Watu wanaitazama Tanzania kwa jicho lingine. Labda huu nao ni ubunifu wa Utawala na pengine ni mafanikio miongoni mwa mafanikio.
Watawala walianza na kile kilichoitwa kutumbuwa mafisadi na kuwasekwa ndani waliotuhumiwa. Mara ikaundwa mahakama ya Mafisadi na kutangaziwa kiama mafisadi wote. Wakati huo nchi ilihanikizwa na sauti za walibambikiziwa kesi mbali mbali na hata wengine kupatwa na vihoro.
Mamia ya Watanzania wamekaa ndani na uchunguzi haufiki kikomo. Lakini la kushangaza hizo kesi za Uhujumu uchumi zilizosajiliwa mahakamani haziendani na idadi ya wingi walioko mahabusu kwa ujhujumi uchumi. Hapo ndipo wasi wasi ulipoanzia.
Sasa baada ya miaka tulitegemea Mahakama hii itumike kutenda HAKI na kuwatia hatiani wale wote walioitwa Mafisadi. Tulitarajia Nguvu ielekezwe kuthibitisha uhujumu uchumi wa hao washukiwa waliobatizwa makosa yao tayari kabla ya Mahakama kuthibitisha na hatma yake nguvu sasa inatolewa kuwataka wakiri na kuomba kuachiliwa hapa kuna nini? Huku ndio kunaitwa kukokoteza na kujiaibisha.
Bahati mbaya Tanzania ndio inaaibishwa na watawala wetu. Tukiambiwa hatufuati sheria kuna watu wanatoka povu lililopitiliza. Unamlazimisha mtu kuomba msamaha wa uhujumu uchumi na kulipa mabilioni lakini unbaacha mahakama ya mafisadfi haina kesi inayoendelea na halafu unakazania kulipwa mapesa. Hii mahakama ina kazi gani? Nani hapa anahadaiwa kwa maslahi yepi?
Ndiyo, Tanzania inaaibishwa, inaaibishwa mifumo yetu ya HAKI na Mahakama kwa kukubali utashi wa mtu kuwa ndio utashi wa Tanzania. Ya nini yote haya?
YA NINI YOTE HAYA?
Huku ni kufeli na kutapatapa. Kuna mahala tulijikwaa. Hakukuwa na ulazima wa kufanya haya tokea mwanzo ukijuwa mwisho wake ni huku. Tulishasema, chini ya utawala wa CCM huwezi kumuadabisha mtu kwa ufisadi na wewe ukawa salama. Tanzania ufisadi uko kwenye mfumo. Baada ya kuwavuruga baadhi ya watu kwa makeke ya kujitakia, leo unakaribia uchaguzi unaanza kuona aibu. Unalazimisha watu wapige goti kwenye Chama na sasa walioitwa mafisadi kwa nguvu zote kabla ya mahakama kuthibitisha wanapewa "deadline" ya kukiri makosa nje ya mahakama na kutakiwa kulipa fedha. Narudia huku ni kutapatapa na kufanya aibu kwa Taifa.
USHAURI WA BURE
Watawala wangechora mstari mwekundu na kushughulika na Katiba mpya kuweka misingi. Hiki kilichofanyika ni hadaa na kuliaibisha Taifa.
Wale wazee na vijana waliobatizwa jina la Mafisadi wasionewe bure tatizo ni mfumo. Tunacheza na maisha ya watu kwea sifa zisizomaana na tumeshindwa kutumia fursa adhimu ya madaraka kuwaandalia Watanzania tunu ya taifa ya Katiba mpya halafu tunaleta mazingaombwe.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Katiba Mpya inawezekana.
Kishada