Kutoka Kwenye Ufukara Hadi Umilionea Na Mwishoe Jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka Kwenye Ufukara Hadi Umilionea Na Mwishoe Jela

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MziziMkavu, Jun 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Claus W mwaka 2005 alipopandishwa kizimbani Saturday, June 06, 2009 6:29 AM
  Bahati nasibu ya euro 750,000 aliyoshinda mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani imeyafanya maisha yake yaende mrama baada ya kuangukia jela kwa makosa ya wizi baada ya pesa hizo kuisha. Mjerumani huyo aliyetambulika kwa jina la Claus W alikuwa akifanya kazi iliyokuwa ikimpatia mshahara wa euro 1,400 hadi mwaka 1997 aliposhinda bahati nasibu ya Lotto na kujishindia kitita kinene cha euro 750,000.

  Maisha yake yalibadilika ghafla kwani aliacha kazi hapo hapo na kuanza kuishi maisha ya kifahari ambayo alikuwa hayajazoea.

  Mwaka wake wa kwanza alioshinda lotto alinunua Mercedes Benz mpya na kuitumia kwenye safari zake za kujirusha akiwa na mkewe, shemeji yake na baba yake.

  Mwaka mmoja tu baada ya kushinda Lotto, nusu ya pesa alizoshinda alikuwa ameishazitumbua.

  Mwaka 1998 alinunua nyumba ya kifahari na kuendeleza maisha ya starehe.

  Miaka minne baadae pesa zote alizoshinda kwenye Lotto zilikuwa zimeishamalizika zote akibakia hana hata sumni.

  Kutokana na kuzoea maisha ya starehe kwa miaka saba Claus alishindwa kuishi maisha ya kawaida na kufanya kazi kama watu wengine na matokeo yake akaingia kwenye wizi ili aendeleze maisha ya starehe aliyoyaonja.

  Claus alikamatwa mwaka 2005 baada ya kushiriki kwenye wizi mara 60 na kuiba vitu vyenye thamani ya euro 12,000.

  Klaus alipatikana na hatia kwa makosa hayo ya wizi na kuhukumiwa kwenda jela miaka minne.

  Milionea huyo wa zamani alikuwa akiulezea mkasa wake huo kwa gazeti la Ujerumani la Bild baada ya kutoka jela.
   
 2. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hii inafundisha kitu kimoja. Utajiri si wingi wa pesa alizo nazo mtu. Utajiri ni mentality. Utajiri ni attitude. Utajiri ni msimamo na mtazamo. Pesa hufuatia.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Maskini!!!!

  Pengine alikosa ushauri!
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...usisahau wenye 'umasikini wa akili' husema, "utanipangiaje jinsi yakutumia pesa yangu?!"
   
Loading...