Kutoka Mövenpick: Mdahalo wa Katiba - Lissu vs Mnyaa

CUF wamekasirika kuambiwa kuwa wana ndoa na ccm! Ukumbi umechafuka ni vurugu tupu!
 
Kuna vurugu kidogo. Mtatiro anasukumwa wakati anatuliza wanaCUF baada ya dongo la TL.
 
Ni makelele tu, Mnyaa anaongea watu hawasikilizi. Mtatiro anaongea, anawataka wanaCUF watulie kama hata kama TL atawaudhi.
 
mh hawa wanachama waopiga kelele si wa CUF watakuwa wa CCM wamekuja vuruga mdahalo
 
Mnyaa: Bado msimamo wetu ni serkali 3, tumekuwa na msimamo huo tangu chadema hawajawa na msimamo huo.
 
TL: Mabadiliko ya katiba znz yameua upinzani znz. Huku bara CCM na CUF wanashirikiana ktk uchaguzi. CUF hawawezi kupinga la CCM.

Makinda, Kombani, Werema wote wanakwepa kuzumngumzia mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar na athari zake kwenye sura ya muungano. Kuna nini nyuma ya Pazia?
 
Mwnykt(R.Mwakitwange): kama wananchi wana wasiwasi kwamba mswada haubebi maoni yao, itakuwaje wakati wa kutoa maoni ya kukubali au kukataa katiba?

Mnyaa: wananchi wana haki ya kukubali au kukataa, hawalazimishwi. Tusiichezee nafasi hii, tuitumie ipasavyo.
 
Back
Top Bottom