Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Ila kuondokewa na wazazi c ndo guarantee ya kufanya maovu ili kujikwamua...ni wangapi wameondokewa na wazazi wao ila wamefanya shughuli halali na kujikwamua?kwa maana hyo anataka kufundisha jamii inayotuzunguka kwamba ukizaliwa na ikatokea bahat mbayaa ukaondokewa na wazazi njia nzur ya kufikia malengo ni kujihusisha na uhalifu?
We jamaa akili yako mgando sana? kwani inabidi ueleweshweje ili uelewe!!??
 
Naja
JamiiForums832274312.jpg
 
Sehemu ya 17

Nilifika pale zilipo ofisi za Daqwa na ticket yangu nilishakatiwa nilikuwa na furaha sana isiyo na kifani kurudi Tanzania haswa nikijua nitaenda kuwaona wadogo zangu nijue maendeleo yao yakoje.

Basi lilishona haswa mpaka zile sehemu za watu kupita watu walikuwa wamejaa yaani sehemu ya kukanyaga hamna mi nilikaa siti ambayo siyo ya dirishani na dirishani alikaa faza mmoja ana kitambi na mkoba wake ameupakatia vizuri sana.

Tulianza kupiga stori na kuzoeana kabla safari haijaanza, na nilimgundua ana hela kwenye mkoba baada ya kutoa burungutu la hela kumpa mtu kwa nje. Nilimtamani sana yule faza na akili ilihama moja kwa moja na amani nilikosa haswa.

Yeye alikuwa amechangamka sana, basi liliondoka na tulifika eneo la kula msosi na kuchimba dawa, tulishuka na mimi kumwambia twende chooni. Tulienda nia na dhumuni langu kuu ni kummalizia huko huko chooni, lakini haikuwa hivyo kwani watu walikuwa wanaingia kwa wingi na kutoka hivyo nilishindwa zoezi langu na roho iliniuma sana.

Tulienda kwenye eneo la msosi nikatoa hela ninunue chakula, ila yeye alisema ataninunulia hivyo nisitumie pesa yangu. Aliniagizia chips na kuku mzima na yeye hivyo hivyo na juice kubwa ya box. Alifungua mkoba na kutoa tena hela kulipia ambapo alizidi kunichanganya kabisa, ikabidi niisihi akili yangu itulie na moyo utulie kwani naelekea mjini hivyo mambo yatakuwa mazuri. Lakini wapi nafsi inakataa kata kata.

Tulirudi kwenye basi na safari iliendelea njiani stori zilikuwa nyingi namimi nikuwa nimefura kwa hasira maana naona hela hizo hapo na sina cha kufanya.

Usingizi ulimpitia na kile kimkoba kilimtoka mikononi na kikawa sasa kama kimenilalia, niliona huu ndio muda muafaka sasa baada ya kama dakika 5 basi lilisimama kuna watu walikuwa wanashuka na kuna wengine wanataka kupanda na mimi wazo la kushuka likanijia hapo hapo.

Nilisimama kuangaza vizuri hayo mazingira kama yanafaa kushuka nikasikia akinisemesha vipi tumefika Kasumulo? Nikamjibu kwa hasira sana bado faza we endelea kupumzika. Safari iliendelea na tulifika boarder mapema kabisa ilikuwa lakini bado jua halijachomoza na adhana bado haijalia kwa muda huo.

Tulishuka pale na watu walikuwa wakisubiri ofisi za migration zifunguliwe kutapopambazuka. Nilikaa nje kule na yule faza na kulipopambazuka wale waliokuwa wanaenda kugongewa mihuri passport zao upande wa Malawi na kisha kwa upande wa Tanzania. Faza yeye aliondoka na aliniacha ambapo mimi nilitulia pale maana sina passport hivyo kwa maelezo niliyopewa ni kuwa kuna mtu atashughulikia suala langu. Alikuja afisa mmoja pale na kunikazia macho kidogo na mimi nikamkazia, akaniambia maswera? Na mimi nikamjibu maswera bonukaye! Muli bwanji? Na mimi nikamjibu ndili bwino kaya inu? Na yeye akajibu tena ndili bwino! Kisha akaniambia takulandirani achimwene! Na mimi nikamjibu zikomo!

Tuliondoka na kwenda kwenye mto pale boarder, ambako nakumbuka ulikuwa ni kwa upande huu wa Malawi ila jina siukumbuki kwa kweli ndio kwa mara ya kwanza na ya mwisho niliuona huo mto. Tulizungumza mengi sana huku akinisihi lazima nijitume kwenye kazi na niache kuendekeza huruma na mapenzi. Roho ya huruma itakugharimu katika maisha yako na mapenzi yatakupoteza na kukutoa kwenye reli ya mafanikio. Alinisihi sana na kuniambia mambo mazuri yapo mbele yangu ikiwa nitasimama kama mwanaume katika nafasi yangu nasio mvulana.

Tuliondoka na kuingia upande wa Tanzania ambapo kule alikutana na baadhi ya watu na mimi nilipita na kuingia rasmi Tanzania. Alinikabidhi kwa kijana mmoja mmoja wa makamu ambaye tuliongozana mpaka Kyela. Kutoka Kyela tuliondoka usiku na kuanza safari ndani ya gari private ambapo tulikuwa wawili tu. Mimi na huyo kijana.

Gari ilikuwa inatembea kwa mwendo sana, tulifika Mbeya na pale Mbeya hatukusimama tuliendelea na safari na majira ya alfajiri tulikuwa tupo Chalinze. Pale tulikaa kama nusu saa kisha tukaanza safari ya Dar ambapo tulifika salama kabisa. Mimi nilifikishwa moja kwa moja ofisini kwa mdosi ambapo alinipokea kwa mikono miwili na kunikaribisha. Mdosi yeye ni mtu wa Machame huko.

Aliniuliza uzoefu wangu kwenye kazi za kiume na mimi nikamjibu atoe shaka yeye anipe kazi hata sasa na hatojuta. Akaniuliza tena utaweza kweli mbona unaonekana kama mtoto wa mama? Nikamwambia mwonekano wa nje hauakisi muonekano wa ndani. Hivyo aliniambia kwa leo hamna majukumu hivyo niende nikapumzike na kulifurahia jiji la Dar kwa muda wa wiki moja.

Alivuta droo nakutoa kitita cha milioni 2 ambacho aliniambia hicho ni kwaajili ya kuburudika kwa hiyo wiki moja kisha ndio nitapangiwa jukumu langu la kazi.

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
ulikuwa unakasirika kwa pesa ya watu dah!
 
Back
Top Bottom