JUkonga
Member
- Dec 30, 2015
- 14
- 13
Mahakama Kuu ya Tanzania leo imesikiliza Shauri la kupingwa kwa Ushindi wa Mbunge wa Ukonga Mh. Waitara Mwita Mwikwabe, katika shauri hilo upanda wa wajibu maombi uliwakilisha na Wakili Msomi Dr. Onesmo Kyauke anayemtetea mh. Waitara, Wakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala.
Kesi hiyo no. 10 ya 2015 inayosikilizwa na Jaji Halfan wa mahakama kuu ilianza kwa upande wa waleta maombi kuleta marekebisho ya Petition na kuwapatia nakala mawakili wa upande wa wajibu maombi.
Ndipo ulipofika muda Wakili msomi Dr. Onesmo Kyauke akaiomba mahakama ijiridhishe kama maombi hayo yaliletwa ndani muda unaotakiwa kisheria ambao ni ndani ya Siku 30 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi. Hoja iliyowasilishwa na Wakili Msomi Dr Onesmo ni kwamba matokeo ya Ubunge wa Ukonga yaliyompa ushindi Waitara yalitangazwa tarehe 27.10.2015 saa kumi alfajiri na maombi ya upande wa Jerry yalifunguliwa mahakama kuu tarehe 27.11.2015 ambayo ni siku ya 31 kinyune na sheria ya Uchaguzi inavyotaka.
Baada ya mahakama kusikiliza pingamizi hilo la mawakili wa upande wa wajibu maombi, Jaji Halfan amewapa muda kila upande ukajiandae ili siku ya Ijumaa tarehe 5 February 2016 mahakama isikilize maelezo ya pande zote kwenye hoja ya muda wa shauri kufunguliwa.
Kwa Maelezo ya Wakili anayemwakilisha Jerry, anadai wao walikuwepo siku ya tarehe 26 na 27 October 2015 matokeo ya ubunge hayakutangazwa hadi alfajiri ya tarehe 28 october 2015 ndipo matokeo yakatangazwa jambo ambalo lilipingwa na mawakili wa upande wa wajibu maombi.
Jambo lingine lililoleta utata ni kitendo cha maelezo ya mawakili wa Jerry kutokutaja siku ambayo matokeo yametangazwa na document yeyote inayoonyesha matokeo ya Ubunge.