Kutoka kwa mimba: Fahamu sababu na Dalili zake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kutoka kwa mimba changa ni nini?

Miscarriage au kutoka kwa mimba changa ni kupoteza ujauzito kabla haujafikia wiki ya 20. Jina la kitaalamu kwa upotevu huu wa ujamzito mchanga ni “Spontaneous abortion” ikimaanisha “upotevu mimba wa ghafla”.

Zaidi ya asilimia 80 ya upotevu mimba changa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Upotevu wa mimba ni vigumu kutokea baada ya wiki 20 za mwanzo za ujauzito kupita. Na kama ikitokea madaktari huita hali hii kama upotevu mimba uliochelewa “Late miscarriage”.

Dalili za upotevu mimba changa

Dalili za “miscarriage” ni pamoja na:

Kutoka kwa damu inayoanza kutoka kidogo kidogo na kuendelea mpaka kuanza kutoka kwa wingi
  • Maumivu makali ya tumbo la kukata (cramps)
  • Maumivu ya tumbo
  • Uchovu
  • Maumivu ya mgongo yanayoongezeka
  • Homa inayoambatana na dalili zozote kati ya hizo hapo juu
  • Kupungua uzito
  • Kutoka uchafu mweupe wenye upinki ukeni
  • Kukaza kwa misuli ya nyonga (contractions)
  • Kutoka kwa vinyama nyama kama damu iliyoganda kutoka ukeni

Dalili dhoofu za ujauzito
Kama una dalili kati ya hizo hapo juu ni vyema kuhudhuria kituo cha afya kwa ushauri Zaidi. Watakuambia kama ni dalili za dharura au kufanyiwa vipimo kuchunguza ujauzito wako kwa ujumla.

Nini husababisha upotevu wa mimba changa kutokea?
Mara kwa mara kutoka kwa mimba changa hutokea pale mtoto anaekua tumboni akiwa na matatizo ya kigenetiki. Matatizo haya hayana uhusiano na mama.

Matatizo mengine yanayoweza kusababisha uwezekano wa kutoka kwa mimba changa ni kama:

Maambukizi
  • Matatizo ya kiafya kwa mama kama ugonjwa wa kisukari au matatizo ya thairoidi
  • Matatizo ya mfumo wa homoni
  • Matatizo katika uitikiaji kinga mwili (Immune response)
  • Matatizo ya kimaumbile kwa mama
  • Matatizo katika umbo la mfuko wa kizazi
  • Uvutaji wa sigara
  • Unywaji wa pombe
  • Matumizi ya madawa ya kulevya
  • Kuwa kwenye uwepo wa ukaribu na mionzi au viambata sumu
  • Mwanamke anakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kupoteza mimba ikiwa changa kama:

Ana umri zaidi ya miaka 35
Ana matatito mengine ya kiafya kama kisukari na matatizo ya kithairoidi
Ameshawahi kupata kupoteza mimba changa mara tatu au zaidi
Udhoofu au kulegea kwa mlango wa mfuko wa uzazi (Cervical Insufficiency)

Kutoka kwa mimba ikiwa changa mara nyingine hutokea pale mama mjamzito anapokuwa na udhoofu au ulegevu wa mlango wa kizazi. Hii inamaanisha mlango wa kizazi hauwezi kuhimili ujauzito kikamilifu na hivyo kufunguka na ujauzito kutoka kabla ya muda wake. Mara nyingi aina hii ya upotevu wa ujamzimto mchanga hutokea katika hatua ya pili ya ujauzito. Huwa kuna dalili chache sana kabla ya upotevu wa aina hii kutokea. Unaweza ukahisi mkandamizo wa ghafla, unaweza ukavunja chupa (maji mengi kutoka ukeni), na nyama nyama pamoja na kondo la nyuma la ujauzito kutoka ukeni bila ya kupata maumivu makali.

Madaktari kwenye nchi zilizoendelea hutibu aina hii ya upotevu mimba changa kwa kushona nyuzi kwenye mlango wa kizazi kwenye ujauzito wako utakaofuata. Hufanya hivi kwenye walau wiki ya 12 ya ujauzito. Nyuzi hizi zitasaidia kuufanya mlango wa kizazi uendelee kufungwa mpaka utakapokaribia kujifungua ndipo nyuzi hizi hutolewa na utajifungua kawaida.

Aina za kutoka kwa mimba changa

Kuna aina mbalimbali za upotevu mimba changa, kama:

Upotevu mimba changa hatarishi. Hii hutokea pale unapokuwa unatokwa na dam una kuna hali ya hatari kwa mama kupoteza ujauzito wake lakini mlango wa kizazi haujafunguka. Katika hali hii kama sababu za kutokwa kwa damu zitatatuliwa basi ujauzito huendelea bila matatizo.

Upotevu mimba changa usioepukika. Hapa mama mjamzito hutokwa na damu na pia anakuwa na maumivu ya tumbo mkazo (crampings), na pia mfuko wa kizazi umefunguka. Uwezekano wa kutoka kwa mimba changa kwenye hali hii ni wa hali ya juu sana.

