KUTOKA KWANGU: Mitindo mbalimbali ya milango ya mbele ya nyumba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,468
9,208

Mlango wa mbele wa nyumba unakuwa katikati ya nyumba na ndio unaowakilisha mvuto wa nyumba kwa hivyo muhimu uwe maridadi. Wengine wanapendelea kuweka glass panels kwenye mlango wa mbele kama hivi kwa ajli ya kuongeza mvuto na mwanga ndani.

Swala la security kwa hapo kwenye glass sio issue kwa ajili kwa ndani kunakuwa na chuma, na wengi wetu tunaweka mlango wa mbao pamoja na grill.

Milango hii ipo ya malighafi na designs nyingi mno wewe tu ushindwe, ipo ya chuma ambayo ikiwa imepakwa rangi kabla hujaigusa huwezi kutofautisha na mbao. Hii ya hivi inauzwa imeshatengenezwa na huwa kwa wale ambao kwa security wanaweka milango ya mbele miwili pamoja (wa chuma na wa mbao) endapo utaweka hii ya chuma huna haja ya kuweka tena wa mbao wala grill.

Mlango wa mbele huwa ni mpana kuliko milango mingine kwa kuwa upana wake ni sawa na upana wa corridor uliopo.

Designs mbalimbali za milango ya mbele, hii imezibwa kote kote haina glass panels

Angalia glass panels za huu zilivyokuwa na shape moja na handle zake, unavutia

HTB1AJAcGXXXXXclXVXXq6xXFXXXN.jpg

Chanzo; Vivimachange
 
hapana. hata simfahamu
Nishawahi kuiskia hii milango ya chuma. Kuna jamaa alinisimulia nyumbani kwake Kibada kigamboni majambazi walim-tight getini wakaingia nae ndani, mke wake akawahi kukimbilia chumbani na mtoto mchanga akajifungia,chumbani wameweka huo mlango. Majambazi wakashindwa kuvunja na alipoingia huko akachukua gobole akaanza kufyatua dirishani ikabidi majambazi wakimbie!
 
Ahahaaa kama movie
 
Kazi mziru mi nna mlango mkubwa pia front window yangu ni 9x9 ambayo pia unaweza kutumia kama mlango japo sio rasmi mimi mwenyewe huwa sipendelei wafanye hivyo
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom