Kutoka Maktaba ya Mchungaji

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,533
Invisible,

Naomba sana ulinde tunayoandika humu. Hiyo miaka ya baadaye, iwe 20 au 50 kutoka leo, tuliyoyasema yawe ya msingi, mzaha au kebehi, yabakie kama zilipendwa na tujikumbushe tuliyoyasema zamani.

Ninayoyaleta hapa ni kutoka Maktaba uchwara yangu ambayo nilaanzisha muda mfupi na mengi ya kiuanaharakati niliyoandika yalikuja kupotea kutokana na NYENZI.COM kufa..

Nayaambatanisha hapa kama kumbukumbu za ushiriki katika harakati na hata kuangalia kilichosewa zama zile kina tofauti gani na yanayofanyika sasa.

Someni kwa Furaha!
 
September 2000
Kishoka
Member
posted 09-02-2000 00:17 http://www.nyenzi.com/cgi/ubb/ubbmisc.cgi?action=getbio&UserName=Kishoka
Winnie
Naona pambano jipya linaanza Dues v/s Milo.
Tukirudi kwenye hoja kuu, wakulaumiwa kuhusu kuoza kwa siasa na Wanasiasa wa Tanzania ni wananchi wenyewe. Ni sisi wenyewe tunaoharibu mambo siku ya kupiga kura. Kura ni siri yako mwenyewe na kama nadhiri yako inakutuma vizuri, basi utafanya uchaguzi ulio safi.
Nimependelea sana kitu ambacho Bw. Keyes alikisema wakati wa mdahalo wa Republican Party Des Moines Iowa. Keyes alisema ni wajibu wako wewe mpiga kura kuchagua kiongozi aliye bora na atakayelitumikia taifa kwa faida ya taifa.
Watanzania inabidi tubadili mtazamo wetu kuhusu wanasiasa wetu na siasa za njii yetu.
Utendaji na mipango mibovu, rushwa, umasikini, ubadhirifu na magonjwa mengine mengio yanayoikabili taifa letu, ni mambo tuliyojitakia na tunaendelea nayo. matatizo ya nci yetu si ya CCM pekee, ni ya watu wote.

Tumejenga silika ya "KU-RECYCLE" wanasiasa na viongozi wetu. tumefikia hatua ya kuwapa Utemi, Umwinyi na hata Ubunge wa maisha. One will ask how do we recycle them? every time we have elections from the time of CCM todate, we keep voting for the same faces everyday. Je hakuna sura nyingine na mpya?
Sura nyingine ninazozungumzia siyo hizi za kina Mrema, Bagenda, Marando au Wassira ambazo vinahama kutoka chama kimoja hadi kingine. Mrema and Company is like old wine in new bottle.
Kwa kuwa Watanzania tume ruhusu siasa kuwa mradi wa binafsi kwa kutokutumia haki zetu ipaswavyo, itakuwa ni kazi bure kulalamika hata kama ni kutaka kufanya mabadiliko ya katiba.
Wanasiasa/siasa, wananufaika sana na imani zetu tulizowajengea na wamegeuza siasa kuwa miradi binafsi kamamradi wa kuku au mchicha. Politics is a new way of entreprenualship in Tanzania where Politicians Amass the nations wealth for their vitambis and their petty kingdoms. Badala ya wao kulitumikia taifa, taifa linawatumika wao, iwe CCM, CUF, CHADEMA au NCCR.
Kennedy aliuliza nitalifanyia nini taifa langu ? wanasiasa wetu wanahoji Waytafanyiwa nini na taifa lao?
Ili kuondokana na uozo huu wa kisiasa, itabidi October hii watanzania tuwe wakweli kama tunataka mabadiliko na mapinduzi.
Nafahamu kutakuwa na kampeni, hongo na kadhalika, lakini siku ya uchaguzi ni siku pekee ambayo tutaleta MAGEUZI ya kwa kuaacha kuwapigia kura wale "tuliowazoea" wala rushwa, wabadhirifu, wabinafsi, wabovu na miungu watu na kujichagulia watu safi watakaoingia katika Bunge letu na Ikulu.
Tukipiga kura kwa makini,(hata wakati wa kupitisha wagombea katika vyama vyetu) tutachagua viongozi bora wataoliingiza taifa katika millenia mpya kwa vishindo.
Watanzania Tuache KU-RECYCLE wanasiasa na watendaji wa serikali zetu kama tunataka MAGEUZI ya KWELI.
Zidumu fikra za......
[This message has been edited by Kishoka (edited 10-02-2000).]
 
Inaendelea..

