Kutoka Mahakamani: Scorpion afutiwa shtaka unyang'anyi wa kutumia silaha na kujeruhi

Heeeeh! Sasa wanataka waendeleze wapi hiyo kesi? Au ndio amemsamehe?

Halafu kosa la unyang'anyi kwa kutumia silaha?? Yani moja tu,

Vipi jaribio la kuua (si kamtoa macho)

Vipi udhalilishaji (Alimvua nguo)

Na mengine mengi.

Sijaelewa bado.
Haya uliyoyaandika unaweza kwenda kuyatolea ushahidi mahakaman? au ndio mmerithi tabia za wazazi wenu za mambo ya kusikia
 
Na wewe usipende sana kuona mambo ya Tanzania ndio ya ajabu.

Mbona hushangai ya Kenya ambao walitaka kuwashtaki waisraeli kwa kumsulubisha na kisha kumuua Yesu?

Kama ni mtanzania basi badili uraia ukachague huko unakoona kuna kufaa au kufa ukazaliwe huko utuachie Tanzania yetu.
Hivi umeelewa ulicho andika au ndio mihemko imekubamba.
 
Mahakama ya Ilala imefuta mashtaka ya unyanganyi wa kutumia silaha ya mshtakiwa Salehe maarufu kama Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuombe liondolewa kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hio mahakamani.

Bado wanamshikilia kwa hio inasemekana wanambadilishia mashtaka

Source: Saint Ivuga nipo Ilala

========

View attachment 420795

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete (Scorpion). Amefunguliwa mashtaka mengine yanayofanana na ya awali ya unyang’anyanyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo Njwete amekana shtaka na kurudishwa rumande,huku Hakimu Flora Haule anayesimamia kesi hiyo akizuia dhamana.

Awali Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka yanayomkabili Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo na Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore alikubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki upya mshtakiwa huyo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho.
embu mcheki kwenye hilo vazi tukisema hii dini ya kigaidi mnakuja juu,sasa jitu linamjeruhi mtu kiasi kile halafu linavaa mavazi matakatifu na porisi wanariachia
 
Mwanzo walisema huyu jamaa hakamatiki, sasa nimeamini kweli jamaa hakamatiki, anyway hii ni fursa nyingine kwa wanaume wa Dar kuweka heshima iliyopotea, wamewarudishia mumhukumu sasa mshindwe nyie.
Mwanaume wa shinyanga huyo , dar kahamia tu.
 
Sasa hapa kizunguzungu huyu side inasemekana ni muhifadhi wa makundi ya vibaka ndomana kapigwa mwenye info zaidi atujuze manake hata ukweli hatujui ni upi?
 
Kwa mtu mwenye hekima angeanza kupata maashaka kwenye tukio hili tangu ile siku ya kwanza! Asiekujua hawezi kukutoa macho na kukudunga visu hovyo! lazima kuna sualaa nyuma ya Pazia ambalo watu ilitakiwa Wajiulize ni lipi! haya sasa!
 
Dah wee Dada ni desperate sana wallahi! Scopion ni romantic? Kwa taarifa yko amebadilishiea shtaka kutoka unyanganyi mpk jaribio LA kutaka kuua na Hugo scorpion hachomoki, I swear u need self evaluation my dear nakuonaga kule MMU lkn skujua ur level of desperate km inafikia hvi
hata Lulu alikuwa na shtaka la kumuua Kanumba...na sasa hivi anakula bata mjini..scorpion ataachiwa hakuna kesi hapo.
 
Naona wengi wamepotezwa maboya na neno 'kufutiwa mashtaka'
Kuna kuachiwa huru kwa maana ya kwamba huna hatia! Huyu hajaachiwa huru na bado ni mtuhumiwa
Siku hizi mashtaka hayaandaliwi polisi tena bali kuna wanasheria wa serikali ndo wanafanya hiyo kazi kwahiyo kama alishtakiwa kwa kosa la unyanga'anyi lakini kama imekuja kuthibitika ni shambulio la mwili/toka maungoni kwa nia ya kudhuru! Shitaka na kwanza linafutwa na kuandaliwa lingine
Kwahiyo hii sio nafuu kwake bali yaweza kuwa ni maumivu zaidi
Tatizo lako sheria huzijui inadanganya watu....Lulu alishtakiwa kwa KUUA bila kukusudia na shtaka lake lilikuwa baya zaidi ya hili....yuko wapi sasa hivi?
 
sasa naanza kuamini kuwa hata LIPUMBA HAKUPEWA PESA YEYOTE NA CCM ni mitandao ya mwendokasi ndio ilituaminisha. back prof. hii nchi sijui ina kashetani gani kameivamia.
mkuu...Uliona wakati Lipumba akipewa hizo pesa? Huo ni uongo wa akina Mtatiro
 
embu mcheki kwenye hilo vazi tukisema hii dini ya kigaidi mnakuja juu,sasa jitu linamjeruhi mtu kiasi kile halafu linavaa mavazi matakatifu na porisi wanariachia
Amevaa kama mapadri wanavyovaa wakiwa kanisani? Hilo ni vazi takatifu la Mapadri na Maaskofu.
 
kumtoa macho mtu sio kukusudia kuua,

hiyo ni shambulio la kudhuru mwili(physical assault)
Na kumchoma visu zaidi ya mara saba cha tumboni akikishindilia na kukivuta juu kama ilivyosimuliwa, kisha kumburuta na kumweka barabarani ili akanyagwe na magari ni kosa gani?
 
mkuu...Uliona wakati Lipumba akipewa hizo pesa? Huo ni uongo wa akina Mtatiro
We are in the same line. ni mitandao ya kina mtatiro na chadomo ndio ninayoilaumu. wanazusha kitu halafu wanakomaa kutuaminisha matokeo yake watu wanaamini uzushi na uongo wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom