa ni viwanja vibovu.
Mpira hauwezi kupiga hatua katika
viwanja vya namna hii. Nafikiri
serikali ya nchi hii inapaswa kuingilia
kati katika hili. Kama hawatabadilisha
hali ya viwanja kwa haraka nafikiri
hata miaka 10 ijayo Tanzania itakuwa
na maendeleo yaleyale katika soka,
hakutakuwa na tofauti kubwa sana.


Simba kuondolewa Caf ni sababu
sahihi kufukuzwa kwake?

“Hatua ya Simba kuondolewa Ligi ya
Mabingwa kila mmoja aliumia.
Inawezekana ilichukuliwa kama vile
wao uongozi ndiyo walioumia peke yao,
lakini hata mimi pia iliniharibia,
nilikuwa na malengo yangu binafsi pia.
“Nimeona uongozi unasema hiyo ni
hatua moja iliyosababisha kunifuta kazi
inawezekana ikawa hivyo, lakini
nafikiri walipaswa kufanya uamuzi huo
wakati uleule tuliotolewa. Kuniacha
kuendelea na kazi na kisha kuniongeza
mkataba huku tukifanya vizuri katika
mechi zetu, kisha uje ufanye uamuzi
huo sasa haiingii akilini kabisa naona
kama ni ujinga. Unaniondoa sasa
wakati timu inaongoza ligi, narudia
kuna sababu zao nyingi na huu ulikuwa
mpango wa muda mrefu.
Kumbe alimwambia MO kuwa Simba
itakuwa na msimu mgumu
“Kuna wakati nilikutana na MO tukiwa
tunazungumza nikamwambia kwamba
msimu huu tutakuwa na msimu mgumu
sana tunapaswa kushikamana sana.
Unajua hili linatokana na mafanikio
ambayo tuliyapata msimu uliopita. Sasa
msimu huu tulitakiwa kuthibitisha
ubora wetu na wakati huo kuna watu
waharibifu wameshafanya uamuzi wa
kuharibu ubora wetu.
“Huu ni mpira kuna lolote linaweza
kutokea, angalia labda niulize nani
alikuwa anajua mabadiliko ya ratiba ya
Caf? Tulipokea taarifa za mabadiliko
hayo tukiwa hatua za awali kabisa za
maandalizi ya msimu, watu
hawaangalii hilo lakini unatakiwa
kujiuliza wakati sisi tukiondoa watu
wetu muhimu wapinzani wetu nao
walifanya makosa kama hayo.
“Simba sio timu kubwa sana kwa
mafanikio Afrika angalau sasa naweza
kuupongeza uongozi kwa kumalizia
uwanja kule Bunju lakini ukiangalia
mpaka sasa Simba haina nyumba
hakuna uwanja wake wa mazoezi
unawezaje kuiita hiyo klabu kubwa
Afrika? Tumekuwa tukitumia viwanja
vya kukodi kwa muda mrefu mara Boko
mara Gymkhana kwahiyo Simba
ilipaswa kukua taratibu na katika
kukua kuna mambo mengi yanatokea.
Anauonaje uwekezaji wa MO?
“Nimekuwa nikifanya kazi Simba lakini
naweza kusema leo Simba imepata mtu
sahihi sana, muda si mrefu Simba
inakwenda kuwa na viwanja vyake vya
mazoezi. Haya ni mafanikio makubwa
kwa Simba lakini hii ni hatua
iliyowezeshwa na MO, alikuwa kila
wakati anaongelea juu ya ndoto zake
anazotaka kuona Simba inakuwa klabu
kubwa. Amekuwa akifanya makubwa
ndani ya timu hii nafikiri bila MO
Simba haina kitu chochote katika
kupata mafanikio huo ndio ukweli
halisi.”


UKARIBU WAKE NA MO DEWJI

“Sidhani kama ni sahihi watu
wakisema kwamba niliwadharau
viongozi wengine na kumuona MO ndio
mtu pekee muhimu. Kuna wakati
lazima tuwe wakweli, wakati nafika
hapa Simba mara nyingi kila kitu
kilikuwa kinamalizwa na MO na yule
aliyekuwa Rais aliyeondoka Salim
(Abdallah ‘Try Again’) lakini pia kuna
dada anaitwa Barbra, mara nyingi
hawa ndio watu nilikuwa nakutana nao
mara kwa mara katika kufanya
majukumu yangu kuwa rahisi.
“Baadaye ndio uongozi ukaja wa bodi,
lakini bado nilikuwa naona kila kitu ili
kifanikiwe lazima kimalizwe na MO
sasa sikuona kama kuna ulazima wa
kuanza kutumia njia ndefu tena ya
kwenda kumuona mtu mwingine wakati
MO yupo. Nafikiri hapo labda ndio kuna
baadhi ya watu wakachukia.
Sasa anaiachaje Simba
“Kwasasa mimi sio kocha wa Simba
tena, lakini klabu hii itabaki kuwa
moyoni mwangu. Hata kama naondoka
akili yangu inaniambia kwamba kwa
kazi ambayo tumeifanya hapa kuanzia
mwanzo wa msimu huu sioni kama
Simba inaweza kukosa ubingwa kirahisi
na ikitokea hivyo wa kulaumiwa
atakuwa kocha mpya atakyekuja badala
yangu.
“Ninachoweza kusema ni kwamba
nawatakia wachezaji, mashabiki na
wanachama kila la kheri katika msimu
huu.
“Nitakuwa naifuatilia Simba katika kila
mchezo watakaokuwa wanacheza
popote nitakapokuwa.”