Kishoka
Member
posted 09-02-2000 20:48 http://www.nyenzi.com/cgi/ubb/ubbmisc.cgi?action=getbio&UserName=Kishoka
Winnie
Lawama nyingi tumemtupia Mwalimu(RIP), lakini mbona aliondoka kitambo madarakani? Huu ni mwaka wa 15 tangu aache urais na wa 13 baada ya kuachia uenyekiti. Je ni lipi ambalo Serikali ya pili na ya tatu imezifanya?
Ukipima kwa utendaji kazi Tanzania, utagundua kuwa ufanisi wetu ni wa hali ya chini. Uzalishaji mali umezorota kwa kiwango kikubwa, kuanzia vijijini(Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uhunzi) hata mijini. Our scapegoat has always been Mwalimu because of Arusha Declaration.
Je ni yeye pekee aliyeharibu Uchumi wetu kwa mipango mibovu? je Azimio la Zanzibar kufuta siasa ya ujamaa na kujitegemea limesaidia nini katika kujenga nchi yetu? je Upinzani umefanya nini katika kumwamsha Mtanzania kuondokana na umasikini? je wasomi wetu(DONS) wa pale mlimani na kwenye taasisi, mashirika na serikali(vijiji,mitaa, wilaya, mikoa, wizara)kuu wamefanya nini cha kumuelimisha mtanzania ?
Mimi nilitarajia kwa kuwa Mwalimu kaondoka madarakani, basi makundi hayo yote niliyoyataja hapo juu(ambayo kwa uhakika yalipingana naye kifikara)yangeleta msukumo na mabadiliko katika mfumo wetu wa uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Yangeleta mapinduzi mapya kwa wananchi ku-prove kuwa Mwalimu alitupeleka pabaya. Yangeondoa ujinga, umasikini na maradhi na kujenga siasa bora.
Lakini hakuna jipya lililotokea kumkwamua Mtanzania kwenye umasikini. badala yake tumeendelea kumlaumu Mwalimu mpaka ametutoka.
Makundi haya badala ya kutumia amani, mshikamano na umoja aliotujengea Mwalimu kuinua uchumi na pato la Taifa, yemegeuza mambo hayo kwa kulinda na kujenga nafsi zao. Ubinafsi, Rushwa hata Ubepari uchwara.
Nilitegemea watu makundi haya na watu hawa kuleta changamoto mpya kwa Watanzania, kwa kutuelimisha tuelewe wajibu wetu na haki zetu kwa Taifa, na ni nini Serikali inapaswa kutufanyia.
Nilitegemea wao wangekuwa wakweli kumuelimisha Mtanzania kwa nini ni wajibu wetu kuilipia katika huduma za jamii(afya na elimu)ambazo tulizoea kupata bure.
Nilitegemea Reforms and Mageuzi yangetumika kumuelimisha Mtanzania kuhusu uhuru wake na haki yake ya kuchagua viongozi wake, viongozi walio safi, wenye dira na nia ya kulitumikia Taifa lao na siyo Matumbo yao au himaya zao.
Uchumi wetu umetufikisha njia panda ambapo hatujui la kufanya, wanasiasa wetu (wote CCM na Upinzani) wanakimbilia kubadilisha Katiba yetu ili kujenga misingi imara ya ulaji na udhalimu wao. Hivi kweli katiba tukiibadilisha itasaidia kupunguza mzigo mzito Watanzania tunaoubeba?
Ndio maana katika Post yangu ya kwanza nimesema kuwa ili kuondokana na matatizo haya tuliyonayo inabidi tufanye kweli October.
Kama ni kwa kupiga kura au kugombea. Kwa wale watakaogombea wasikimbilie kulia kuwa tukishaiondoa CCM ndipo tutaleta mabadiliko, wasikimbilie kung,ang'ania kuingia Ikulu, Wasikimbilie kugombea ili watumikiwe. Wagombee ili kulitumikia taifa, na wawe wenye moyo safi na nia njema kwa taifa. Pia tunahitaji Damu mpya na sura mpya, iwe CCM au Upinzani.
Tunataka Mapinduzi mapya yatakayo rudisha sifa na hadhi ya Mtanzania, mapinduzi ya kweli yatakayotokomeza wale wote tuliowapa dhamana na imani yetu kutuongoza na wakakatuma vibaya dhamana hiyo. mapinduzi ya kidemokrasia na si ya umwagaji damu au nguvu.
Tunataka mapinduzi ambayo yatamuondolea Mtanzania Umasikini, Ujinga, Njaa na Maradhi.
 
October 2, 2000

Kishoka
Member
posted 10-02-2000 02:54 http://www.nyenzi.com/cgi/ubb/ubbmisc.cgi?action=getbio&UserName=Kishoka
Dues, Usimaindi, Winnie na wengine
Nashukuru sana kwa mawazo yenu. Lakini safari yangu ni bado ndefu sana. Wakati utakapokuwa muafaka, basi nitajitokeza kama Hon. Milosevic alivyofanya.
Napenda niongeze haya.
Usimaindi
Maswali yako ni mazuri mno na ni kitu tunachotakiwa kuwauliza wanasiasa wetu wanaogombea uongozi. Nafikiri Wananchi tuwe wakali kwa hawa wanasiasa, kwa kuwa wadanganyifu.
Kila kampeni zikifika wanaomba tuwaongezee miaka 5 zaidi, umeme hakuna,Pembejeo hakuna, barabara mbovu, Afya na Elimu vimebakia wasiwasi na bei za mazao ni za chini. Hawa hawastaili kupigiwa kura, wanatakiwa wachapwe mijeledi(kwa kutowachagua)na kuwaacha Solemba.

Dues
Pamoja na ukaribisho wako CHADEMA, bado sijaridhika na jinsi mfumo mzima wa Siasa na vyama vya siasa nchini. Sijui ni wapi pa kuanzia kama ni kwa Liundi, Chenge au Vyama vyenyewe.
Matatizo makubwa yanayovikabili vyama vyote vya siasa(hata CCM), ni kukosekana kwa Uongozi na Mipango bora.Pamoja na hayo Umasikini (wa mfukoni),tofauti ya ki-Itikadi katika wanachama na kutofuatwa kwa Katiba na Ilani za Vyama zimeongeza matatizo.
Mfano CCM ina kambi mbili CCM(a) na CCM(b).
Kwa ninavyoelewa mimi Bwana Mkapa jahazi linamwendea kombo si kwa hiyari yake bali kutokana namgawanyiko huu. CCM-A ni ya wenye moyo safi ambao ni wachache na hawana nguvu za kutosha, Kihali, Mali au Kikatiba(Kura). CCM-B ni ya wenyewe kama wanavyojigamba. hawa ni wengi na wamekubuhu katika Re-cycle plant yetu kwenye uchaguzi. Wao ndio walioshika njia kuu za Uchumi Kichama, kiserikali na kibinafsi.

Ukija Upinzani, nako ugonjwa unaoikabili CCM umeenea. Kuna wenye moyo safi na walaji.Kuna tofauti za kiutendaji wa nani awe nani(kugombea umashuhuri ili kutukuzwa) Katiba hazifuatwi na watu wanagombea Uwenyekiti ili kutawala ruzuku. CCM-B wanatumia weakness ya Upinzani kujiimarisha.
Vyama vyote vinategemea ruzuku ya serikali na kwa kuwa CCM iko madarakani, basi mzigo mwingine wa kuendesha chama uko serikalini kutokana na nafasi/vyeo walivyonavyo hawa Wakubwa.
Upinzani bado una mushikeli, katiba hazifuatwi na huvunjwa kila siku(eg. NCCR, TLP) kukidhi haja ya wachache. Responsibility and Accountability bado haipo, nilitegemea wao wangekuwa wa kwanza kuonyesha mfano kwa CCM lakini bado sijaona labda vyama viwili au vitatu.
Upinzani itabidi ichuje(hasa nafasi za uongozi) wale wote walioshindwa CCM na kukimbilia Upinzani. Upinzani usishabikie kupokea mateka au wakimbizi kutoka CCM, wengi wao ni Makapi na Wameoza. Hawa ndio wanaoambukiza magonjwa yaliyokomaa CCM.
Upinzani unabidi uendeshwe Scientifically kama kuna nia ya kuingoa CCM. Kuingoa CCM na kuleta Mageuzi hakutaletwa kwa kuingia Ikulu pekee yake, bali ni kuleta msukumo wa kubadilisha na kuboresha maisha ya mwananchi wa Tanzania.
Upinzani unabidi Uhubiri mambo ambayo CCM imeshindwa kuyahuburi na kuyaweka wazi kwa Wananchi.
Kundi Mmoja ambalo linaloweza kushirikiana na Upinzani kuleta mageuzi ya kweli ni Vyombo vya habari kama vitaacha kupiga porojo na kujenga ushabiki.

Ningekuwa mgombea ningehakikisha yafuatayo yanakuwa ngao yangu kwenye kampeni.

1. Kurudisha na kuimarisha Heshima na Hadhi ya Mwananchi na Taifa la Tanzania.
2. Kurudisha na kuimarisha Heshima na Hadhi ya kazi na kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini.
3. Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi.
4. Kubuni mbinu za kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida(haswa wenye vipato vya chini na wakulima)au kama tunavyowaita Walalahoi.
5. Kuhakikisha kuwa Sheria, Katiba na Kanuni zilizowekwa zinafuatwa ipaswavyo na vyombo vyote husika na Wananchi. Aidha kuweka maamuzi na mipango ya Serikali wazi kwa wananchi wote, kwa kuwa wao ndio waliotoa dhamana.
6. Kuwaelimisha Wananchi haki zao,wajibu wao na sehemu yao katika Taifa.
7. Kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Rushwa, Ubadhilifu, Udini, Ukabila na kutowajibika kwa watendaji wa Serikali na tasisi zake vinaendelezwa kwa kushirikisha Wananchi.
8. Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya Taifa.
9. Kuhamasisha na kuhakikisha kuwa Uzalishaji mali(Kilimo, Viwanda,Uvuvi, Ufugaji, Biashara, Madini, Utalii na Maofisini) unafanyika kwa dhati, Kisayansi,kiushindani, kiuwajibikaji na kwa ubora.
10. Kuhakikisha kuwa Huduma za Msingi zinafikishwa kwa Wananchi:- Afya, Elimu, Maji safi, Barabara na Chakula
.

Vipengele vyote hivyo kumi ni vile ambavyo binafsi naviona ni vya muhimu sana katika kumsaidia mwananchi wa kwawaida. Inawezekana kuna vingine nilivyoacha, Dues unaweza kuongezea.
Yote haya hayawezi kutimilika kwa miaka mitano, lakini kama tutajenga msingi mzuri na kuwa waadilifu na watu wenye kuweka ahadi zetu basi Katika kipindi cha miaka 10 taifa letu litakuwa na sura mpya yenye Afya.
 
Reaction ya insha ya Nicholls Boas :Mkapa's failed Presidency in Tanzania.


[FONT=Verdana, Arial]Kishoka[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]Member[/FONT]
icon1.gif
[FONT=Verdana, Arial][FONT=Verdana, Arial]posted 05-10-1999 21:51 [/FONT]Ndugu Wananchi,
napiga hodi huku kumbini na kwa maneno ya dakitari wetu aliyeko huko ughaibuni, mimi nina haya ya kusema.
Inawezekana sana kwa takwimu za bwana kuwa sahihi au zina walakini. Je tukimleta Mrema barabara zitajengwa? Sera za kiuchumi za wapinzani ni bora , sera hizo ni zipi ambazo zinaweza kubadilisha nchi yetu kwa miaka mitatu bila madhara?
Huyu Docta, ni wapinzani gani anaowazungumzia ambao wameshindwa kujenga nyumba zao na kutoa boriti kwenye macho yao, itakuwa ni kibanzi kwa jirani? kila siku kugombea kuwa mwenyekiti na kuchukua ruzuku.
Ukweli ni kwamba we are on a recorvery program and our priority is to settle our external debt that had matured 6 or 7 years ago. Sambamba na kulipa madeni uzalishaji mali wetu umekuwa ukishuka kila mwaka, kuanzia kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, madini hata viwanda. Je bwana Docta anatakwimu za uzalishaji mali wetu ulivyoshuka?
Je anajua kuwa tunaishi kwa kukopa na imports zetu ni karibu mara 5 ya exports zetu?
Je anajuwa kuwa viwanda vingi vimeshindwa kuendelea kwa ajili ya mazoea ya kutegemea ruzuku kutoka hazina na wahisani?
Je swala la uongozi bora ni la Mkapa na CCM pekee yake au ni jukumu la watanzania wote kuwajibika katika shughuli zote za uzalishaji mali?
Huyu Docta anaweza kutuambia kuwa hii free economy ambayo tumeiadapti 1990's inasema hakuna cha bure tena na imekuwa vigumu kwa wananchi kuelewa hivyo na wanasiasa wote CCM na upinzani ni wajibu wao kumwelimisha mwananchi sababu za kulipia matibabu na elimu na hakuna cha bure tena na kuacha kusingizia ulalahoi?
Je docta anaposema hali ngumu anafananisha maisha ya Baltimore na Kisiju? haoni tofauti ya muundo wa maisha na shughuli za utendaji kazi zilivyo tofauti?
Je Docta wewe ni dakitari wa nini? Who are conies if not all those who abuse the social systems of a country. Je ni CCM pekee yake which is conny or is the society as whole? alamsiki
[/FONT]
 
Reaction ya Boas inaendelea...


