Kutoka Mahakamani kesi ya Mkulima : "Hoja tatu nzito" za Tanzania zabainishwa

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289
Daily News hatimae limeripoti kile ambacho msemaji wa serikali Dr. Abbas alisema ni "hoja tatu nzito" lakini akakataa kuzitaja...

1. Ndege inatumika na Rais, ina mitambo ya mawasiliano inayoweza kudukuliwa, imekwamisha kazi za Rais

2. Mkulima Mstaafu alitakiwa kukata rufaa Tanzania

3. kukamatwa kunaitia hasara Tanzania kwa kusitisha ratiba za ndege

MY TAKE:

1. Mngekuwa mnajali usalama wa mawasiliano ya Rais ndege hii isingekuwa inapakia abiria. Gari la Usalama wa Taifa haliwezi kutumika kupiga mingo za Uber nyakati za usiku halafu likikamatwa kupelekwa kituoni ukasema unajali litadukuliwa.

2. Mkulima Mstaafu hajakwepa hukumu ya TZ wala hajakata rufaa SA, Mkulima Mstaafu amekaza hukumu ya Jaji Mackanja ya 2010 kwa mujibu wa sheria za kimataifa zinasosema ukiona mali ya mdeni sugu imezagaa popote ulimwenguni omba mahakama iifunge minyororo

3. mngejali ratiba ndege zisingekuwa zinatoka kwenye ratiba kwenda kusafirisha wanasiasa na nyama za mbuzi kwenda Dubai. Watu walishushwa kwenye ndege Mbeya kumsubiri naibu spika Tulia Ackson aliyechelewa uwanjani. Wakasema watu wameshushwa kupisha mazoezi ya kijeshi! Wanatufanya wajinga. Mnajalije ratiba nyinyi????
 
Back
Top Bottom