Anaingaliaje Simba mbele ya Yanga

“ Simba bado ni timu nzuri mbele ya
Yanga. Nafahamu kwamba Yanga
imekuwa na mabadiliko msimu huu
hilo ni kweli lakini bado sidhani kama
wanaweza kuitingisha Simba sana
katika mbio za ubingwa, nimeona
wanapata matokeo lakini sio kwa kiasi
kikubwa kuna maeneo wanapata shida
kidogo, nafahamu kwamba mwisho wa
msimu mbio zitakuwa baina ya timu
hizi. Labda wasiwasi wangu ni jinsi
gani Simba itaendelea baada ya
mabadiliko ya benchi lao la ufundi na
hata wachezaji kuwa katika utulivu.
 
ALISHTUKIA MAPEMA

Alipoulizwa amechukuliaje uamuzi wa
kufutwa kazi, Aussems alisema; “Ni
muda mrefu nilikuwa najua tutafikia
hatua hii kati yangu na Simba. Ni
muda mrefu walikuwa wanataka
kukata shingo yangu, namaanisha
kwamba kuna baadhi ya viongozi kila
mwezi walikuwa na malengo ya kutaka
kuniondoa hapa. Mwezi mpaka mwezi
hakukuwa na zuri ninalolifanya katika
uso wao, daima walikuwa
wakipambana kuhakikisha kazi yangu
hapa inaharibika.

“Unajua mimi sio kocha wa kunipangia
kipi cha kufanya hasa katika ufundi wa
soka, mfano kuniambia mchezaji huyu
anatakiwa kucheza au huyu hatakiwi
kucheza hii ndio ilikuwa akili yao sasa
nilipowakatalia wakatengeneza chuki
kwa muda mrefu, hivyo uamuzi huu
haukunishtua kabisa kwa kuwa
nilikuwa najua kwamba kuna watu
wanapambana kunitoa.”


MAISHA YALIKUWAJE SIMBA?

“Maisha yalikuwa mazuri wakati
tunaanza hapa na kila kitu kilikwenda
sawa. Kidogo maisha yalianza
kubadilika baadaye hasa msimu
uliopita wakati tukipata mafanikio.
Tuwe waungwana, inawezekana Simba
ilikuwa inajulikana hata Ulaya, ila kwa
kazi ya msimu uliopita iliifanya klabu
kujulikana zaidi. Watu walikuwa
wanazijua klabu kubwa za Afrika lakini
Simba haikuwa na jina kubwa.”
“Tulianza kwa kuhakikisha kwanza
tunakuwa na falsafa ya mpira wetu
hapa kwa kutafuta wachezaji
watakaoendana na falsafa hiyo.
Tulifanya kazi kubwa sana msimu
uliopita. Wachezaji walikuwa na ubora
wa juu kwa mchezaji mmoja mmoja
hadi timu nzima. Angalia mchezaji
kama Erasto (Nyoni), Kagere (Medie),
Okwi (Emmanuel), Chama (Clatous)
walifanya kazi kubwa sana, kifupi
tulifanya kitu ambacho kilituingiza
katika historia kubwa ya klabu hii kwa
kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, kuchukua taji la ligi
hapa Tanzania na Ngao ya Jamii.”


ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU

“Tatizo lilianzia wakati tunaanza
kufikiri katika kwenda msimu mpya.
Kuna makosa makubwa tuliyafanya.
Kuna wachezaji mahiri na bora
tuliwaacha. Hapa ndio tulipoanza
kuingiza matatizo. Kuna wachezaji
waliondoka ambao hadi naondoka hapa
sasa sikukubaliana na huu uamuzi wa
kuwaacha. Nafikiri uamuzi huu
ulitokana na baadhi ya watu. Kuna
biashara zao walitaka kuzifanya,
walinishinda nguvu wakafanya uamuzi
wao wanaoujua.
“Sikukubaliana kabisa na kuondoka
kwa wachezaji kama Okwi, Kotei hawa
ni wachezaji waliokuwa na nguvu
kubwa katika mafanikio ya Simba
msimu uliopita. Hata kama kulikuwa
na vitu haviko sawa lakini tulipaswa
kujaribu kuviangalia na kuvifanyia kazi
kama uongozi lakini sio kuwaondoa,
kuwaondoa wachezaji kama Kwasi
(Asante), Haruna (Niyonzima) au hata
Gyan (Nicholas) sikuwa na tatizo lakini
hao wawili nilijua uamuzi huu
ulifanyika wakati ambao tayari
nimeshasaini mkataba mpya. Kama
ingekuwa kabla sijasaini nahisi
ningekuwa na uamuzi tofauti.
“Unajua katika timu hakuna wachezaji
muhimu kama washambuliaji na kila
mmoja alikuwa anajua nguvu ya Okwi
na morali yake ya ushindani. Alikuwa
ni mchezaji ambaye ni mshindani hasa
anapovaa jezi ya Simba. Nilijua
kwamba tutapata shida na tulipoanza
msimu mpya tu washambualiaji wetu
tuliotakiwa kuwategemea wawili
wakaumia Da Silva akaumia na Bocco
akaumia mpaka sasa hawajarudi
tunategemea nguvu ya Kagere peke yake
na hili likawa ndio msingi wa anguko
letu katika Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu huu kwa kutolewa hatua ya
awali.


Vipi kuhusu wachezaji waliosajiliwa?

“Kuhusu wachezaji waliosajiliwa
wakati tunafikiria wachezaji gani wa
kuwaongeza, niliwapa majina ya
wachezaji ambao nawahitaji. bahati
mbaya zaidi mpaka sasa naondoka kuna
mchezaji mmoja tu Kahata ndiye
waliyemleta wengine wote
hawakuletwa.


Vipi kuhusu usajili wa Wabrazili?

“Usajili wa wachezaji wa Brazili
nakumbuka MO alinipigia simu akitaka
tushauriane juu ya hawa wachezaji,
sikutaka kumdanganya nilimwambia
wazi kwamba hiki wanachotaka
kufanya ni kama kurusha shilingi
wakati unataka kuamua kitu. Upande
utakaoangukia hauna namna,
unalazimika kukubaliana nao. Unajua
Wabrazil hawa hawajui utamaduni wa
soka la Afrika. Nilimwambia MO
kwamba hii ni kama kamari ngumu.
Walivyokuja mpaka sasa aliwaonaje
“Kila kitu kipo wazi sio lazima mimi
Patrick niseme tunaweza kujiuliza
wamefanya kazi ambayo tuliitarajia?
Nakubaliana na wengi kwamba
mchezaji wa kigeni anayekuja hapa ni
vyema akawa na ubora mkubwa kuliko
mchezaji wa ndani.”


Vipi usajili wake wa Zana Kulibaly?

Wakati Aussems akiwataja viongozi
wake kuhusika katika usajili mbovu
sasa anajibu swali juu ya usajili wa
beki Zana Kulibaly ambaye naye
aliondoshwa akisema: “Ilikuwa hivi
wakati tunaanza msimu uliopita
niliona tatizo la beki wa kulia. Wakati
huo tulikuwa na Kapombe pekee,
nikawaambia viongozi ikatokea
Kapombe akiumia au kukosekana kwa
namna yoyote tutakuwa na shida
tunatakiwa kutafuta beki mbadala wa
kulia.
“Nikashauri tunatakiwa kusajili
mchezaji mwenye uzoefu mkubwa.
Nilipopeleka majina mawili kwa Magori
Crescentius alikubalia kila kitu tena
alishangilia na kunisifia kwamba
nimepata beki mzuri na kuniuliza
nimepata wapi beki mzuri kama huyu?
Tatizo kubwa la Zana lilikuwa alitumia
muda mrefu kuzoea mazingira ya soka
la Tanzania, baadaye alianza kubadilika
na kuonyesha uwezo mkubwa.
“Shida kubwa ambayo ilikuja kumtokea
baadaye ni kitendo cha kuruhusu
kusikiliza watu wanasema nini juu yake
huwezi kucheza vizuri kila siku,
nimecheza mpira pia, alipaswa hata
kama watu wanamlaumu asisikilize
sana nini watu wanasema badala yake
azidi kuongeza juhudi. Hakufanya hayo,
presha ikawa kubwa kwake.
Aussems:Bila MO simba haina lolote


Ushindani wa ligi aliuonaje?