[FONT=Verdana, Arial]Kishoka[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]Member[/FONT]
icon1.gif
[FONT=Verdana, Arial][FONT=Verdana, Arial]posted 09-10-1999 17:46 [/FONT]Dostana and others,
Nafikiri kuchoka kwetu kuona serikali yenye watu wale wale ndiyo kunakofanya tupige domo la kutaka tubadilishe dictator. watu walioko opposition walikuwa katika same system na wameshindwa kutuonyesha wananchi ni kipi tofauti watafanya. Chukulia mfano Mrema , tamaa ya kuwa mwenyekiti kila anapokwenda, angalia jinsi upinzani ulivyoanza the Original NCCR before the big split that led to 10 or more opppositipon parties.
Je kama hawa wapinzani wameshindwa kuwa na uongozi bora katika vyama vyao itakuwa nchi nzima? si heri kuendelea na aliyeko tuliyemzoea na matatizo yote. Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Mtikila alipoanza kwa kusema kubadilisha raisi ni kubadilisha dictator au sura katika kuta zetu(picha). Bila kubadilisha tabia zetu na mfumo wetu kama jamii hakuna faida ya kubadilisha raisi na kutegemea kuwa kila kitu kitakuwa sawa.
Mabadiliko katika jamii ni katika ngazi zote za jamii kuanzaia mtu mmoja, familia, kijiji, wilaya mpaka taifa.
Kama wananchi wote tutapiga vita rushwa kwa kukataa kutoa au kupokea rushwa hapo tutakuwa tumepiga hatua kubwa kuliko kikosi cha kuzuia rushwa. Kupiga vita rushwa siyo kazi ya mkapa pekee yake au idara ya kuzuia rushwa, ni jukumu la kila mtanzania na tusitumie visingizio vya hali ngumu, mishahara midogo, ili tuhalalishe rushwa.
Rushwa ni utumwa na ni kitu cha kuogopewa na kutokomezwa. Kwanini tusitumie njia halali katika shughulli zetu? ndiyo kuna wakubwa walioko kwenye madaraka ambao ni currupt lakini kama na sisi tunajifariji na kusema kuwa hata fulani anafanya kwa hiyo ni haki yetu kufanya kama yeye hayo ni makosa makubwa. Labda tuanzishe firing squad kwa kila mtoa na mpokea rushwa anyongwe hadharani labda watu watabadilika. Rushwa imeota mizizi mikubwa mno kwa maana ni kazi kumtoia kwenye hatia mtoaji na mpokeaji.
Suala lingine Mdosi umesema kuwa huoni maendeleo yoyote. Je kama wengine wote walivyouliza kipimo gani tunatumia kupima maendeleo ya tanzania?
Suala la kukusanya kodi ndio lipo lakini priority yetu imekuwa ni kulipa madeni na siyo maendeleo. ndiyo sababu mambo mengi ya maendeleo yanaenda polepole. Lakini kinachoipa maendeleo nchi ni kukusanya kodi tu? je uzalishaji mali wetu ukoje? ukiangalia takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji mali umeshuka mno na kwamba sasa hivi tunategemea mno foreign products, kuanzia magari, madawa hata chakula. We can not keep on blaming nature with its El nino while tumepiga vita mabwana shamba na hakuna anayeheshimu wakulima kwa ajili ya "USOMI" wetu.
Viwanda vingi vimefungwa kwa sababu ya substitute products that are imported and to some extent of better quality.
Could yo tell me why should we import cement while we have three cement factories? Isn't this some kind of manipulation by one retailor or wholesaler who imports the cement at a cheap price and create monopoly by lowering the price and make twiga cement to shut down.
Free market economy has really screw us we depend on imports to the point no one wants to produce.
Tell me mdosi when some of our traders used our foreign exchange alocation to import toys and other luxury needs and seek for import duty and tax exemption and sell the products with a margin of 600% profit. Watu kama hawa wanastahili kunyongwa kwa sababu wanaliibia Taifa na ndio wanaochochea wizi, rushwa na ubadhirifu katika jamii na kuishi kama miungu watu.
The Last thing to you Mdosi if you are not aware, Watanzania tumekuwa wavivu, baada ya serikali ya awamu ya pili kuja, kila mtu amestarehe na kusema ewa ni wakati wa kula sasa. Kisa Nyerere kaondoka. Sera za ujamaa hazikuwa mbaya tatizo lilikuwa ni utekelezaji. Je hali yetu mbaya ya uchumi mpaka lini tutaendelea kuilamu kupitia mgongo wa Kifimbo kwamba alituacha masikini? Je ina maana kuwa miaka kumi ya awamu ya pili ndiyo tumetajirika? kwa kuwa wazembe, wavivu, wezi na wala rushwa kwa kutumia Rukhsa?
Simlaumu Mwinyi kwa maana yeye ni binadamu kama sisi. Je tumetumia udhaifu wake kujitajirisha na kisha kumtupia lawama kama tulivyofanya kwa nyerere?
Kwa nini leo panapoanza kuwa na udhibiti katika serikali pamoja na mfumo wa uchumi tunaanza kuuita Ukapa. Je Ukapa ni hali ya kuwa masikini ? au tafsiri yake ni nini
Tusipobadilisha mienendo yetu na kuongeza juhudi na kuwa na nidhamu katika shughuli zetu zote katika jamii, kamwe hatutafika popote tutatafuta Raisi mwingine, chama kingine na serikali nyingine kutupia lawama za umasikini wetu.
[/FONT]
 
Tamati kuhusu Boas..


