Kutoka kucheza Ligi ya NBA mpaka kuja kucheza ligi ya mkoa wa Dar (RBA) Kuna La Kujifunza Kwenye Maisha Ya Hashim Thabit

MIJITU INAANZISHA UZI KUJADILI WATU

Mbona anacheza Ligi bongo katoka NBA.

Mamaee, ulitaka akifika bongo aanze kutumbua maishaa. Awe na maisha ya ANASA ,achangamane na Chawa....ndo mseme Jamaa katoboa???

Huyo ni mchezaji, mwili wake keshauzoea mazoezi

Angecheza nn ??? Akacheze mpira wa miguuu ili hali yeye nimchezaji wa basketiboli?

Kwahiyo Samata akiamua kutundika daluga la kimataifa, akirudi bongo, akae kwake?

SASA MNIAMBIE.... KATI YENU NYINYI... NA HASHIMU NA SAMATA... NANI ANAMAISHA MAKUBWA KUZIDI MWINGINE?

Kamtu kamekaaa kitandani kwa Baba yake. Hakajapiga hata mswaki, chai kanipikiwa kwao, kameamka kameshika simu, kameingia mtandaoni

Kanafungua Uzi..Hashimu kafuliaaa..... Kafulia ya nyoko?

Samata namuonea hurumaa.... Huruma ya nyoko?

KWEMDENI HUKO, MIJINAFIKI NYINYI
Umemkamataa uyo mtot wa kike
 
Aya nijibu haya maswali

anacheza ligibya Bongo kwa sababu Kiwango kimeshuka??

anacheza bongo kwa sababu amefulia mpaka uchumi ivo anaamua kucheza kupata shilingi?

Kaja kucheza ili kusaidia Ligi ya bongo kukua kukua kwa mapenzi yake?

Karudi nyumban, akiwa na mipango yake, baada ya kuona keshavuna mapesa mengi, lkn kwakua umri wake na mwili wake aliuzoesha mazoezi, kaona ajichanganye na wana?

Je Samata siku akirudi bongo, akatua Simba atakua kafulia kimpira au kichumu au vyote kwa pamoja?

Je Kiwango cha samata kikiwa hakimruhusu tena kucheza kimataifa, atatakiwa kubaki amekaaa tu home kuendesha shuguli zake?

Je samata na pesa zake, akiona aje tu bongo na kwasababu ni mtu wa mpira, akiona ajitolee kukipiga BIASHARA U bila malipo ni shida?

KILA KITU KINA MUDA NA WAKATI WAKE JOOO.
Acha wivu Dada
 
Nakumbuka miaka ya 2008-2009 Hashim Thabit Akiwa bado ana umri mdogo, alionekana kitaifa baada ya kufikisha wastani wa alama 13.6 na alama 10.8 ya mipira ya kurudisha.

Alianza kujikita zaidi kwenye mchezo huo triple-double akilipocheza dhidi ya Providence College tarehe 31 Januari Mwaka 2009 akipata alama 15 na 11 mipira ya kurudisha na kuzuia mara 10 Alizuia mara 152 msimu mzima.

Hashim Alitajwa kuwa mchezaji bora wa kuzuia ya wakubwa Big East Player of the Year with Pitts DeJuan Blair.

Hashim alitajwa kuwa mchezaji wa timu ya pili kitaifa ya mchezaji bora wa kuzuia kitaifa. Hashim alipita alama 1000 dhidi ya Purdue alikuwa mcheza wa tatu wa UConn kufikia rekodi kwenye msimu huo Jerome Dyson na A. J. Price ndio wachezaji wengine walioweza kufikia hiyo rekodi.

Hashim aliisaidia timu yake ya UConn kwa mara ya kwanza kufika kwenye finali za t Final Four mwaka 2004 Akiwa mwaka wake wa mwisho chuo.

Nakumbuka Hashim alichaguliwa na chama kinachosimamia ligi ya mpira wa kikapu kitaifa cha NBA kama mmoja ya wa chezaji wanaoruhusiwa kuchezea ligi hiyo

Hasheem alichezea timu ya chuo cha UConn kabla ya kuchaguliwa kama chaguo la pili mwaka 2009 katika timu ya Memphis Grizzlies. Kuna la Kujifunza Sana Kwenye Maisha ya Basketball ya HT.

Hasheem amecheza NBA katika timu kama za Memphis Grizzlies, Houston Rockets, Portland Trail Blazers, Oklahoma City Thunder na Grand Rapids Drive kabla ya 2017 kujiunga na Yokohama B-Corsairs ya nchini Japan.

Lakini Leo Hii aliotoka nao UConn bado Wako NBA.

By the way kupanga ni kuchagua wakuu.

View attachment 1956744
Ameamua kufanya program ya kuukuza mchezo huo kwa vijana wa Bongo ili wapate shavu majuu.

Mnasagia sana kunguni loh
 
Dah,sema bahati mbaya tu sijui dogo why kapotea mapema sana
Alivyokamata channel ya NBA top players akawa hafikii viwango sababu ya mazoezi hafifu. Alikuwa hajifui vya kutosha so progress ikawa ina drop ikabidi wamteme tu. Sema hela alizipata kwa kipindi chake.
 
Back
Top Bottom