“Unajua bado kuna maeneo nayaona
kuna changamoto, soka la nchi hii
haliwezi kukuwa kama litaendelea
kuwa ubingwa unakuwa mali ya
Simba, Yanga au Azam zinapocheza
timu hizo tatu ndio ushindani mkubwa
unaonekana lakini zikicheza na timu
zingine matokeo yanakuwa ya
kutabirika sana ndio mana timu hizi
tatu zikiwa bingwa na kutoka
kushindana na mabingwa wengine huko
zinapata matokeo mabaya.
“Angalia ligi katika nchi kama Algeria,
Misri, Morocco Kongo na hata Afrika
Kusini kuna mechi nyingi ngumu katika
ligi unaweza kukuta katika ligi kuna
mechi mpaka 10 ngumu kila mwisho
wa wiki unatarajia kukutana na mechi
ngumu. Lakini hapa ni tofauti. Bado
kuna timu nyingi nyepesi. Changamoto
nyingine kubwa ni viwanja vibovu.
Mpira hauwezi kupiga hatua katika
viwanja vya namna hii. Nafikiri
serikali ya nchi hii inapaswa kuingilia
kati katika hili. Kama hawatabadilisha
hali ya viwanja kwa haraka nafikiri
hata miaka 10 ijayo Tanzania itakuwa
na maendeleo yaleyale katika soka,
hakutakuwa na tofauti kubwa sana.


Simba kuondolewa Caf ni sababu
sahihi kufukuzwa kwake?

“Hatua ya Simba kuondolewa Ligi ya
Mabingwa kila mmoja aliumia.
Inawezekana ilichukuliwa kama vile
wao uongozi ndiyo walioumia peke yao,
lakini hata mimi pia iliniharibia,
nilikuwa na malengo yangu binafsi pia.
“Nimeona uongozi unasema hiyo ni
hatua moja iliyosababisha kunifuta kazi
inawezekana ikawa hivyo, lakini
nafikiri walipaswa kufanya uamuzi huo
wakati uleule tuliotolewa. Kuniacha
kuendelea na kazi na kisha kuniongeza
mkataba huku tukifanya vizuri katika
mechi zetu, kisha uje ufanye uamuzi
huo sasa haiingii akilini kabisa naona
kama ni ujinga. Unaniondoa sasa
wakati timu inaongoza ligi, narudia
kuna sababu zao nyingi na huu ulikuwa
mpango wa muda mrefu.
Kumbe alimwambia MO kuwa Simba
itakuwa na msimu mgumu
“Kuna wakati nilikutana na MO tukiwa
tunazungumza nikamwambia kwamba
msimu huu tutakuwa na msimu mgumu
sana tunapaswa kushikamana sana.
Unajua hili linatokana na mafanikio
ambayo tuliyapata msimu uliopita. Sasa
msimu huu tulitakiwa kuthibitisha
ubora wetu na wakati huo kuna watu
waharibifu wameshafanya uamuzi wa
kuharibu ubora wetu.
“Huu ni mpira kuna lolote linaweza
kutokea, angalia labda niulize nani
alikuwa anajua mabadiliko ya ratiba ya
Caf? Tulipokea taarifa za mabadiliko
hayo tukiwa hatua za awali kabisa za
maandalizi ya msimu, watu
hawaangalii hilo lakini unatakiwa
kujiuliza wakati sisi tukiondoa watu
wetu muhimu wapinzani wetu nao
walifanya makosa kama hayo.
“Simba sio timu kubwa sana kwa
mafanikio Afrika angalau sasa naweza
kuupongeza uongozi kwa kumalizia
uwanja kule Bunju lakini ukiangalia
mpaka sasa Simba haina nyumba
hakuna uwanja wake wa mazoezi
unawezaje kuiita hiyo klabu kubwa
Afrika? Tumekuwa tukitumia viwanja
vya kukodi kwa muda mrefu mara Boko
mara Gymkhana kwahiyo Simba
ilipaswa kukua taratibu na katika
kukua kuna mambo mengi yanatokea.
Anauonaje uwekezaji wa MO?
“Nimekuwa nikifanya kazi Simba lakini
naweza kusema leo Simba imepata mtu
sahihi sana, muda si mrefu Simba
inakwenda kuwa na viwanja vyake vya
mazoezi. Haya ni mafanikio makubwa
kwa Simba lakini hii ni hatua
iliyowezeshwa na MO, alikuwa kila
wakati anaongelea juu ya ndoto zake
anazotaka kuona Simba inakuwa klabu
kubwa. Amekuwa akifanya makubwa
ndani ya timu hii nafikiri bila MO
Simba haina kitu chochote katika
kupata mafanikio huo ndio ukweli
halisi.”