[FONT=Verdana, Arial]Kishoka[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]Member[/FONT]
icon1.gif
[FONT=Verdana, Arial][FONT=Verdana, Arial]posted 09-10-1999 22:14 [/FONT]Pobo DL,
Akhsante sana, lakini nafikiri nitaendelea na aya zangu kama ifuatavyo.
Ndugu Dostana(Mdosi) & Company,
Mengi yamezungumziwa kuhusu elimu na afya ambavyo ni vitu muhimu katika maendeleo ya jamii. Kusema ukweli huduma za Afya na Elimu zimedoroa kwa zaidi ya Miaka 15 sasa. Je unaikumbuka taasisi ya elimu ya watu wazima ? je ni nani aliyeifunga? je wakati serikali ilipointroduce cost sharing katika chuo na afya, wananchi waliambiwa sababu za msingi zilizofikia hatua hiyo?
Ukweli unauma na ni mchungu. baada ya kuishi maisha miaka arubaini jangwani Musa (kifimbo) alituacha katika hali ngumu kiuchumi kwa ajili ya siasa za ujamaa na kujitegemea. katika miaka 20 ya kwanza tangu tuwe huru , huduma za afya na elimu zilitolewa bure.
Tulikuatumezoea maisha ya Dezo lakini we do noty take into account how costly it was to the nations ecenomy bearing the fact that our productivity had started to show signs of slumping.
At the Time Kifimbo left our currency was still strong though we were forced to devalue by our darlings IMF and World bank.
Came Rukhsa when "liberazition of trade" took over and madukas were full of imported stuff and a great influx of importing cars begun. Lakini furaha ya macho haiumizi duka we started braging o uchumi wetu ni mzuri maduka yamejaaa, barabara zimejaa, kila kitu unaweza kukipata madukani. Where was the purchasing power? If you conducted stock taking of madukas you would have foound that most of them hardly sold anything kwa mwananchi wa kawaida or as we call them now walalahoi.
The only goods that had good trading circle were hardware, misumari, rangi, vifaa vya ujenzi , vipuri and somehow pembejeo kwa wakulima.
At the same time no one in the business community paid attention on importing any medical supllies or educational materials.
We have pharmmacy mshenzis and masumin who sale stationaries, Je text books and stethascope/microscopes nani alikuwa anaziuza was it Aisco, Naphco or TEs?
1992 the CCM tunayipiga vita came with azimio la Zanzibar ambalo neno ujamaa na kujitegemea became a poison in the society. It was the time when Rukhsa was "remixed" and if I am not wrong leadership code that had govern during mwalimu was flushed in the toilet and wakubwa na viongozi with their acomplices wakaanza kujichotea.
Mdosi, conditions za Imf and world bank lbrought us to a brink because we looked at the ERP and SAP as miunguz wa kutuletea maendeleo. Wasaomi wetu wakashangilia hewa na wananchi wakasema sasa kazi basi. lakini masharti yalitaka kila nyanja ijitegemee na serikali iache kutoa ruzuku kwa viwanda, wakulima, elimu na afya. watu wakawa wanapunguzwa kazi, uzalishaji mali unashuka, wizi ukaongezeka lakini fahari ya macho ikatupofusha,
The truth is it is not possible for the govt to foot/subsidize medicare and education. Mambo yakusema sisi ni masikini na walalahoi inabidi tuyaache. Wenzetu wote wanalipia kila kitu hakuna cha bure, Je huko Oklahoma unatibiwa bure?
Inabidi Serikali kwa ujumla pamoja na pamoja na wapinzani kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kuongeza uzalishaji na kwamba serikali haiwezi kuwa yaya(babysitter and spoonfeder) tena. Mishahara ya madaktari, wuguzi na waalimu italipwa kutokana na ada zitakazotolewa na wananchi.
Free market economy ni ngumu jamani na siyo rahisi. Aliyenacho ataongezewa na asiyekuwa nacho atanyanganywa, msahafu umesema. Tumeukata na kuukimbia ujamaa, Capitalism is not a joke, tell me Salim in oklahoma na ugraduate wako kama hufanyi Odd jobs?
Wengi wetu huku tunafanya kazi yeyote inayokuja ili tusurvive, dhana hii ingekuwepo nyumbani tungekuwa mbali sana na huduma tunazolilia serikali izishughulikie zingeshughulikiwa. Let us not blame the Serikali for every thing while it is our responsibility to take care of ourselves and make sure that we are accountable and responsible for our country socio-economy welfare. Kwa Jasho lako Utaishi Mungu alimwambia Adamu 7000 years ago.
[/FONT]
 
Mzee, ulikuwa umezihifadhi wapi? Je naweza kupata nakala za posts zangu pia?
 