Upotevu mimba changa usiokamilika. Baadhi ya nyama nyama kutoka kwa mtoto wako na sehemu ya kondo la nyuma na mfuko wa mimba vinatoka nje ya uke na baadhi vinabaki ndani ya uke.

Upotevu mimba changa uliokamilika. Ujauzito wote unatoka nje ya mwili wako. Kila kitu kinatoka, yaani, mtoto, mfuko wa mimba na kondo la nyuma. Aina hii mara nyingi hutokea kabla ya wiki ya 12 ya ujauzito kufika.

Upotevu mimba ulionusurika. Aina hii inahusisha kifo cha kiini cha mimba lakini nyama nyama za ujauzito husika zinabaki kwenye mfuko wa uzazi bila kutoka nje.

Upotevu mimba changa unaojirudia rudia. Aina hii inatambulika pale unapopoteza mimba zaidi ya tau mfululizo ambazo hazikufikia umri wa zaidi ya wiki 12. Aina hii ya upotevu mimba changa hutokea kwa asilimia moja tu (1%) ya wenza wanaojaribu kupata mtoto.

Daktari atatambuaje kwamba una tatizo la upotevu mimba changa?

Kuhakikisha kwamba umepata upotevu mimba changa, daktarin wako atafanya yafuatayo:

Uchunguzi wa mlango wako wa kizazi kuangalia kama umefunguka
Kipimo cha “ultrasound” Hapa atajaribu kuangalia maendeleo yam toto tumboni na kutafuta mapigo ya moyo ya mtoto. Kama itashindikana kupata jibu la moja kwa moja kipimo hiki kinaweza kurudiwa baada ya wiki moja.
Vipimo vya damu.

Hapa daktari ataangalia uwepo wa homoni za ujauzito kwenye damu yako na kulinganisha kiwango cha homoni hizi na vipimo vilivyofanywa huko nyuma. Pia ataangalia wingi wa damu kama umekuwa ukitokwa na damu nyingi ukeni.

Vipimo vya vinyama vinyama vilivyotoka ukeni pia huweza kufanyika kama vilikuwa vinatoka. Hii husaidia kuwa na uhakika kwamba umepata upotevu mimba changa na pia kuweza kutambua kama kuna matatizo mengine yanayosababisha kupatwa na tatizo hili.
Kipimo cha kromosomu (chromosome test). Kipimo hiki kinaweza kufanyika kama wewe na mwenza wako mmepoteza zaidi ya mimba changa mbili mfululizo. Daktari atachunguza kama mfumo wenu wa genetiki ndio unaosababisha upotevu huu.
Matibabu ya upotevu mimba changa

Asilimia 85% ya wanawake wanaopata upotevu mimba changa huenda kupata ujauzito salama na kujifungua salama baadae. Kupata upotevu mimba changa haimaanishi una tatizo la uwezo wa kupata watoto. Kwa upande mwingine, karibia asilimia 1 mpaka 2 ya wanawake hupata upotevu mimba changa unaojirudia rudia. Yani mara tatu au zaidi. Baadhi ya watafiti wanaihusisha hali hii na magonjwa ya ukinzani wa kinga mwili binafsi (autoimmune diseases)

Kama umepata upotevu mimba changa mara mbili mfululizo, ni vyema kuacha kujaribu kupata ujauzito, tumia uzazi wa mpango na wasiliana na mtaalamu wa afya ili waweze kutambua sababu ya upotevu wako wa mimba changa mfululizo.

Kama upotevu wako wa mimba changa ni uliokamilika na mfuko wa uzazi ni mtupu, inawezekana hautahitaji matibabu zaidi.

Wakati mwingine sio tishu zote na nyama nyama hutoka nje ya mfuko wa uzazi. Kama hili litatokea, daktari wako atafanya “Dilation and Curretage”. Haya ni matibabu ambayo itambidi daktarin aupanue mlango wa uzazi na kutoa kila kitu kilichabaki kwenye mfuko wa uzazi kwa umakini. Pia kuna madawa ambayo ukitumia husaidia kutoa tishu zilizobaki kwenye mwili ziweze kutoka nje.

Baada ya utokaji wa damu kuisha unaweza ukaendelea na shughuli zako za kila siku. Kama mlango wako wa uzazi umefunguka lakini ujauzito bado upo salama daktari wako ataweza kufunga mlango wa kizazi kwa kuushona ili kuepusha ujauzito kutoka mpaka pale wakati wa kujifungua utakapofika.

Kama kundi la damu yako ni lile lenye Rh hasi (Rh-), daktari wako anaweza akakupa chembechembe tiba za damu ziitwazo (Rh Immune Globulin). Hizi husaidia kuepusha wewe kutengeneza kinga mwili (antibodies) ambazo zinaweza zikamdhuru mwanao au mimba zijazo.

Unaweza ukafanyiwa vipimo vya damu, vipimo vya genetiki au madawa kama umeshapata upotevu mimba changa mara mbili mfululizo. Kuweza kuhakikisha kwamba una upotevu mimba changa mfululizo (recurrent miscarriages) daktari wako atafanya vipimo vifuatavyo:

“Ultrasound” ya nyonga
Hysterosalpingogram (Hii ni X-ray ya mfuko wa uzazi na mirija ya uzazi kwa pamoja)
Hysteroscopy (Daktari wako atatumia mrija mrefu mwembaba wenye mwanga na kamera kuingia kwenye mfuko wako wa uzazi kuweza kuona kama una matatizo yoyote)
Dalili mbalimbali baaya ya kupata upotevu mimba changa

Kutoka kwa damu na hali ya kujisikia vibaya ni dalili mojawapo baada ya kupata upotevu mimba changa. Kama utakuwa na kutoka kwa damu nyingi ikiambatana na homa, mwili kutetemeka na maumivu makali, hudhuria kitua cha afya haraka kwani hizi ni dalili za maambukizi.

Pamoja na dalili za kimwili unaweza pia ukawa unajihisi kuwa na hisia za huzuni, kujilaumu na pia kuwa na wasiwasi kuhusu mimba zitakazofuata. Unachojisikia ni kawaida na ni vyema kupitia hatua hii ya huzuni kuliko kuipotezea mbali na kuiacha ikusononeshe ndani kwa ndani.

Kama unaweza na hautajali, ni vyema kuliongelea swala hili na watu wako wa karibu kama mwenza wako, rafiki au mwanafamilia uliyemzoea. Vikundi vya wamama waliopoteza mimba kwenye jamii vinaweza kuwa na manufaa makubwa kwako na kwa mwenza wako. Pia muulize daktari wako kama kuna taarifa ua ushauri wa ziada ambao anaweza kukupatia. Kumbuka kila mtu anapona na kuhuzunika na kurudia hali yake ya kawaida tofauti. Hivyo usikate tamaa.

Kupata mimba tena baada ya upotevu wa mimba changa

Unaweza ukapata ujauzito tena baada ya upotevu wa mimba changa. Zaidi ya 85% ya wanawake waliojaribu mara moja baada ya kupoteza mimba changa walipata ujauzito na kuendelea na kuja kujifungua salama. Kuwa na upotevu wa mimba changa haimaanishi kwamba una tatizo kwenye uwezo wako wa kupata mtoto. Hivyo hivyo asilimia 1 mpaka 2 ya wanawake wanaweza wakapata upotevu mimba changa unaojirudia rudia (mara tatu au zaidi).

Kama umepata upotevu mimba changa mara mbili mfululizo, ni vyema kuacha kujaribu kupata ujauzito, tumia uzazi wa mpango na wasiliana na mtaalamu wa afya ili waweze kutambua sababu ya upotevu wako wa mimba changa mfululizo.

Ni wakati gani ujaribu kupata ujauzito tena baada ya kupoteza mimba changa

Ni vyema kufanya mazungumzo haya na daktari wako. Wataalamu wengine wa afya wanasema ni vyema kusubiria kwa muda fulani kabla ya kupata ujauzito mwingine. Muda kati ya mzungumko mmoja wa hedhi mpaka miezi mitatu kabla ya kufikiri kujaribu tena kupata ujauzito. Kuzuia upotevu mwingine wa mimba changa daktari wako anaweza kukupa matibabu kutumia “Progesterone”, homoni inayosaidia kiini mimba kujishika kwenye mfuko wa uzazi na kusaidia maendeleo yake kwenye hatua za mwanzo za ujauzito.

Kuchukua muda kupona kimwili na kiakili ni muhimu pia baada ya kupoteza mimba changa. Ni vyema kutokujilaumu na kujiona mwenye makosa. Hakikisha unapata msaada wa kimawazo na ushauri kujitayarisha na kuwa tayari pale utakapoweza kujaribu tena.

Je, utazuiaje kutokea kwa upotevu mimba changa?

Upotevu mimba changa mara nyingi hutokea kwa sababu kuna tatizo kwenye ujauzito husika. Huwezi kuzuia hili. Kama daktari wako atakupima na kuona tatizo, aina mbalimbali za matibabu zinapatikana.

Kama una ugonjwa, kuutibu ugonjwa husika kutaongeza uwezekano wa kupata ujauzito ulio salama na kujifungua bila matatizo. Njia bora unayoweza kuchukua mwenyewe ni kuhakikisha unakuwa mwenye afya kadiri uwezavyo kabla ya kujaribu kupata ujauzito:

Fanya mazoezi ya mara kwa mara
Kula mlo kamili na wenye afya
Zingatia kuwa kwenye uzito wako kiafya. Epuka maambukizi
Usivute, kunywa pombe au kutumia madawa ya kulevya
Punguza utumiaji mkubwa wa “caffeine” kama kahawa.
 
Back
Top Bottom