UKARIBU WAKE NA MO DEWJI

“Sidhani kama ni sahihi watu
wakisema kwamba niliwadharau
viongozi wengine na kumuona MO ndio
mtu pekee muhimu. Kuna wakati
lazima tuwe wakweli, wakati nafika
hapa Simba mara nyingi kila kitu
kilikuwa kinamalizwa na MO na yule
aliyekuwa Rais aliyeondoka Salim
(Abdallah ‘Try Again’) lakini pia kuna
dada anaitwa Barbra, mara nyingi
hawa ndio watu nilikuwa nakutana nao
mara kwa mara katika kufanya
majukumu yangu kuwa rahisi.
“Baadaye ndio uongozi ukaja wa bodi,
lakini bado nilikuwa naona kila kitu ili
kifanikiwe lazima kimalizwe na MO
sasa sikuona kama kuna ulazima wa
kuanza kutumia njia ndefu tena ya
kwenda kumuona mtu mwingine wakati
MO yupo. Nafikiri hapo labda ndio kuna
baadhi ya watu wakachukia.
Sasa anaiachaje Simba
“Kwasasa mimi sio kocha wa Simba
tena, lakini klabu hii itabaki kuwa
moyoni mwangu. Hata kama naondoka
akili yangu inaniambia kwamba kwa
kazi ambayo tumeifanya hapa kuanzia
mwanzo wa msimu huu sioni kama
Simba inaweza kukosa ubingwa kirahisi
na ikitokea hivyo wa kulaumiwa
atakuwa kocha mpya atakyekuja badala
yangu.
“Ninachoweza kusema ni kwamba
nawatakia wachezaji, mashabiki na
wanachama kila la kheri katika msimu
huu.
“Nitakuwa naifuatilia Simba katika kila
mchezo watakaokuwa wanacheza
popote nitakapokuwa.”

Anaingaliaje Simba mbele ya Yanga

“ Simba bado ni timu nzuri mbele ya
Yanga. Nafahamu kwamba Yanga
imekuwa na mabadiliko msimu huu
hilo ni kweli lakini bado sidhani kama
wanaweza kuitingisha Simba sana
katika mbio za ubingwa, nimeona
wanapata matokeo lakini sio kwa kiasi
kikubwa kuna maeneo wanapata shida
kidogo, nafahamu kwamba mwisho wa
msimu mbio zitakuwa baina ya timu
hizi. Labda wasiwasi wangu ni jinsi
gani Simba itaendelea baada ya
mabadiliko ya benchi lao la ufundi na
hata wachezaji kuwa katika utulivu.
Huyu ndo fundi wa soka
He is very technical
God bless you
 
Huyu ndo fundi wa soka
He is very technical
God bless you
Angekuwa technical angejua ni kikosi gani kilitakiwa kucheza na Mwadui, au angejua kwanini Prison haijapoteza mchezo hata mmoja na hivyo mie nicheze vipi.
Matokeo yake akazidiwa kabisa kimbinu na Adolf Rishad. Hamna kocha pale tusidanganyane
 
Angekuwa technical angejua ni kikosi gani kilitakiwa kucheza na Mwadui, au angejua kwanini Prison haijapoteza mchezo hata mmoja na hivyo mie nicheze vipi.
Matokeo yake akazidiwa kabisa kimbinu na Adolf Rishad. Hamna kocha pale tusidanganyane
Wale waliokuwa wanabisha kuhusu ishu ya kupangiana kikosi mkisoma hapa mtakubaliana na Aussems.
 
Wale waliokuwa wanabisha kuhusu ishu ya kupangiana kikosi mkisoma hapa mtakubaliana na Aussems.
Aussems hajui kupanga kikosi, hata mashabiki uwanjani tulikuwa tunajua kuwa anachemsha, subs ndio kabisa ni mwendo wa kubahatisha tu.

Mechi na Ud Songo, Manula hakuwa fit, Kakolanya ndie aliyedaka ugenini na alifanya excellent saves, mechi ya Dar akampanga unfit Manula tukachemka.
 
Aussems hajui kupanga kikosi, hata mashabiki uwanjani tulikuwa tunajua kuwa anachemsha, subs ndio kabisa ni mwendo wa kubahatisha tu.

Mechi na Ud Songo, Manula hakuwa fit, Kakolanya ndie aliyedaka ugenini na alifanya excellent saves, mechi ya Dar akampanga unfit Manula tukachemka.

Teh!! Mkuu kocha si anakuwa nao mazoezini hao wachezaji na yeye ndo anajua hali zao vizuri. Wewe ni daktari wa timu? Kama ndio basi Aussems alichemka.
 
ALISHTUKIA MAPEMA

Alipoulizwa amechukuliaje uamuzi wa
kufutwa kazi, Aussems alisema; “Ni
muda mrefu nilikuwa najua tutafikia
hatua hii kati yangu na Simba. Ni
muda mrefu walikuwa wanataka
kukata shingo yangu, namaanisha
kwamba kuna baadhi ya viongozi kila
mwezi walikuwa na malengo ya kutaka
kuniondoa hapa. Mwezi mpaka mwezi
hakukuwa na zuri ninalolifanya katika
uso wao, daima walikuwa
wakipambana kuhakikisha kazi yangu
hapa inaharibika.

“Unajua mimi sio kocha wa kunipangia
kipi cha kufanya hasa katika ufundi wa
soka, mfano kuniambia mchezaji huyu
anatakiwa kucheza au huyu hatakiwi
kucheza hii ndio ilikuwa akili yao sasa
nilipowakatalia wakatengeneza chuki
kwa muda mrefu, hivyo uamuzi huu
haukunishtua kabisa kwa kuwa
nilikuwa najua kwamba kuna watu
wanapambana kunitoa.”


MAISHA YALIKUWAJE SIMBA?

“Maisha yalikuwa mazuri wakati
tunaanza hapa na kila kitu kilikwenda
sawa. Kidogo maisha yalianza
kubadilika baadaye hasa msimu
uliopita wakati tukipata mafanikio.
Tuwe waungwana, inawezekana Simba
ilikuwa inajulikana hata Ulaya, ila kwa
kazi ya msimu uliopita iliifanya klabu
kujulikana zaidi. Watu walikuwa
wanazijua klabu kubwa za Afrika lakini
Simba haikuwa na jina kubwa.”
“Tulianza kwa kuhakikisha kwanza
tunakuwa na falsafa ya mpira wetu
hapa kwa kutafuta wachezaji
watakaoendana na falsafa hiyo.
Tulifanya kazi kubwa sana msimu
uliopita. Wachezaji walikuwa na ubora
wa juu kwa mchezaji mmoja mmoja
hadi timu nzima. Angalia mchezaji
kama Erasto (Nyoni), Kagere (Medie),
Okwi (Emmanuel), Chama (Clatous)
walifanya kazi kubwa sana, kifupi
tulifanya kitu ambacho kilituingiza
katika historia kubwa ya klabu hii kwa
kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, kuchukua taji la ligi
hapa Tanzania na Ngao ya Jamii.”


ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU

“Tatizo lilianzia wakati tunaanza
kufikiri katika kwenda msimu mpya.
Kuna makosa makubwa tuliyafanya.
Kuna wachezaji mahiri na bora
tuliwaacha. Hapa ndio tulipoanza
kuingiza matatizo. Kuna wachezaji
waliondoka ambao hadi naondoka hapa
sasa sikukubaliana na huu uamuzi wa
kuwaacha. Nafikiri uamuzi huu
ulitokana na baadhi ya watu. Kuna
biashara zao walitaka kuzifanya,
walinishinda nguvu wakafanya uamuzi
wao wanaoujua.
“Sikukubaliana kabisa na kuondoka
kwa wachezaji kama Okwi, Kotei hawa
ni wachezaji waliokuwa na nguvu
kubwa katika mafanikio ya Simba
msimu uliopita. Hata kama kulikuwa
na vitu haviko sawa lakini tulipaswa
kujaribu kuviangalia na kuvifanyia kazi
kama uongozi lakini sio kuwaondoa,
kuwaondoa wachezaji kama Kwasi
(Asante), Haruna (Niyonzima) au hata
Gyan (Nicholas) sikuwa na tatizo lakini
hao wawili nilijua uamuzi huu
ulifanyika wakati ambao tayari
nimeshasaini mkataba mpya. Kama
ingekuwa kabla sijasaini nahisi
ningekuwa na uamuzi tofauti.
“Unajua katika timu hakuna wachezaji
muhimu kama washambuliaji na kila
mmoja alikuwa anajua nguvu ya Okwi
na morali yake ya ushindani. Alikuwa
ni mchezaji ambaye ni mshindani hasa
anapovaa jezi ya Simba. Nilijua
kwamba tutapata shida na tulipoanza
msimu mpya tu washambualiaji wetu
tuliotakiwa kuwategemea wawili
wakaumia Da Silva akaumia na Bocco
akaumia mpaka sasa hawajarudi
tunategemea nguvu ya Kagere peke yake
na hili likawa ndio msingi wa anguko
letu katika Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu huu kwa kutolewa hatua ya
awali.


Vipi kuhusu wachezaji waliosajiliwa?

“Kuhusu wachezaji waliosajiliwa
wakati tunafikiria wachezaji gani wa
kuwaongeza, niliwapa majina ya
wachezaji ambao nawahitaji. bahati
mbaya zaidi mpaka sasa naondoka kuna
mchezaji mmoja tu Kahata ndiye
waliyemleta wengine wote
hawakuletwa.


Vipi kuhusu usajili wa Wabrazili?

