Uchaguzi 2020 Kutoka Lindi: Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za Chama cha ACT-Wazalendo

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Kampeni zinaendelea na leo Chama cha ACT-Wazalendo wanazindua kampeni zao Lindi, wagombea wote kwa upande wa Jamhuri na Zanzibar wameshawasili uwanjani na kwa sasa kikundi cha burudani kutoka Lindi kinatoa burudani ya utangulizi. Tuwe pamoja kujuzana yatakayojiri.

=====

Maalim Seif: Nasema wametuonea siku nyingi, sasa wakati wa uhuru umefika na mkombozi si mwingine bali ACT-Wazalendo. Sitaki nizungumze sana, ndege inanisubiri. Kazi yangu ni kuzindua kampeni na nazindua Rasmi sasa.

Bwege: Ulisikia wapi mtoto kumpa mama yake mume, ulisikia wapi? Kuna mgombea wetu ametekwa na vijana wamekamatwa ili mtu apite bila kupingwa.


Habari zaidi...

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mgombea uRais kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema akichaguliwa nakuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya serikali atakayounda na kuongoza haita wabughuzi wafanyabiashara wadogo wanaonunua mazao kwa wakulima ambao katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanatambulika kama kangomba.

Membe ametoa ahadi hiyo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mpilipili, manispaa ya Lindi. Uzinduzi ambao pia ulihudhuriwa na kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na mwenyekiti wa taifa, Maalim Seiff Shariff Hamad.



Membe alisema serikali atakayounda na kuongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais haitawabughuzi wafanyabiashara hao. Kwani anatambua kwamba uchumi wa nchi zote zilizofanikiwa kiuchumi duniani unategemea wafanyabiashara wa kati. Kwahiyo atawaruhusu wananunue mazao kwa wakulima bali walipe kodi.

Alisema hata wanaonunua mazao kwa wakulima kutoka mataifa ya nje ni kangomba wa kimataifa. Kwahiyo haoni sababu ya kuwaruhusu kangomba wa ndani kununua mazao ya wakulima. Bali kubwa ni kuhakikisha wanalipa kodi.

Katika kuhakikisha azima yake hiyo inafanikiwa, Membe amejinasibu kwamba ataunda wizara ya biashara ambayo itakuwa na wajibu wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima. Huku akihaidi kupita katika mikoa yote kuzungumzia changamoto za kila mkoa ambazo wananchi wanakabiliana nazo ili kuwapa matumaini ya kutatua changamoto hizo iwapo atachaguliwa kuwa Rais.

” Wakulima watapeleka na kuuza mazao yao popote bila ya kuingiliwa na serikali, bali walipe kodi,” Membe alisisitiza.

Aidha Membe alisema kama atakuwa Rais atapandisha mishahara ya watumishi na kuwapandisha madaraja. Kwani ni haki ya watumishi wa umma. Huku akihaidi kuwalipa fedha za likizo.

Mgombea huyo wa uRais licha ya kuhaidi hayo, lakini pia amehaidi kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali duniani. Kwamadai kwamba hivi sasa Tanzania imekuwa kama kisiwa kilichojitenga na mataifa mengine kuhusu mahusiano na ushirikiano.

Katika hatua nyingine Membe alisema anauhakika wakushinda uchaguzi. Kwani hata ndani ya Chama Cha Mapinduzi wapo wengi wanaomuunga mkono kutokana na kuchoshwa na hali ya mambo.

“Nawafurahia sana wanaCCM kwani wamechoka, wananiunga mkono. Wapo wanaosema watabaki na kadi tu,” Membe alijagamba.

Uzinduzi wa kampeni za ACT- Wazalendo ulizinduliwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad. Ambaye katika hotuba yake ya uzinduzi alizungumzia kitendo cha tume ya uchaguzi kuwaengua wagombea wa ubunge kupitia chama hicho. Hasa wagombea waliopo katika kisiwa cha Pemba.
IMG-20200901-WA0042.jpg

LINDI.jpg

IMG-20200901-WA0040.jpg
IMG-20200901-WA0041.jpg

 
Hili ndio Nyomi la Uzinduzi wa Mampezi za Kitaifa za Urais za Chama cha ACT Wazalendo.

Na naambiwa kuna Changamoto za Malipo ya Jukwaa mpaka sasa kwamba Jukwaa halijalipiwa sasa sijui Kweli aaah

Vipi wazee!
wataweza Mziki wa CCM hawa ACT?


IMG_9440.jpg

IMG_9435.jpg

IMG_9434.jpg

IMG_9433.jpg

IMG_9432.jpg

IMG_9436.jpg

IMG_9439.jpg

IMG_9438.jpg

IMG_9437.jpg
 
Hili ndio Nyomi la Uzinduzi wa Mampezi za Kitaifa za Urais za Chama cha ACT Wazalendo.

Na naambiwa kuna Changamoto za Malipo ya Jukwaa mpaka sasa kwamba Jukwaa halijalipiwa sasa sijui Kweli aaah

Vipi wazee!
wataweza Mziki wa CCM hawa ACT?


View attachment 1555458
View attachment 1555459
View attachment 1555460
View attachment 1555461
View attachment 1555462
View attachment 1555463
View attachment 1555464
View attachment 1555465
View attachment 1555466
Nataka arushe picha zitto na abdul Nondo ndio nitaamini wengine wote mtatuhujumu tunajua ufipa hamtupendi ndio maana mkaweka mapingamizi ubungo!
 
Bwege: Ulisikia wapi mtoto kumpa mama yake mume, ulisikia wapi? Kuna mgombea wetu ametekwa na vijana wamekamatwa ili mtu apite bila kupingwa.
 
TBC wamejitahidi sana kuwa wavumilivu. Bwege amemuongelea sana majaliwa lakini hawajakata matangazo.
Uvumilivu wa act utawafikisha mbali.
 
Hivi mgombea au mnadi sera akisema "wangapi wataichagua chama changu kwenye uchaguzi huu?" kamera ilitakiwa kuelekezwa wapi? Bila shaka inatkiwa kuelekezwa kwa wanaonyosha mikono

TBC na leo mnapaswa kufukuzwa tena na hata msilalamike
 
Hivi mgombea au mnadi sera akisema "wangapi wataichagua chama changu kwenye uchaguzi huu?" kamera ilitakiwa kuelekezwa wapi? Bila shaka inatkiwa kuelekezwa kwa wanaonyosha mikono

TBC na leo mnapaswa kufukuzwa tena na hata msilalamike
Hata kama wasipowafukuza lakini angalau wao act tunawapata kuliko cdm kujifanya wajuaji wakati hata online yao imewashinda kurusha live.
 
Chadema wenyewe lazima wataje CCM na Magufuli vinginevyo mikutano yao inadoda.CCM na Magufuli ndio habari ya mjini
Ccm inavyotajwa na CDM ni tofauti sana na inavyoongelewa hapa kwenye mkutano wa ACT.
Tofauti kabisaaa.

Kwenye mkutano wa chadema ikitajwa ccm basi lumumba ni maumivu ila kwa hapa hawa ACT wanavyowataja nawaona mnavyochekeleaa
 
Back
Top Bottom