Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya James Mbatia kupinga mchakato wa Job Ndugai kujiuzulu Uspika

Hapo ni kukumbushana kufuata katiba. Mkishazoea kutokufuata katiba katika mambo yenu, mtajikuta mnajenga mazoea ambayo siku fulani isiyojulikana,itawagharimu pakubwa.
Kama nyie mnavyofuata katiba kwa kumuweka nwenyekiti wa milele a.k.a Gaidi
 
Kesi ya Kikatiba namba 2 ya Mwaka 2022 imeshaanza kusikilizwa hapa Mahakama Kuu upande wa Jamhuri unawakilishwa na Jopo la mawakili wafuatao.

1. Gabriel P Malata - Solister General (Wakili Mkuu wa Serikali)

2. Mack Lwambo
3. Mussa Mura
4. deodatusi Nyoni
5. Konsiano Lukosi
6. Hangi Chana
7. Vivian Method
8. Sandey Kaliku

Na upande wa mleta madai Ndugu James Francis Mbatia anawakilishwa na jopo la Mawakili wafuatao
1. Daimu Khalifani
2. Boniface Mwabukusi
3. Prisca Chegoro
4. Eden Silayo
5. Pasiance Mlowe
6. Mohamed Tibanyendera

Kesi imeanza kusikilizwa mnamo saa5:30 na upande wa Jamhuri wameweka mapingamizi mawili pingamizi la kwanza ni kwamba Mleta madai alikuwa na room nyingine ya kwenda kuomba Judicial review juu ya kifungu cha Katiba kilichovunjwa na pili Mleta madai Ndugu James Mbatia hajaonesha popote katika madai yake kifungu cha Katiba kilichovunjwa kimemuathiri vipi yeye personally.

Upande wa Mleta madai wanajibu hoja hizo mbili kwa kusite vifungu mbalimbali vya Sheria na kwamba pingamizi la kwanza halina mashiko kwani sheria hiyo walioitaja inahusu maamuzi ya Viongozi wakiwa kwenye Operation za kikazi ( Matamko) na haihusiani kabisa na ombi la mleta madai na Pingamizi la pili kwamba limemuathiri vipi yeye personal halina mashiko vile vile kwani Katiba imempa haki mleta madai kupitia Ibara ya 26 na kesi hii ni ya Kikatiba ni public Interest not Personal Interest

Kesi inaendelea kwa majibizano makali ya kisheria ya pande zote mbili upande wa Serikali sasa Wakili Mkuu wa Serikali anaongoza jahazi.

Baada ya Majaji wa Mahakama Kuu kusikiliza hoja za Mapingamizi ya upande wa Serikali dhidi ya shauri la Mleta Madai Ndugu James Francis Mbatia na baada ya Majibu ya Mawakili wa upande wa Mleta madai.

Majaji: Tumewasikiliza na tumesikiliza pande zote mbili lakini kama tunavyoona hii kesi inauharaka wake na hivyo mapingamizi yaliyowekwa na upande wa Jamhuri tumeyasikia na Majibu ya upande wa Mleta madai tumeyasiki ila tutaoa majibu yetu baadae lakini kwasasa tuendelee na kesi ya Msingi iliyopo mezani tumsikilize Petitioner.

Mawakili wa upande wa Jamhuri wameomba Dk 15 za mapumziko Mahakama itarejea saa 8:55 za Mchana.

BAADA YA UPANDE WA SERIKALI KUBANANISHWA WATOA NYARAKA INAYOSEMAKANA JOB NDUGAI ALIIPELEKA KWA KATIBU WA BUNGE.

Waheshimiwa Majaji naomba kujibu hoja za Upande wa Jamhuri kama ifuatavyo

Upande wa Jamhuri wameleta barua kwamba ndio Ndugai Aliipeka kwa Katibu wa Bunge na barua hiyo haipo hata kwenye Website ya Bunge wala gazeti la Serikali wala popote pale sijui upande wa Serikali hii barua wao wamepata wapi maana haipo popote pale katika taarifa za Kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai.

Ukiisoma hii barua haionekani hata imepokelewa lini na imesema Kama mlivyosikia maana yake alishajiuzulu hivyo anamtaarifu Katibu wa Bunge kwamba kama mlivyosikia je ni wapi wamesikia ??

Kinanani hao na hii ndio document yake ya kwanza iliyokwenda kwa Katibu wa Bunge kama upande wa Serikali wanavyosema?? Taarifa ipi sahihi katiba barua zote tatu??

Waheshimiwa Majaji hadi sasa Tangazo lililopo kwenye website za Bunge ni ile ya Katibu wa Bunge kukiri amepokea nakala ya Barua kutoka kwa Job Ndugai na akasema anasubiria Maelekezo kutoka kwa chama cha Mapinduzi hii taarifa ya barua ya Serikali imetoka wapi?

Na kama kweli ilikwepo why Katibu alikiri kwa mdomo wake na kwa Tangazo Official la Bunge kwamba amepokea nakala na haijabadilika hadi leo.
.
Na Barua hii inatuma a very serious not kwamba kuna taarifa za uongo zinataka kupenyezwa katika Mahakama hii.
.
Hoja ya kwamba aliandika barua kwa Katibu wa chama chake (CCM) kwa maana ndio mdhamini wake basi Ndugai alipaswa kufanya hivyo kama angekuwa anajiuzulu uwanachama wake nasio Uspika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania bunge sio chombo cha CCM.
.
Waheshimiwa Majaji Upande wa Serikali wamesema kwamba Mleta mashtaka anapaswa kulipa gharama za usumbufu wa Mahakama na Reserch walizofanya na kwamba wamepata tabu sana kujibu hoja za Mleta Madai.

Majibu yetu ni kama Ifuatavyo hawa wote wanalipwa na Serikali kwa kodi zetu kila tukinunua Sukari 18% zinarudi kama kodi sasa ni Ajabu Serikali kuomba walipwe wakati tunawalipa mishahara sasa unaombaje kulipwa mara 2? Wanasema wametumia muda wao kureserch sasa walitaka nani awasaidie kazi yao?? Nikazi yao na tunawalipa kwa kazi hiyo ndio maana wapo hapa na magari yote pale nje tumeweka mafuta kwa kodi zetu

Jaji Mgeta Tumetumia muda mwingi sana kusikiliza tuwashukuru sana Pande zote mbili kwa kuwa wavumilivu kwa siku nzima ya leo, kazi hii ni kubwa sana asanteni sana.

Tunaenda kufanya kazi hatua kwa hatua na kwa kuzingatia hoja za pande zote mbili hivyo tutaoa Uwamuzi wa Shauri hili Siku ya Ijumaa tarehe 28.01.2022

Mahakama Imehairishwa hadi Ijumaa kuanzia saa 4:00 Asubuhi

Waheshimiwa Majaji Upande wa Serikali wamesema kwamba Mleta mashtaka anapaswa kulipa gharama za usumbufu wa Mahakama na Reserch walizofanya na kwamba wamepata tabu sana kujibu hoja za Mleta Madai.

Majibu yetu ni kama Ifuatavyo hawa wote wanalipwa na Serikali kwa kodi zetu kila tukinunua Sukari 18% zinarudi kama kodi sasa ni Ajabu Serikali kuomba walipwe wakati tunawalipa mishahara sasa unaombaje kulipwa mara 2? Wanasema wametumia muda wao kureserch sasa walitaka nani awasaidie kazi yao?

Ni kazi yao na tunawalipa kwa kazi hiyo ndio maana wapo hapa na magari yote pale nje tumeweka mafuta kwa kodi zetu.

Mawakili Wa Serikali Wanataka Kusema Kwamba Job Ndugai aliandika Barua Nyingine Kwa KM Wa Bunge?
Mbatia ni malaya wa siasa na jinsia pia. Wakati wa Mwendazake aliahidiwa majimbo 20 Bungeni, hivyo akaweka mortgage nyumba yake ili apate Mkopo wa benki kwa ajili ya kampeni.

Mwendazake hakumuachia Jimbo hata moja, kwa hiyo hana ruzuku, hana chanzo cha fedha na hana haiba ya siasa zinazoendana na Rais SSH. Benki wanataka marejesho, Mbatia hana hela, atapata wapi?

Kwa hiyo ameamua kuwa msumbufu fulani ili watu wa system wamuone ni mwiba na ikibidi watafute namna ya kumalizana naye.

Mark hii post, Mbatia atasumbua sana kwa sababu ya nyumba yake ya Mbezi Beach
 
Back
Top Bottom