“Usajili wa wachezaji wa Brazili
nakumbuka MO alinipigia simu akitaka
tushauriane juu ya hawa wachezaji,
sikutaka kumdanganya nilimwambia
wazi kwamba hiki wanachotaka
kufanya ni kama kurusha shilingi
wakati unataka kuamua kitu. Upande
utakaoangukia hauna namna,
unalazimika kukubaliana nao. Unajua
Wabrazil hawa hawajui utamaduni wa
soka la Afrika. Nilimwambia MO
kwamba hii ni kama kamari ngumu.
Walivyokuja mpaka sasa aliwaonaje
“Kila kitu kipo wazi sio lazima mimi
Patrick niseme tunaweza kujiuliza
wamefanya kazi ambayo tuliitarajia?
Nakubaliana na wengi kwamba
mchezaji wa kigeni anayekuja hapa ni
vyema akawa na ubora mkubwa kuliko
mchezaji wa ndani.”


Vipi usajili wake wa Zana Kulibaly?

Wakati Aussems akiwataja viongozi
wake kuhusika katika usajili mbovu
sasa anajibu swali juu ya usajili wa
beki Zana Kulibaly ambaye naye
aliondoshwa akisema: “Ilikuwa hivi
wakati tunaanza msimu uliopita
niliona tatizo la beki wa kulia. Wakati
huo tulikuwa na Kapombe pekee,
nikawaambia viongozi ikatokea
Kapombe akiumia au kukosekana kwa
namna yoyote tutakuwa na shida
tunatakiwa kutafuta beki mbadala wa
kulia.
“Nikashauri tunatakiwa kusajili
mchezaji mwenye uzoefu mkubwa.
Nilipopeleka majina mawili kwa Magori
Crescentius alikubalia kila kitu tena
alishangilia na kunisifia kwamba
nimepata beki mzuri na kuniuliza
nimepata wapi beki mzuri kama huyu?
Tatizo kubwa la Zana lilikuwa alitumia
muda mrefu kuzoea mazingira ya soka
la Tanzania, baadaye alianza kubadilika
na kuonyesha uwezo mkubwa.
“Shida kubwa ambayo ilikuja kumtokea
baadaye ni kitendo cha kuruhusu
kusikiliza watu wanasema nini juu yake
huwezi kucheza vizuri kila siku,
nimecheza mpira pia, alipaswa hata
kama watu wanamlaumu asisikilize
sana nini watu wanasema badala yake
azidi kuongeza juhudi. Hakufanya hayo,
presha ikawa kubwa kwake.
Aussems:Bila MO simba haina lolote


Ushindani wa ligi aliuonaje?

“Unajua bado kuna maeneo nayaona
kuna changamoto, soka la nchi hii
haliwezi kukuwa kama litaendelea
kuwa ubingwa unakuwa mali ya
Simba, Yanga au Azam zinapocheza
timu hizo tatu ndio ushindani mkubwa
unaonekana lakini zikicheza na timu
zingine matokeo yanakuwa ya
kutabirika sana ndio mana timu hizi
tatu zikiwa bingwa na kutoka
kushindana na mabingwa wengine huko
zinapata matokeo mabaya.
“Angalia ligi katika nchi kama Algeria,
Misri, Morocco Kongo na hata Afrika
Kusini kuna mechi nyingi ngumu katika
ligi unaweza kukuta katika ligi kuna
mechi mpaka 10 ngumu kila mwisho
wa wiki unatarajia kukutana na mechi
ngumu. Lakini hapa ni tofauti. Bado
kuna timu nyingi nyepesi. Changamoto
nyingine kubwa ni viwanja vibovu.
Mpira hauwezi kupiga hatua katika
viwanja vya namna hii. Nafikiri
serikali ya nchi hii inapaswa kuingilia
kati katika hili. Kama hawatabadilisha
hali ya viwanja kwa haraka nafikiri
hata miaka 10 ijayo Tanzania itakuwa
na maendeleo yaleyale katika soka,
hakutakuwa na tofauti kubwa sana.


Simba kuondolewa Caf ni sababu
sahihi kufukuzwa kwake?

