Kutoka kwenye Kampeni Jimbo la Uzini Zanzibar: Dr. Slaa aweka sawa hoja ya posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka kwenye Kampeni Jimbo la Uzini Zanzibar: Dr. Slaa aweka sawa hoja ya posho

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Tumaini Makene, Jan 31, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wakuu tuko tunaendelea na pilika pilika za kampeni huku Uzini, ofcourse masuala ya yanayoendelea kujiri nitayaweka na ku-update katika thread husika unless itakapolazimu tofauti.

  Katika mikutano kadhaa tuliyoipiga leo na Mgombea wa CHADEMA, Maalim Ali Mbarouk Mshimba, Dkt. Willibrod Peter Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, ameamua kulizungumzia suala la akirirejesha katika perspective iliyo sahihi, katika misingi inayosimamiwa na chama.

  Kama mjuavyo, suala la posho ilikuwa ni ajenda iliyoanzishwa na Dr. Slaa katika bunge la tisa, akawa kinara wa suala hilo, akipambana na wabunge wa CCM na baadhi ya waliokuwa kwenye kambi ya upinzani wakati ule. Akaambiwa kila aina ya maneno na kejeli. Wakamtishia kuwa ametoa siri ya mishahara yao, hivyo ni kosa kisheria. Naye akaruka mtego wao kwa kuwaambia kama mishahara yao isiyoangaliwa wala kuendana na hali halisi ya ucuhumi na makundi mengine wanayoyaongoza, ni siri, basi yeye anauweka mshahara wake hadharani. Wakanywea. Wakakimbia. Wakashindwa vita na mapambano ya hoja. Wakasalimu amri. Hata kama hawakuwahi kukiri hivyo hadharani.

  Wakati ule kelele za Dr. Slaa zilikuwa juu ya mshahara wa sh. milioni 7 (unaohusisha posho kedekede, ikiwemo hiyo sitting allowance inayoongezwa kwa kasi ya roketi), kwa mwezi wakati makundi mengine ya kijamii, katika kada na sekta mbalimbali (mathalani katika elimu-walimu, afya-wauguzi, madaktari na watumishi wengine wa kada mbalimbali) yakiendelea kutaabika kwa mishahara midogo, isiyokuwa na posho kabisa ama kiduchu.

  Baada ya hapo, Dr. Slaa akilipigia kelele sana suala hilo wakati akinadi Ilani ya CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2010, ambayo ilieleza bayana msimamo wa CHADEMA juu ya masuala ya kulipana posho. Pia CHADEMA, kupitia kwa Kamati ya Wabunge,ikaweka msimamo wake wazi juu ya masuala ya posho.

  Katika mkutano wa bunge la bajeti, Mwenyekiti Freeman Mbowe aliweka msimamo sawa, kuwa suala sin posho za wabunge pekee, bali concept nzima ya kulipana posho, hasa kwa sitting allowance, kwa majukumu ambayo kimsingi yanakuwa ni sehemu ya kazi zao ambazo kwazo waliajiriwa au kuchaguliwa kuzifanya. Mwenyekiti Mbowe alisistiza sana suala hilo ni uamuzi wa chama, si suala la mtu mmoja. Akaongeza kuwa alikuwa anawashangaa baadhi ya waandishi wa habari na wanasiasa wa uapnde wa pili, CCM na CUF, kwa kuamua kuli-presonalize, ili kumuadhibu Zitto, ambaye alizungumzia suala hilo kwa kutumwa na Kambi ya Upinzani Bungeni, kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi.

  Hoja ilikuwa ni impact ya posho hizo. Ikafafanuliwa kama tatizo ni mishahara haitoshi kwa watendaji wa serikali na wabunge, basi irekebishwe katika kada zote, si kuacha kundi dogo la watumishi wa kada fulani, wakiwemo watendaji wa serikali, mashirika ya umma na wanasiasa, kulipana posho kubwa kwa kisingizo cha mishahara midogo na ukali wa maisha.

  Sasa leo, Dr. Slaa kakumbushia yote hayo, akiitaka serikali ya Kikwete kuwaambia ukweli Watanzania juu ya kupandishwa kwa posho za wabunge mpaka kufikia kiwango hicho kikubwa namna hiyo. Amesema kuwa serikali ya Kikwete, irejee ushauri wake kuwa ihuishe mishahara na posho za kila kada, kwani wananchi wote wanakabiliwa na makali ya maisha na uchumi unaodorora kwa ubovu wa Seikali ya CCM.

  Amesema ni aibu, kufuru na dhambi kubwa mbele ya mwenyezi Mungu, kwa serikali ya Kikwete, kuidhinisha ongezeko la posho ya mbunge kwa siku na kwa kiwango ambacho kinazidi mshahara wa mwalimu, muuguzi askari polisi, askari jeshi, n.k, watu ambao wanafanya kazi za suluba katika kulijenga taifa. Amesema ni aibu kwa taifa, mebele ya wananchi, serikali hiyo hiyo inashindwa kuwalipa vyema madaktari wake, kuboresha mfumo wa sekta ya afya, katika kuhudumia wananchi kwa namna inayowastahili katika nchi tajiri kama hii, kisha inapandisha posho za wabunge.

  Amekumbushia kauli yake aliyowahi kusema kuwa suala la posho kubwa kwa watawala huku wananchi wakizidi kutopea katika lindi la umaskini wa kipato na ukosefu wa huduma muhimu za jamii katika kufikia maendeleo yao, ni bomu lililokuwa likisubiri kulipuka "na sasa limelipuka tayari kama nilivyowahi kusema," amesema Dkt. Slaa.