Mzee, ulikuwa umezihifadhi wapi? Je naweza kupata nakala za posts zangu pia?

Ulikuwepo Nyenzi? ulikuwa ukitumia jina gani? nina posti kadhaa ambazo niliwahi kuzihifadhi kwenye disk baada ya Nyenzi kuanza kusuasua lakini it was a bit late, nikaweza okoa chache sana. Ninaz kwenye disk kama word documents, nitaziambatanisha hapa wavuni soon.
 
Mapinduzi ya Viwanda kuimarisha uchumi


[FONT=Verdana, Arial]Kishoka[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]Member[/FONT]
icon1.gif
[FONT=Verdana, Arial][FONT=Verdana, Arial]posted 10-10-1999 19:28 [/FONT]Bwana Powers,
The only way we can revolutionize of our industries particularly those by indeginous citizen is to give full support in the local industries that deals with designing and manufacturing of tools, electrical and machinery products.
I think Sido and NDC were introduced to motivate and oversee the growth of local industries. but right now I am not sure what are they doing though Mr Simba, after his budget speech he spoke of something about reviving SIDO and NDC.
Tuna shida moja Powers, na shida hiii imetutawala sana watanzania. Ni tabia ya kudharau home products na kukimbilia imports. Hii imesababisha viwanda vingi kufungwa na suala la maendeleo katika nyanja za ufundi, uhunzi hata useremala kurudi nyuma.
Hatuheshimu jitihada za wazawa katika kujiendeleza katika nyanja za sayansi na teknolojia. Kulikuwa na shulue nyingi za ufundi lakini sidhani kama zinapewa mwamko na changamoto katika kubuni namna mpya ya kutengeneza vitendea kazi.
Angalia wenzetu wa China walivyoendelea na katika sayansi na teknolojia, hata kama wameipata kwa wizi. Ukiangalia kwa makini sana ni jinsi gani China, pamoja na kuwa ni nchi ya kikomunisti(Kijamaa) na "historia ya ukandamizaji wa haki za binadamu", lakini imepiga hatua kubwa kimaendeleo kiasi kwamba inakuwa tishio kwa nchi zilizoendelea.
Bahati mbaya sana pamoja na urafiki na undugu mkubwa uliopo kati yetu na wachina, bado tunaabudu na kukimbilia katika nchi za magharibi(zilizoendelea) na huko ndiko tunapopata masharti ambayo sasa yanatuumiza kiuchumi.
China ni mnyonge mwenzetu lakini amejitahidi kujifunza kwa kuiga, kuiba na kubuni vifaana shughuli za sayansi na teknolojia na sasa kila mtu anamtegemea hata nchi za magharibi.
Watanzania hasa nyumbani tunapoona vitu vimetengenezwa China tunadharau na kukimbilia vitu vya magharibi ambavyo ni ghali kwa ajili ya Cost of production.
I know you have been to USA and know that almost everything(Consumer Products particularly electronics) reads made in China, malaysia, Thailand, Mexico, Taiwan and even Kenya and Botswana.
Tutapanuka kama tutakubali na kuweka mkazo katika kujifunza mbinu mpya za sayansi na teknolojia na kama tutaheshimu ufundi tulionao. Wenzetu walipitia hatua zote kufikia hapo walipo.Industrial revolution ilianzia wapi?
Lakini Powers siwezi kuiacha serikali bila kuilaumu kwa kushindwa kulinda viwanda vyetu na kuimarisha sekta ya sayansi na teknolojia. Je imekuwa ni wimbo tuu kwamba "ni lazima tuingie katika dunia ya leo ya sayansi na teknolojia" wakati hata majembe yanaanza kutushinda kutengeneza? Sijui UFI, Urafiki, Mwatex, Voil, General Tyres na ALAF kama bado viko hai na vinahimili competition from imported goods. Kifimbo alisema Wenzetu wamefika Mwezini sisi bado tunatambaa. Inabidi tukimbie ili tuweze kufika mwezini.
[/FONT]
 
