Kutoka katika Vituo vya Mabasi ya Mikoani, hatimaye Siri za Abiria wa Kiume zafichuka rasmi!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ni kwamba katika hali isiyo ya kawaida kama si ya kushangaza imegundulika kuwa 99% ya Wanaume ambao husafiri na Mabasi ya Mikoani huwalazimisha Makondakta au Mawakala wa yale Mabasi wawapangie siti moja na Wanawake na kwamba kuna wengine hudiriki hadi ' kuwanyang'anya ' wale Wakata ' tiketi ' vile vitabu na kuanza kukagua kwa macho ya ' kutukuka ' kabisa majina ya jinsia ya Kike na kama wakikutana nalo halafu siti inayofuata ipo wazi ' hung'ang'ania ' wakatiwe hiyo.

Kama hii haitoshi inasemekana kwamba wapo Wanaume wengine ambao wakishajua tu kuwa Kesho wanataka kusafiri kwenda Mkoani huwapigia mapema Simu wakatisha tiketi katika Vituo vikubwa vya Mabasi na kuwaambia wawaangalizie siti ambazo zinakaliwa na Wanawake na kama ikitokea Mtu wa pili ni Mwanaume basi hao Watu ( Wanaume wakware ) wapo radhi hata kuwahonga hao wakatisha tiketi Pesa yoyote ile ili tu wao waweze kukaa karibu na hao abiria wa Kike kisha wamalize ' mchezo ' wa ' kutongoza ' na ' kuwabandua '.

Ifuatayo ni moja tu ya nukuu ya maneno ya abiria mmoja leo katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo akiwa anazungumza na mkatisha tiketi na naiweka hapa kama ' Mnakunaku ' Mimi nilivyoisikia ' mubashara ' kabisa.

Abiria : Oya Kaka mambo niaje?
Mkatisha Tiketi : Poa tu Kamanda vipi unasafiri nini?

Abiria : Sasa kama sifasiri unadhani hapa nimefuata nini?
Mkatisha Tiketi : Acha zako hizo Kaka!

Abiria : Niambie Kesho nataka kutinga Mkoa kidogo vipi kuna siti?
Mkatisha Tiketi : Ndiyo zipo kama nane ( 8 ) hivi nikukatie Kaka?

Abiria : Kwanza kabla ya kunikatia hebu niambie hao nane wote ni Mimi au Wao?
Mkatisha Tiketi : Sijakuelewa hapo Kaka.

Abiria : Hivi mbona Wewe unakuwa mshamba hivi? Namaanisha wote hao nane ni Wanaume wenzangu au ni Wanawake?
Mkatisha Tiketi : Kumbe ni hivi sasa si ungenyoosha tu maneno Kaka tumalizane?

Abiria : Haya niambie.
Mkatisha Tiketi : Kati ya hao nane abiria saba ni Wanaume tena Wazee na ile moja ni ya Mwanamke lakini ni Bibi hivi nadhani anarudi Kijijini je nikukatie ipi Kaka?

Abiria : Kwahiyo unataka unikalishe Mimi na Wazee hao pamoja na huyo Bibi unadhani nitaongea nao nini kwa mfano?
Mkatisha Tiketi : Kwani na Wao siyo Watu Kaka?

Abiria : Watu lakini wameshakuwa magari ya mkaa sasa ( akimaanisha Wazee ) hivyo hata nikikaa nao hakutakuwa na jipya sana sana watanilalia tu na kunitemea miudenda yao halafu nikifika ninakoenda nitakuwa nanuka tu.
Mkatisha Tiketi : Acha dharau Wewe Kaka na Watanzania hatuishi hivi kwa kubaguana.

Abiria : Utajiju! Hebu niambie hakuna siti ambayo imekaliwa na Demu wa nguvu?
Mkatisha Tiketi : Ipo tena Demu mwenyewe huyo hapo anakuja si unamwona alivyonona Kaka?

Abiria : Mama yangu! Ebhana fanya kila uwezalo nikae nae siti moja na hata ikiwezekana nikupe Hela umtoe anayekaa nae karibu nipo tayari.
Mkatisha Tiketi : Sawa Mimi nakufanyia hivyo ila nitoe kabisa na changu kisha namuhamisha yule abiria na unakaa nae Wewe kisha utamalizana nae mbele kwa mbele.

Abiria : Safi sana Mimi napenda Watu wajanja kama Wewe hivyo kamata hii Tsh 30,000/ yako halafu nifanyie mambo. Dunia hii ya leo huwezi ukawa tu na Mkeo nyumbani halafu kama hivi unasafiri usitafute Kipoozeo cha huko uendako na huyu naenda kumbandulia Singida halafu Mke wangu ikifika tu usiku nitamdanganya Basi limepata hitilafu hivyo tunalala ili kuepukana na Majangili njiani kisha Mimi nitaenda nae Lodge huyu Demu hadi Kesho kutwa ndipo tutatimba maguu Town Shycom. Halafu Kijana namba yangu ya Simu huna hebu ichukue yangu ili hata siku zingine nikikupigia tu kukuambia nataka kusafiri Wewe kabla ya kuniambia kama kuna siti kwanza angalia kama kuna siti yoyote amekata Demu mkali kisha ndiyo unijibu ipo kisha utanikatia sawa? Mwenyezi Mungu ametuumbia sisi hawa Viumbe hivyo tutawabandua tu na hakuna namna.
Mkatisha Tiketi : Poa tiketi yako hii hapa sasa Wewe tulia hapa chini kwanza Mimi nipande katika Basi nikajifanye kumkomalia Yule Jamaa kuwa Tiketi yake aliikata Kimakosa na kwamba kumbe hatakiwi kukaa pale na akisimama tu nampeleka zile siti za nyuma ili akarushwe rushwe hadi akome na akifika huko Kwao awe ameshafanyishwa mazoezi ya kutosha ya kukomazwa safarini.

Mambo yaliishia hapo na ' Mnakunaku ' Mimi nikasepa zangu na kugundua kuwa kumbe ukipanda haya Mabasi na kukuta abiria mwenzako wa Kiume anakununia na hakupi ushirikiano wa Kiabiria basi jua tu ya kwamba hakufurahishwa Wewe kukaa nae karibu hapo kwakuwa wote ni Team Mikuyenge na Yeye alitamani Mbunye iwe jirani yake.

Sasa nautupa Kwenu abiria wa Kiume je hili jambo ni la Kweli? Na je nyie Dada zetu humu ambao huwa mnasafiri kwenda Mikoani je huwa mnakutana na hii kadhia kutoka kwa Wanaume kwa kutongozwa muwapo safarini na mmekaa siti moja?

Nawasilisha na karibuni katika ' utiririkaji '.
 
Mkuu umeandika ukweli ila kinyume chake ndio sana.
Kuna stand moja Makonda ndio wanawahamasisha abiria wa kiume kukaa siti moja na wadada kama ushawishi wa kupanda hilo basi.
Imewahi kunitokea "nakupa hii siti ukae na mtoto Mkali" na ndivyo ilivyokuwa. Kwa heshima ya kiapo na mkataba wa family nikabaki Bila madhara hadi nilipofika.
 
bonge la reject hilo la SAUT Mwanza
 
Niliwahi kuangalia kwa majina mazuri. Nimeenda kukata tiketi nikakuta Mary Johnson, nikamuambia mkata tiketi nikatie hapa.

Kesho nakuja nakaa na bibi. Daah!. Niliboeka sana lakini mimi alikuwa born town, mjanja kinoma. Basi wala hata sifikiriagi tena haya madude.
 
Mkuu umeandika ukweli ila kinyume chake ndio sana.
Kuna stand moja Makonda ndio wanawahamasisha abiria wa kiume kukaa siti moja na wadada kama ushawishi wa kupanda hilo basi.
Imewahi kunitokea "nakupa hii siti ukae na mtoto Mkali" na ndivyo ilivyokuwa. Kwa heshima ya kiapo na mkataba wa family nikabaki Bila madhara hadi nilipofika.

Na ndiyo maana nikaamua leo niuvae ' Unakunaku ' wangu ili niende pale Ubungo Terminal nikafanye huu ' utafiti ' wangu mdogo na bahati nzuri kumbe hata Wewe Mkuu umeshawahi kukumbana nao ' mubashara ' safi sana!

Cc: Joseverest
 
Niliwahi kuangalia kwa majina mazuri. Nimeenda kukata tiketi nikakuta Mary Johnson, nikamuambia mkata tiketi nikatie hapa.

Kesho nakuja nakaa na bibi. Daah!. Niliboeka sana lakini mimi alikuwa born town, mjanja kinoma. Basi wala hata sifikiriagi tena haya madude.

Kwahiyo kumbe pamoja na ' ujanja ' wote huo bado tu ulilishwa ' tango pori ' Mkuu?
 
Hata hao madem pia uona raha kukaa seat moja na lidume, tena wana tabia chafu mara uingiapo uanza kukujangamkia mpk hata waliipo jirani seat yenu udhani ni mtu na mtu wake. Tahadhari si wote unaokutana nao ni watu wema,utagharamikia gharama zote njia km kula na kadhalika lakin ikawa,ni hasara kwako tu,TUJITAMBUE
 
hiyo tabia ya kuangalia jina la kike kuna siku iliniponza, nilienda scandnavia kukata tiketi ya kampala nikaomba ile chati niangalie nikaona jina la kike nakamwambia nipe hii, sasa nimefika pale ubungo naingia kwenye basi nakuta jirani yangu amekaa mama mtu mzima very serious nukajua nimejichanganya, hapo mfukoni nina chupa yangu ya konyagi, safari imeanza mama akatoa biblia akawa anasoma, kufika pale mombo nikaamua nianze kula konyagi niliporudi ndani ya gari yule mama kusikia harufu ya pombe alianza kunipa risala njia nzima, nilipofika arusha nikaamua kuhama siti, uzuri wa safari ya k'la mnalala njiani basi ile baridi ya eldoret na kisumu ni full kubambia!
 
Back
Top Bottom