  Amesema iwapo serikali ya Kikwete itaendelea na mpango huo, huku kukiwa na mkanganyiko wa ukweli juu ya ongezeko la posho badala ya kufumua mfumo wa posho serikalini, kwa watendaji na wanasiasa, kama ambavyo CHADEMA kupitia hotuba yake bungeni kilishauri, ushauri ulioendana na mpango wa taifa wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni ukiwa na kipengele hicho cha kuondoa posho, basi CHADEMA itaenda kwa wananchi kulieleza jambo hilo, ili sasa lipate hukumu kubwa ya mahakama ya umma ambao ndiyo wenye mamlaka ya nchi yao.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu nadhani haukutulia vizuri wakati unaiandika hii habari. Please ipitie upya na uifanyie editing! Of course natambua mazingira duni ya huko.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli aliyoongea dr Slaa, but nadhani magamba wamelaaniwa ndo maana wanakwenda bila hata kujua mwisho wao ni nini, wakinamwakwembe, sitta na kilango wameshatusaliti watz.
   
 4. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha iende hivyo hivyo, message sent!!!
   
 5. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama cha mandamano na sera ya posho.
   
 6. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Thanks Mkuu japokua mtiririko wa habari hauko vizuri sana ila ujumbe umefika
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naon Network inakusumbua mzee lakini Big up!
   
 8. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  chama cha mafisadi na kunyweshana sumu....
   
 9. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  One of these days linaweza kutokea tukio kubwa hapa nchini ambalo litatufanya tukapige kura upya.
  Hii serikali iiyopo imezidi vituko.
   
 10. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara hii mutamaliza maneno yenu yote mpaka mate mdomoni yawakauke lakini mwisho wa siku jimbo la Uzini hamulipati (Raza ndiye mwenye mali). Kama hamuna kazi ya kufanya vukeni Bahari muje Pemba huku mujumuike na Wanyamwezi wa Tabora na Wasukuma wa Shinyanga tuwape mashamba ya mikarafuu mutuondolee magugu na pori! Njooni huku kuna Mapesa ya Bure ya Wajomba zetu toka Arabuni, mukirejea 'Bongo' nyote mupo full vibaraghashia huku mukiwa mumejaza tende kwenye viroba.
   
 11. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Malengo ya CDM siyo jimbo la uzini pekea yake bali ni pamoja na kuhakikisha kuwa elimu ya uraia inawafikia wana Uzini. CCM kama ilivyo mazoea yake itafanya kila jitihada kuiba kura au kuhonga wapiga kura. Lakini jambo la faraja ni kuwa watu wanazidi kubadilika kwa kasi kinyume na matarajio ya CCM
   
 12. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  ninyime pesa,ninyime mavazi,ninyime chakula lakini nipe elimu,nitapata vyote ulivyonikosesha.cdm imejikita ktk kuufanya umma ujitambue na utambue wajib wa wanao wachagua ili wakifanya tofaut wawawajibishe.nafurahi kuwa ukweli haubadiliki na uongo hauna safari.watz tusimamie ukweli daima nasi tutafika tunapohitaji kufika.pale uzini wakielewa watu watano pekee ninaamini ndiyo watakaofanya na wengne waelewe.chukua mfano wa mwalimu yeye m1 ndiye anajua mahesabu lakini akifundisha wanafunzi 45 wanakuwa wajuzi wa mahesabu ndivyo kwa cdm ilivyo.
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  hatimaye Cdm yaingia Zanzibar
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  pemba +chadema=uhuru kamili.
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sioni kama taarifa ina matatizo labda ungeonyesha wapi hukuelewa tukusaidie
   
 16. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hongra Dr.Slaa wengine ni vigeugeu
   
 17. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ami waitambua Pemba weye!
   
 18. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hv kwnn hilo jimbo hakugombea slaa?
   
 19. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dr.amefanya vizuri sana kukumbushia jinsi alivyoanzisha mapambano haya dhidi ya posho za wabunge katika bunge la 9 na hatimaye Mbowe kuweka hili suala bayana katika bunge la bajeti kwamba posho si hoja ya mtu binafsi bali ni hoja yachama.

  Nakubali kwamba Zitto ni waziri kivuli wa fedha na ndiye aliyetumwa na chama kusemea chama chake. Zitto kaendeleza alipoishia Dr. Slaa kuhakikisha hoja haifi, lakini Zitto ameenda hatua ya ziada ya kuamua kuacha kuchukua posho ili kuonyesha njia. Njia pekee ya Chadema ni kumuunga mkono kiongozi wake kwa kuagiza wabunge wake wasipokee posho za vikao.

  Dr. Slaa alilisemea lakini hakuacha kupokea na bahati mbaya sana hivi sasa anapokea jumla ya fedha ambazo wabunge wanapata, na fedha hizi ni za Serikali kupitia ruzuku.

  Umma unatambua kuwa hoja ni ya CHADEMA na inasimamiwa na Zitto kama wazirikivuli wa fedha,hivyo tunategemea kuona chama kinakuwa nyuma ya Zitto ili kuipa hoja uzito na sio hivi ambapo mnaonyesha mnaumizwa na msimamo wa Zitto.Kwakweli kitendo cha wabunge wa Chadema kuungana mkono na wabunge wa CCM kutetea posho kinatia aibu sana.
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kisebusebu na kiroho papo
   
Loading...