Kutoka kijiweni: Wanaume muwe mnaangalia na kesi za kushtaki na nani unamshtakia, vitu vingine aibu

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
69,748
136,849
Good morning,

Kushare yanayokusibu moyoni si vibaya make inakupa ahueni na faraja pia sometimes, ila nani unaemwambia na unamwambia nini ni swala lingine tena.

Jana hiyo kijiweni, mke wa mtu anamwaga mchele yeye na mme wake wakizinguana, mme nduki hadi kwa dada zake kushtaki ni muda mrefu amekua akifanya hivo mke anamueleza kistaarabu kabisa asali wake kuwa ugomvi wao waumalize wenyewe au kama anaona anahitaji kushare na mtu atleast amshirikishe mtu mzima mwenye busara zake atapata ushauri, japo mme nae full makolokocho kufumaniwa kila siku ya kalenda anapiga hadi beki tatu ndani ila mke huwa hasimulii anakufa na tai shingoni, mme ndio ana kazi ya kukimbilia kwa dada zake (mawifi kushtaki) huko ni kupandikiza chuki na ndugu upande wa mme make mawifi nao vidomo hadi ma mkwe yanamfikia, mme hasikii wala haelewi hadi anahisi mme wake kile alichonacho sio kichwa ni nazi.

Kilichomkera kuliko yote siku za hivi karibuni kuna ex wake alimtext, mwenyewe anadai hawana kabisa uhusiano ila ndo hiyo jamaa mara chache chache anatuma msg, basi mme kakuta hizo msg kwenye simu ya mkewe wakaongea akaomba msamaha akajua yameisha kumbe habari zishawafikia mawifi, mme kaenda kushtaki.

Nilibaki nashangaa kama fala, najiuliza how come mme akawasimulie dada zake ugomvi kama huo ni ujinga au utaahira, serious? Kuna wanaume kweli vichwa panzi huku kujilizaliza kwenu mnajiliza hadi kupitiliza yani dada ndio wakukimbilia kuwaambia matatizo ya ndoa yako? Ovyoovyo sana.

PANIC AT YOUR OWN RISK!
 
huyo mwanamke hujaona kama na yeye hana akili?

Kwa nini amwage mambo ya mumewe kijiweni?

Halafu unamuona huyo mwanamke yuko sawa kweli? Anaona eti kuwasiliana na Ex ni sawa tuuuuuuu

Ujinga wa hali ya juu

Huo hafai kuwa mke anafaa kuwa kahaba

I cant comment about a man ...kwa sababu wewe mwenyewe mleta mada hauko objective...Umebase kwa huyo mwanamke na kumuona as if yuko sahihi.....
 
Nilibaki nashangaa kama fala, najiuliza how come mme akawasimulie dada zake ugomvi kama huo ni ujinga au utaahira, serious??? Kuna wanaume kweli vichwa panzi huku kujiliza liza kwenu mnajiliza hadi kupitiliza yani dada ndio wakukimbilia kuwaambia matatizo ya ndoa yako??? Ovyoooo ovyo sana

PANIC AT YOUR OWN RISK!!!

Halafu mpendwa toka nauli zimefutwa unajidai!
 
Kwanini umejenolaizi wanaume wote wakati mmeo ndio ana matatizo hayo halafu ujue mtu hupeleka matatizo yake sehemu anayoona atapata msaada.
 
huyo mwanamke hujaona kama na yeye hana akili?

Kwa nini amwage mambo ya mumewe kijiweni?

Halafu unamuona huyo mwanamke yuko sawa kweli? Anaona eti kuwasiliana na Ex ni sawa tuuuuuuu

Ujinga wa hali ya juu

Huo hafai kuwa mke anafaa kuwa kahaba

I cant comment about a man ...kwa sababu wewe mwenyewe mleta mada hauko objective...Umebase kwa huyo mwanamke na kumuona as if yuko sahihi.....
mkuu hili ni tatizo.. Na hiki husababishwa na sisi wanaume kuoa makahaba.. Kumbe kijiweni kuyamwaga ni sahihi lakini kuwaambia ndugu ni ujinga? Sikuwahi kuwaza
 
They deserve each other, lakini kwa kufikiri haraka tu, mke kwanza anakaa kijiweni (what the heck), na kusimulia upuuzi wa chumbani kwa wakazi wa kijiweni...wewe mleta mada umemuweka mtu wa namna hiyo kwenye kundi gani?
 
Mpendwa wacha hizi mambo. Achilia mbali jamaa kuwashirikisha ndugu zake wa karibu katika mambo yanayoihusu familia yake, ila pia anaowashirikisha ni wanawake. Pengine anahitaji mtazamo wa kike, ili kujaribu kumuelewa mkewe.

Ila sasa mwanamama yeye kaleta kwenye hadhira isiyowahusu. Unaamini vipi tuhuma anazotoa mwanamke anayemdharau mumewe mbele za watu? Bibie kasema mumewe hana kichwa, bali nazi. You just can't be this biased bana, c'mon!
 
Back
Top Bottom