“Hatua ya Simba kuondolewa Ligi ya
Mabingwa kila mmoja aliumia.
Inawezekana ilichukuliwa kama vile
wao uongozi ndiyo walioumia peke yao,
lakini hata mimi pia iliniharibia,
nilikuwa na malengo yangu binafsi pia.
“Nimeona uongozi unasema hiyo ni
hatua moja iliyosababisha kunifuta kazi
inawezekana ikawa hivyo, lakini
nafikiri walipaswa kufanya uamuzi huo
wakati uleule tuliotolewa. Kuniacha
kuendelea na kazi na kisha kuniongeza
mkataba huku tukifanya vizuri katika
mechi zetu, kisha uje ufanye uamuzi
huo sasa haiingii akilini kabisa naona
kama ni ujinga. Unaniondoa sasa
wakati timu inaongoza ligi, narudia
kuna sababu zao nyingi na huu ulikuwa
mpango wa muda mrefu.
Kumbe alimwambia MO kuwa Simba
itakuwa na msimu mgumu
“Kuna wakati nilikutana na MO tukiwa
tunazungumza nikamwambia kwamba
msimu huu tutakuwa na msimu mgumu
sana tunapaswa kushikamana sana.
Unajua hili linatokana na mafanikio
ambayo tuliyapata msimu uliopita. Sasa
msimu huu tulitakiwa kuthibitisha
ubora wetu na wakati huo kuna watu
waharibifu wameshafanya uamuzi wa
kuharibu ubora wetu.
“Huu ni mpira kuna lolote linaweza
kutokea, angalia labda niulize nani
alikuwa anajua mabadiliko ya ratiba ya
Caf? Tulipokea taarifa za mabadiliko
hayo tukiwa hatua za awali kabisa za
maandalizi ya msimu, watu
hawaangalii hilo lakini unatakiwa
kujiuliza wakati sisi tukiondoa watu
wetu muhimu wapinzani wetu nao
walifanya makosa kama hayo.
“Simba sio timu kubwa sana kwa
mafanikio Afrika angalau sasa naweza
kuupongeza uongozi kwa kumalizia
uwanja kule Bunju lakini ukiangalia
mpaka sasa Simba haina nyumba
hakuna uwanja wake wa mazoezi
unawezaje kuiita hiyo klabu kubwa
Afrika? Tumekuwa tukitumia viwanja
vya kukodi kwa muda mrefu mara Boko
mara Gymkhana kwahiyo Simba
ilipaswa kukua taratibu na katika
kukua kuna mambo mengi yanatokea.
Anauonaje uwekezaji wa MO?
“Nimekuwa nikifanya kazi Simba lakini
naweza kusema leo Simba imepata mtu
sahihi sana, muda si mrefu Simba
inakwenda kuwa na viwanja vyake vya
mazoezi. Haya ni mafanikio makubwa
kwa Simba lakini hii ni hatua
iliyowezeshwa na MO, alikuwa kila
wakati anaongelea juu ya ndoto zake
anazotaka kuona Simba inakuwa klabu
kubwa. Amekuwa akifanya makubwa
ndani ya timu hii nafikiri bila MO
Simba haina kitu chochote katika
kupata mafanikio huo ndio ukweli
halisi.”


UKARIBU WAKE NA MO DEWJI

“Sidhani kama ni sahihi watu
wakisema kwamba niliwadharau
viongozi wengine na kumuona MO ndio
mtu pekee muhimu. Kuna wakati
lazima tuwe wakweli, wakati nafika
hapa Simba mara nyingi kila kitu
kilikuwa kinamalizwa na MO na yule
aliyekuwa Rais aliyeondoka Salim
(Abdallah ‘Try Again’) lakini pia kuna
dada anaitwa Barbra, mara nyingi
hawa ndio watu nilikuwa nakutana nao
mara kwa mara katika kufanya
majukumu yangu kuwa rahisi.
“Baadaye ndio uongozi ukaja wa bodi,
lakini bado nilikuwa naona kila kitu ili
kifanikiwe lazima kimalizwe na MO
sasa sikuona kama kuna ulazima wa
kuanza kutumia njia ndefu tena ya
kwenda kumuona mtu mwingine wakati
MO yupo. Nafikiri hapo labda ndio kuna
baadhi ya watu wakachukia.
Sasa anaiachaje Simba
“Kwasasa mimi sio kocha wa Simba
tena, lakini klabu hii itabaki kuwa
moyoni mwangu. Hata kama naondoka
akili yangu inaniambia kwamba kwa
kazi ambayo tumeifanya hapa kuanzia
mwanzo wa msimu huu sioni kama
Simba inaweza kukosa ubingwa kirahisi
na ikitokea hivyo wa kulaumiwa
atakuwa kocha mpya atakyekuja badala
yangu.
“Ninachoweza kusema ni kwamba
nawatakia wachezaji, mashabiki na
wanachama kila la kheri katika msimu
huu.
“Nitakuwa naifuatilia Simba katika kila
mchezo watakaokuwa wanacheza
popote nitakapokuwa.”

Anaingaliaje Simba mbele ya Yanga

“ Simba bado ni timu nzuri mbele ya
Yanga. Nafahamu kwamba Yanga
imekuwa na mabadiliko msimu huu
hilo ni kweli lakini bado sidhani kama
wanaweza kuitingisha Simba sana
katika mbio za ubingwa, nimeona
wanapata matokeo lakini sio kwa kiasi
kikubwa kuna maeneo wanapata shida
kidogo, nafahamu kwamba mwisho wa
msimu mbio zitakuwa baina ya timu
hizi. Labda wasiwasi wangu ni jinsi
gani Simba itaendelea baada ya
mabadiliko ya benchi lao la ufundi na
hata wachezaji kuwa katika utulivu.
Bila Mo Simba haina kitu. Statement kubwa sana hii.
Kwa wenye akili lakini. Kwa oyaoya, haina maana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom