Kutoka kwa Padre Silvio Mnyifuna kuna kitu cha kujifunza hapa!

Enugu

Member
Nov 7, 2017
70
72
GAWANYIKENI MTAWALIWE KIULAINI
(DIVIDE ET IMPERA)

Tanzania ni nchi nzuri. Wakazi wake huitwa na majirani zao kuwa "AKO NA KISWAHILI MREFU," pia "ADHIBU KWANZA KUJITETEA BAADAYE" mabingwa wa kucheza mpira wa miguu kwa mdomo.
Kisiasa ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi. Hata hivyo tofauti za kivyama zimewagawa wafuasi na kutazamana kama watoto wa nyumba dhidi ya watoto wa kambo. Misuguano baina ya vyama haileti sura ya burudani katika tofauti, bali karaha katika tofauti. Mwenye nguvu si faraja kwa asiye na nguvu bali ni mzigo na mateso kwa aliye dhaifu. na kutambuliwa kwa mnyonge ni pale anapolalamika kwa juhudi na maarifa ili asikike. Hata hivyo uwepo wa vyama vingi ni wa manufaa sana kwa taifa la Tanzania.
Kiuchumi: Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi...watu, mambo ya kale, mbuga za wanyama, ardhi nzuri ya kilimo, madini, gesi, maziwa, mito na bahari. Hata hivyo utajiri wa asili haukuwa na tija kwa taifa. Watu wameendelea kuwa masikini, wanyonge, wenye fikira tegemezi, huku wachache mno kati yao wakiwa na utajiri wa kutisha. Kwa sasa jitihada zimeanza kuzaa matunda. Wizi wa mali kwa maneno ya uwekezaji hasa katika utalii, bandari, ndege, uvuvi, ubinafsishaji wa viwanda na mashamba hasa yaliyokuwa ya umma...mabadiliko yanazaa matunda.A heavy purse makes a mouth to speak. Bila shaka uchumi imara wenye kugusa mwananchi wa kawaida utaondoa unyonge kitaifa na kwa mtu mmoja mmoja.
Kijamii (Elimu, burudani, dini): Watanzania wanapata elimu ambayo inajidhihirisha zaidi katika bahasha za kaki zenye kusheheni vyeti, stashahada, na shahada. Elimu ambayo haina mkakati wa kuandaa ubunifu bali kuwa ombaomba. Mawaziri wa elimu huleta vurugu kwenye mfumo kadiri ya vionjo vyao. Burudani imeingiliwa na siasa, na wasanii wamehamishia sanaa yao katika mapenzi kwani wakiimba nyimbo zenye kuakisi hali ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni....wanaisoma namba.
DINI: Kupitia machache yaliyojiri hivi karibuni kumekuwa na mgawanyiko mkubwa sana. Kipindi cha JK viongozi wa dini waliungana na kuushinda umadhehebu na kutoa miongozo, makaripio na ushauri kwa serikali. sasa hapana. TEC walitoa mwongozo wa Tafakari ya Kwaresma kwa mwaka huu...Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo akaukataa.
Maaskofu wa KKKT wameandika waraka...wamesingiziwa kuwa maandiko yale ni ya CHADEMA na mwandishi ni Mheshimiwa Godbless Lema, Prof Kitila Mkumbo akajitosa kuwakosoa wachungaji wake.
SDA wamejitahidi kufurahia umoja uliokuwepo miaka ya JK na kupinga mgawanyiko uliopo kwa kuipongeza sana serikali iliyopo madarakani.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania haoni haja ya nyraka kwa sasa.
TUNARUDI ENZI ZA WAFALME NA NABII YEREMIA (Manabii wa kweli na manabii wa uongo). Hakuna umoja katika kushauri, kukemea, kukaripia na kuonya.

MWONEKANO WA SERIKALI

Serikali inaonekana kama ina mtindo wa kujihami. haitaki maandamano, mikutano ya hadhara, kukutana na viongozi wa siasa, viongozi wa dini. Jaziba katika hotuba na vitisho vya matumizi ya vyombo vya dola kama jeshi, polisi, mahakama, n.k. Pia wakosoaji wakubwa kutafutiwa kashfa na mitaani watu wana hofu sana, fununu za hapa na pale za watu kuchukuliwa (kutikwa ati kwa sababu waliandika vitu fulani katika mtandao).
Kumbukumbu zinaonesha kuwa 2015 ilikuwa ngumu.Chama tawala kilipata wataka nia 42 kwa ajili ya kiti cha urais. Kulikuwa na makundi mengi...KATA TU...ilisababisha kupatikana kwa JPM kwa namna ya ajabu. hata hivyo kwa jinsi nchi ilivykuwa kipindi hicho na kilio cha watu kutaka mabadiliko...JPM akawa ni mtu pekee ambaye angeleta ushawishi kwa wanachi kukichagua tena chama tawala.
Utendaji wake katika wizara mbalimbali ulimpa kibali kuwa angekuwa rais mwenye tija kwa taifa.
Kampeni za mwaka huo (2015) zilikuwa ngumu kabisa. Kuna muda JPM ilikuwa afanye kampeni bila pesa (wenzake walificha au hawakumtaka kutokana na ahadi alizozitoa na mkakati wake kwa serikali atakayoiunda...mahakama ya mafisadi, kufufua viwanda, elimu bure, kupitia upya mikataba ya madini, kukusanya kodi...na pengine ndani ya upinzani alioupata ndanimo...akajiapiza kukifanyia mapinduzi chama chake.

UPINZANI DHIDI YA SERIKALI HII UNATOKA WAPI?

Mtingo (style)wa uongozi
Vita dhidi ya ufisadi (wahujumu uchumi na wenye kutajirika kinyume na taratibu...hapatoshi).
Namna ya kushughulikia kero ni ya mwendo kasi..kutumbua majipu....wengi wamepoteza kazi.
Vyeti vya kughushi na mitambo inaonekana ni mtandao wa watu wa serikalini tangu zamani...kazi hakuna...na kuna ombwe la watumishi katika kada ya ualimu na afya.
Mtandao kuanzia ngazi ya wakurugenzi wa wilaya hadi taifa kulipana mishahara hewa...na TAMISEMI kuwa na uozo kwa miaka nenda miaka rudi...kuokolewa kwa fedha hiyo.
ACACIA na mtandao wa kutorosha madini kwa miaka 18 bila haya huku WATAALAMU WA NCHI AKA WAZAWA WAKIHUSIKA...aibu ya aina yake...mtandao huo hauwezi kumpenda JPM.
Kujadiliwa kwa miswada kwa hati ya dharura na hivyo kupitishwa mabadiliko dhidi ya mikataba ya hovyo katika sekta ya madini. Wapiga deal wana hasira sana.
Biashara ya dawa za kulewa haikuwa inakomeshwa kwa kuwa wahusika wakuu walikuwa hawaguswi. sasa wameguswa. Chuki dhidi ya serikali.
Huduma katika ofisi za umma ulikuwa wa kimazoea na matumizi mabaya ya fedha ni sehemu ya ujanja. sasa kuna hofu ingawa ushetani umebaki vilevile.
Bila shaka hujuma dhidi ya wanyama mbugani wahusika wakuu walikuwa ni watumishi wa serikali. Kibano hiki kimeleta chuki dhidi ya serikali.
Uvuvi wa holera katika bahari sehemu ya Tanzania...TANZANIA NI SHAMBA LA BIBI. sasa ni kazi.
Nyaraka za viongozi wa dini pia zinachangia kwa namna moja au nyingine serikali kujiona inaandamwa...ATI MALALAMIKO NI MAPATO YA FEDHA ZA KIFISADI HAZIFIKI KANISANI...SADAKA IMEPUNGUA.
Utaratibu wa wa sasa kikatiba ambao uandai sifa ya mtu kuwa diwani, mbunge...ajue kusoma na kuandika badala ya kuweka makazo wa kuwa msomi...baadhi ya wabunge au wapo tu, au wanatumika kuihujumu serikali kwa kutetea masilahi ya matajiri kwa fedha kiduchi wapewayo na mabwana hao...au wasomi wachache katika udiwani na ubunge...wanaelemewa na NDIYO...za wanaojua kusoma na kuandika tu...na hivyo bunge kutokuwa msaada sana katika kuielekeza serikali...na kwa namna ya pekee...SERIKALI INAYOBANA MATUMIZI.
Kichapo kwa maharamia na magaidi waliokuwa katika mapango ya Amboni na Kibiti....waliowaleta wana hasira sana.

MAPENDEKEZO

1. Viongozi wa dini waisome sana serikali hii na waone namna bora ya kutimiza wajibu wao wa kinabii.
2. Wanasiasa washiriki matukio ya kila siku yenye kuhusika na serikali ili kuviziana kufe na pia kupashana pongezi na kero katika mazingira ya furaha.
3. Iwepo falsafa iliyojawa na ubunifu kiasi cha kuwa na vikundi ...IN PRAISE OF THE FOOL...ili kuboresha mahusiano na kukuza demokrasia bila kutokwa na mapovu.
4................
5.................
Asanteni kwa kusoma andiko hilo.
 
Kwa kweli andiko limeandikwa, aliye na macho na ufahamu na asome na kuelewa andiko hili lililoandikwa.
 
Umeandika vitu vya maana sana...point tupu, ila huyu Malaika mkuu na vijakazi wake hawatakuelewa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Baba ubaya sidhani ka ana Akili timamu za kuweza kuelewa maandishi haya maudhui yake
 
  • Thanks
Reactions: BAK
..mtiririko wa hoja ktk makala hii ni wa mashaka-mashaka.

..Padri aliyefuzu hawezi kuandika makala ya hovyo-hovyo namna hii.

..aliyeandika atakuwa ni kijana wa uv-ccm.
 
Back
Top Bottom