Lugha yetu Kiswahili


[FONT=Verdana, Arial]Author[/FONT] [FONT=Verdana, Arial]Topic: Tuimarishe Lugha Yetu ya Kiswahili[/FONT] [FONT=Verdana, Arial]Kishoka[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]Member[/FONT]
icon1.gif
[FONT=Verdana, Arial][FONT=Verdana, Arial]posted 10-10-1999 20:13 [/FONT]Webmaster na Waungwana,
Napenda kutoa hoja.
Kiswahili, lugha yetu kuu wana wa Tanzania na watu wa Afrika Mashariki ni lugha ambayo imetufanya tuonewe wivu na watu wengi duniani hasa Barani Afrika.
Ukichukulia kwa msingi kuwa tuna zaidi ya makabila 130(ethnic gruops) na wote tumeunganishwa na kuwa wamoja kwa kutumia lugha hiii marudufu. Amani, utulivu na mshikamano wa watanzania umetokana na lugha hii ambayo katika miaka 100 ijayo kuna hatari kuwa inaweza kuwa Lugha kuu Afrika, na kwa Jamii za watanzania lugha za asili zinaweza kusahaul;ika.
Kwa sasa hivi takwimu zinasema kuna wazungumzaji kiswahili zaidi ya milioni 60 duniani, na kiswahili kimekuwa ni lugha ya mawasiliano tu.
Changamoto ninayotoa kwenu enyi wana bodi ni kwamba ni Lini tutakapokiimarisha kiswahili na kukifanya kiwe lugha kuu katika matumizi yetu ya kila siku kuanzia nyumbani, mashuleni, makazini hata katika ngwe na viwanja vya kimataifa?
Nia yangu ya kusema hivyo ni kuwa katika jamii zote nilizowahii kuishi nazo(kimataifa) kila jamii inajigamba kwa kuwa na lugha kuu inayotumika katika nchi yao na hawaoni soni(aibu) kutumia lugha yao. Kwa bahati mbaya sana na labda huu ni ugonjwa mbaya, watanzania tunashindwa kujivunia lugha yetu na tunakimbilia kutukuza lugha za wageni.
Nitatoa mfano mmoja ambao ni mkubwa. Imekuwa ni kawaida yetu kumcheka mtanzania ambaye haongei kiingereza vizuri au haongei kiingereza kabisa na na tumefikia hatua ya kuwaita hao ndugu zetu washamba, wakuja au hawajasoma na kuwacheka. Kuongea na kutumia kiingereza kumetufanya kujenga matabaka ya walioendelea(wasomi) na wasioendelea. Na hii inatupeleka pabaya kwa sababu ya kudharau lugha na utamaduni wetu na kukimbilia lugha za kigeni.
Natumaini wengi wetu tumewahi kutembelea sehemu mbalimbali duniani na tumeona jinsi inavyotubidi kujifunza lugha zao na mara nyingine ni vigumu kupata mtu anayezungumza kiingereza.
Wenzetu wote ukiondoa waafrika, wanatumia lugha zao kwa ajili ya mawasiliano yao ya kila siku na lugha zao zinatumika katika kufundishia masomo katika ngazi zote kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu.
Ukiangalia kwa makini nchi hizi zimepiga hatua kimaendeleo katika nyanja zote za biashara, kiuchumi, sayansi na teknolojia kwa sababu moja kuu. Elimu inayotolewa katika nchi hizi ni katika lugha wanayoilelewa na waliyokuwa nayo. Mfano China, Japan, Russia, Norway, Brazil nk.
Kiingereza, Kifaransa au lugha yeyote ile ya kigeni zimefundishwa kama lugha za ziada na hazijatumika katika kufundishia masomo mengine. Masomo mengine yetu iwe ni hesabu, fizikia, historia, uchumi,udaktari nk, yamefundishwa kwa lugha zao za asili.
Kwa kufanya hivyo idadi ya watu walioenda shule na kufaulu katika nyanja mbalimbali imeongezeka kwa ajili ya kutumia lugha wanayoifahamu vizuri katika kujielimisha.
Hii imesaidia sana katika maendeleo ya taifa lolote lile hata kama taifa hilo ni bado masikini, lakini kunatoa nafasi kubwa ya kupiga hatua kimaendeleo. wengi wetu bado hatukielewi vizuri kiingereza na hata waalimu wengi katika shule za msing na sekondari bado hawajaweza kumudu kiingereza vizuri.
Je waungwana manonaje basi tukikifanya kiaswahili kitumike katika kufundishia masomo yote ukiachia kiingereza chenyewe?
Je ule mpango wa serikali ulioanza miaka ya themanini ya kubadilisha mfumo wetu wa elimu na kufanya Kiswahili kiwe lugha kuu ya kufundishia(kutoa elimu) umefikia wapi? Napenda kutoa hoja
[/FONT]
 
Mkuu Reverend, maneno mazito sana kwenye posti zako hizo,
Mimi ninadhani badala ya kuzihifadhi kielectroniki tu, ni vyema ukatengeneza kitabu pia, kwa kufanya hivyo utakuwa umepeleka mapambano katika ngazi nyingine kabisa!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom