Kutoka mahakamani: Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake, asema Hakimu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Leo Novemba 1, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kusema kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi wake, Hakimu Simba amesema amepitia hoja zote za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu hoja za kupokelewa ama kutopokelewa kielelezo hicho, ambapo ameona akipokee.

"Mahakama inatupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka kielelezo kisipokelewe, hivyo nimekubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kielelezo kinapokelewa",

Hakimu Simba amesema sababu za kupokea kielelezo hicho ni kwamba Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake bali ni nyumba yake, hivyo haina tatizo kama ilipekuliwa na askari wa kiume.

"Kama upekuzi ungehusu maungo ya mwili wake basi kungekuwa na tatizo, lakini umefanywa nyumbani kwake".

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16, 2017.

Mbali na Wema katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kiwango cha kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

NB: Hii kesi ifutwe. Maana dana dana ni nyingi mno.

=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
Leo Novemba 1, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kusema kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi wake, Hakimu Simba amesema amepitia hoja zote za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu hoja za kupokelewa ama kutopokelewa kielelezo hicho, ambapo ameona akipokee.

"Mahakama inatupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka kielelezo kisipokelewe, hivyo nimekubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kielelezo kinapokelewa",

Hakimu Simba amesema sababu za kupokea kielelezo hicho ni kwamba Wema Sepetu hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake bali ni nyumba yake, hivyo haina tatizo kama ilipekuliwa na askari wa kiume.

"Kama upekuzi ungehusu maungo ya mwili wake basi kungekuwa na tatizo, lakini umefanywa nyumbani kwake".

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16, 2017.

Mbali na Wema katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kiwango cha kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

NB: Hii kesi ifutwe. Maana dana dana ni nyingi mno.
what was the issue in dispute, hujatuweka sawa,
 
Mkuu wanasema kuna kielelezo ambacho hakijakamilika. Wema hakupekuliwa kwenye mwili wake kwahivyo hapo lazima kesi iendelee kuunguruma. Leo hii ilitakiwa kutolewa uamuzi.

Sijui umenipata?
 
ASANTE bado nisikusumbue. Nani ameleta hoja hiyo? kielelezo hicho kinataka ku establish nini?
 
Kesi ya kubambikiziwa hiyo huchelewi kusikia hukumu ya wema ni amri kutoka juu kusikonulikana
 
NB: Hii kesi ifutwe. Maana dana dana ni nyingi mno.
Lulu amezidisha maombi siku hizi nyumbani kwake,unatakiwa umshauri kamanda wema aongeze maombi badalaya ya kutaka kesi ifutwe!.sheria ni msumeno
 
Cku hiz ni hatar hakuna kudharau kesi kama zaman sheria inafuata ipasavyo rushwa rushwa zimepungua kila mtu anaogopa wasiojulikana
 
Back
Top Bottom