Kutoka Kwenye Ufukara Hadi Umilionea Na Mwishoe Jela

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,041
2178642.jpg

Claus W mwaka 2005 alipopandishwa kizimbani Saturday, June 06, 2009 6:29 AM
Bahati nasibu ya euro 750,000 aliyoshinda mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani imeyafanya maisha yake yaende mrama baada ya kuangukia jela kwa makosa ya wizi baada ya pesa hizo kuisha. Mjerumani huyo aliyetambulika kwa jina la Claus W alikuwa akifanya kazi iliyokuwa ikimpatia mshahara wa euro 1,400 hadi mwaka 1997 aliposhinda bahati nasibu ya Lotto na kujishindia kitita kinene cha euro 750,000.

Maisha yake yalibadilika ghafla kwani aliacha kazi hapo hapo na kuanza kuishi maisha ya kifahari ambayo alikuwa hayajazoea.

Mwaka wake wa kwanza alioshinda lotto alinunua Mercedes Benz mpya na kuitumia kwenye safari zake za kujirusha akiwa na mkewe, shemeji yake na baba yake.

Mwaka mmoja tu baada ya kushinda Lotto, nusu ya pesa alizoshinda alikuwa ameishazitumbua.

Mwaka 1998 alinunua nyumba ya kifahari na kuendeleza maisha ya starehe.

Miaka minne baadae pesa zote alizoshinda kwenye Lotto zilikuwa zimeishamalizika zote akibakia hana hata sumni.

Kutokana na kuzoea maisha ya starehe kwa miaka saba Claus alishindwa kuishi maisha ya kawaida na kufanya kazi kama watu wengine na matokeo yake akaingia kwenye wizi ili aendeleze maisha ya starehe aliyoyaonja.

Claus alikamatwa mwaka 2005 baada ya kushiriki kwenye wizi mara 60 na kuiba vitu vyenye thamani ya euro 12,000.

Klaus alipatikana na hatia kwa makosa hayo ya wizi na kuhukumiwa kwenda jela miaka minne.

Milionea huyo wa zamani alikuwa akiulezea mkasa wake huo kwa gazeti la Ujerumani la Bild baada ya kutoka jela.
 
Kwanza tuelewane hapa, yaani mtu ana €750, 000 unamwita milionea? Halafu kwa hela hizo bora alinunua nyumba, sio nyumba ya kifahari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom