figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Kesi ya Mwenyekiti Mbowe Vs RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura Mahakama Kuu imeshaanza na inaendelea muda huu, Chemba namba 64.
Baada ya kesi, Viongozi wa Chama pamoja na Wanasheria watazungumza na waandishi wa habari hapa hapa mahakamani kuhusu tukio la jana la Mwenyekiti kushikiliwa polisi hadi saa 7 usiku alipoachiliwa kwa dhamana baada ya kupekuliwa nyumbani kwake na kutakiwa kuripoti tena Jumatano wiki hii.
Aidha watazungumza kuhusu kesi hii ya kikatiba namba 1 ya 2017.
NB; Tunaomba mpuuze uzushi unaoenezwa kwa njia mbalimbali kwamba Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward atazungumza na vyombo vya habari leo, Ni habari za uongo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) tarehe 10 February 2017 alifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.
Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).
Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.
Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe afungua kesi ya kikatiba dhidi ya RC Makonda
=======
Naongezea Updates tena wakati tunasubiri Tamko kutoka CHADEMA
=======
*Mkuu wa Mkoa Makonda na Kamanda Sirro hawajaonekana Mahakamani, lakini kuna Muda nlimuona Kamanda Wambura viunga vya Mahakama ila sijui akapotelea wapi.
*Jana kabla Mbowe hajakamatwa, alikuwa Kapeleka Maombi Mahakamani ili Waamuru Polisi wasimkamate Mbowe hadi Kesi yake itakaposikilizwa ila kabla ya Polisi kufikishiwa Wito wa Mahakama wakawa wamemkamata.
*Leo Mahakama imetoa Maamuzi ya muda kwamba Mbowe asikamatwe hadi Ijumaa saa saba Mchana baada ya Maombi yake kusikilizwa, kama wataamua wasimkamate mpaka kesi ya Msingi itakaposikilizwa au la.
*Kwenye hii kesi ya Msingi Mwanasheria wa Serikali ndo alikuja kuwawakilisha wakati alikuwa hajashitakiwa, Mahakama imemshauri Mbowe na Lissu kwamba akarekebishe hati yake ya Mashitaka amuongeze Mwanasheria Mkuu halafu wairudishe Jumatatu.
*Wakina Kibatala walikuwa wanalalamika kwamba Wakina Sirro, Makonda na mwenzie Wambura walikataa kupokea hati ya wito ya Mahakama, Sasa Tundu Lissu akamuuliza Mwanasheria wa Serikali, Imekuwaje umekuja wakati Mlikataa kupokea hati ya Mahakama, taarifa za kuja ulizitoa wapi wakati wahusika hawajaja, wewe umekuja kama nani? Baada ya Mwanasheria wa Serikali kuona kaulizwa swali Muhimu, Mahakama ikaamua wajadiliane offrecord ndo Wakaja na hiyo ya Kumuingiza mwanasheria wa Serikali kwenye Mashitaka.

Wakuu ni vyema nikawatambulisha kwenu mawakili wasomi watakaomwakilisha Mh.Mbowe katika kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Kamanda Sirro na Wambura. Kesi hii ambayo imechukua attention kubwa sana siku ya leo itakwenda kutoa maamuzi muhimu sana sio kwa Mbowe tu bali ni kwa Watanzania wote dhidi ya ulevi wa madaraka
Mawakili na Majaji majina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu ndani ya mioyo ya Watanzania.
- Wakili Msomi na mgombea uraisi Tanzania Law Society-Tundu Lissu
- Wakili Msomi Peter Kibatala
- Wakili Msomi John Mallya
- Wakili Msomi Albert Msando
Watanzania watambue kwamba hukumu ya kesi hii itatusaidia wengi bila kujali itikadi zetu, kujua haki zetu kwani ulevi wa madaraka kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa utaweza kumdhalilisha yeyote popote Chato,Sumbawanga,Iramba, Newala na kwingineko ambapo Wakuu wa Wilaya wameonyesha kutokuzingatia haki za kikatiba na kisheria.
Kama ni maombi basi hapa ndipo panapostahili maombi kwa mawakili na majaji ili watumie weledi wao vyema kufanya maamuzi. Dalili ya mvua ni mawingu,tetesi za Makonda na Sirro kujificha kutokana na wito halali wa Mahakama ni dalili nzuri