Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura

Lakini kama kesi ni kuzuia Makonda asiite watu, na ameshakabidhi jukumu kwa mwenye jukumu lake hii kesi bado ina mantiki?

RC akifunguliwa kesi ya kuchafua mtu akatakiwa kulipa fidia pesa atatoa mfukoni mwake au zitachukuliwa kodi za wananchi?

Issue hapa siyo kuwaita watu wa unga bali nikufuata sharia na mamlaka zilizopo katika kuwaita watu katika suala lolote la kiserikali na si kupiga miluzi au kutumia TV na redio vitu ambavyo siyo utaratibu wa kisheria au kiserikali!!!!!!!!
 
Wewe ni msemaji wa upande huo?

Any way,

Kesi kama hizi ni kama kupoteza nguvukazi za watu (kodi) kwa faida ya wachache


Mfano,


Hii kesi inaweza kuzalisha chochote cha manufaa zaidi ya kumtoa mshindi ambaye hata hivyo sio wote watakubali ameshinda?


Tunahitaji kuachana na hizi siasa, REAL Tunaichelewesha Tanzania bila sababu

Hazina faida!


Kama Hapa ni kazi Tu,

Zifanyike kazi physical, Sio illusions ambazo zinakula TIME!


HAMTANIELEWA!
Kesi hiyo Ina Umuhimu...Upande wa Mbowe ukishinda na hivyo Vifungu vikifutwa...

Serikali za mitaa hawata kuwa na Nguvu na Pia Wakuu wa mikoa hawata kua na Nguvu tena ya Kudhalilisha watu, kutishia au Kukamata
 
Wewe ni msemaji wa upande huo?

Any way,

Kesi kama hizi ni kama kupoteza nguvukazi za watu (kodi) kwa faida ya wachache


Mfano,


Hii kesi inaweza kuzalisha chochote cha manufaa zaidi ya kumtoa mshindi ambaye hata hivyo sio wote watakubali ameshinda?


Tunahitaji kuachana na hizi siasa, REAL Tunaichelewesha Tanzania bila sababu

Hazina faida!


Kama Hapa ni kazi Tu,

Zifanyike kazi physical, Sio illusions ambazo zinakula TIME!


HAMTANIELEWA!
god idea but kama watu wanaonewa waache wafungue kesi kudai haki zao.
 
Kesi ya Mwenyekiti Mbowe Vs RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura Mahakama Kuu imeshaanza na inaendelea muda huu, Chemba namba 64.

Baada ya kesi, Viongozi wa Chama pamoja na Wanasheria watazungumza na waandishi wa habari hapa hapa mahakamani kuhusu tukio la jana la Mwenyekiti kushikiliwa polisi hadi saa 7 usiku alipoachiliwa kwa dhamana baada ya kupekuliwa nyumbani kwake na kutakiwa kuripoti tena Jumatano wiki hii.

Aidha watazungumza kuhusu kesi hii ya kikatiba namba 1 ya 2017.

NB; Tunaomba mpuuze uzushi unaoenezwa kwa njia mbalimbali kwamba Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward atazungumza na vyombo vya habari leo, Ni habari za uongo.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) tarehe 10 February 2017 alifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.

Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).

Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.

Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe afungua kesi ya kikatiba dhidi ya RC Makonda

=======

Naongezea Updates tena wakati tunasubiri Tamko kutoka CHADEMA

=======

*Mkuu wa Mkoa Makonda na Kamanda Sirro hawajaonekana Mahakamani, lakini kuna Muda nlimuona Kamanda Wambura viunga vya Mahakama ila sijui akapotelea wapi.

*Jana kabla Mbowe hajakamatwa, alikuwa Kapeleka Maombi Mahakamani ili Waamuru Polisi wasimkamate Mbowe hadi Kesi yake itakaposikilizwa ila kabla ya Polisi kufikishiwa Wito wa Mahakama wakawa wamemkamata.

*Leo Mahakama imetoa Maamuzi ya muda kwamba Mbowe asikamatwe hadi Ijumaa saa saba Mchana baada ya Maombi yake kusikilizwa, kama wataamua wasimkamate mpaka kesi ya Msingi itakaposikilizwa au la.

*Kwenye hii kesi ya Msingi Mwanasheria wa Serikali ndo alikuja kuwawakilisha wakati alikuwa hajashitakiwa, Mahakama imemshauri Mbowe na Lissu kwamba akarekebishe hati yake ya Mashitaka amuongeze Mwanasheria Mkuu halafu wairudishe Jumatatu.

*Wakina Kibatala walikuwa wanalalamika kwamba Wakina Sirro, Makonda na mwenzie Wambura walikataa kupokea hati ya Mahakama, Sasa Tundu Lissu akamuuliza Mwanasheria wa Serikali, Imekuwaje umekuja wakati Mlikataa kupokea hati ya Mahakama, taarifa za kuja ulizitoa wapi wakati wahusika hawajaja, wewe umekuja kama nani? Baada ya Mwanasheria wa Serikali kuona kaulizwa swali Muhimu, Mahakama ikaamua wajadiliane offrecord ndo Wakaja na hiyo ya Kumuingiza mwanasheria wa Serikali kwenye Mashitaka.




Yaani huwa nikimsikiliza Tundu lisu kuna kitu huwa kinajiongeza kwenye ubongo wangu sijui kwa nini
 
MAAMUZI MAHAKAMA KUU: Mahakama Kuu Dar imeamuru kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe asikamatwe wala kuwekwa kuzuizini hadi kesi yake dhidi ya RC Makonda, Kamishina Sirro na Mkuu wa Upelelezi Dar, Wambura itakaposikilizwa Ijumaa, wiki hii.[HASHTAG]#MwananchiLeo[/HASHTAG]

94187f59912f8cbc19d179aecbe0696a.jpg


[HASHTAG]#mwafa[/HASHTAG]
emoji125.png
emoji125.png
"Hivi ni mahakama gani hiyo na hakimu gani huyo aliyetoa hii hukumu!? ...i wish i could be judge"
 
Hivi kweli wewe ni binadamu mwenye akili timamu kuandika hivyo!
Mkuu, neno akili timamu ni subjective...! In case kama nimekukera, take easy! though nakukumbusha kuwa anza kufuatilia mambo yanavyokwenda kwa mapana yake. usiishi kwa ajili ya kuishi...No!
 
Wewe ni msemaji wa upande huo?

Any way,

Kesi kama hizi ni kama kupoteza nguvukazi za watu (kodi) kwa faida ya wachache


Mfano,


Hii kesi inaweza kuzalisha chochote cha manufaa zaidi ya kumtoa mshindi ambaye hata hivyo sio wote watakubali ameshinda?


Tunahitaji kuachana na hizi siasa, REAL Tunaichelewesha Tanzania bila sababu

Hazina faida!


Kama Hapa ni kazi Tu,

Zifanyike kazi physical, Sio illusions ambazo zinakula TIME!


HAMTANIELEWA!
Na kweli hautaeleweka kwa maana msingi wa kesi hujui
 
Mkuu, neno akili timamu ni subjective...! In case kama nimekukera, take easy! though nakukumbusha kuwa anza kufuatilia mambo yanavyokwenda kwa mapana yake. usiishi kwa ajili ya kuishi...No!
Duh watu wana hasira aisee!!!
 
Kiu Taratibu hapo Mwanasheria wa Serikali ndio ata wa Wakilisha

Sababu hayo matendo walitenda muda wa kazi
 
Back
Top Bottom