Kutoka JNICC Dar, Nafasi ya Vyombo vya habari katika kueneza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
865
427
Wakuu,

Wadau wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, kuanzia jana walikuwa wanafanya mkutano wa namna vyombo vya habari vinavyoweza kushiriki kueneza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Octoba 25, 2015.

====================

Anayeongea sasa ni
Dr. Gideon Shoo: Anasema vyama vya Siasa vikubwa hapa nchini vinafanana hivyo kunakosekana maadili ya Uongozi.

Anasema mwaka 1992 Tanzania ilipotea njia anakumbushia kifo cha Azimio la Arusha, likazaliwa kwa Azimio la Zanzibar na kupotea kwa maadili anawatolea mfano kuwa 'tunao akina Mtikila wengi hapa nchini, watu waliojaa siasa za chuki'.

-Mimi nasoma kwenye Social Media, kuna wakati hadi nashtuka kwa chuki zinazojengwa dhidi ya watu mbalimbali nchini.

-Social Media inaweza kupelekea kuibuka kwa Violence, ipo mijini kwa wingi na vurugu huanzia mijini kuliko vijijini.7

-Maneno ya kwenye Social Media yanasambaa haraka na yanaaminiwa na vijana wetu

-Mwaka huu vijana waliozaliwa 1997 watapiga kura; hawa 'Role Models' wao ni viongozi wezi, wakwapuaji, Mafisadi

-Hatuna ajira nchini sababu ya kukosekana Maadili ya Uongozi. Ni lazima turejeshe mfumo ambao utarejesha Maadili ya Uongozi

Sheikh Juma Mbuguzi: Inasikitisha, kwa sasa watu wamefikia hatua wanawaamini wanasiasa zaidi ya viongozi wao wa dini.

-New World Order imetufikisha hapa; Tanzania tunawezaje kurudi kwenye misingi yetu kama Taifa katika hali hii?

Dr. Shoo: New World Order haikulazimishi kukubali ndoa za jinsia moja; ni utashi wa kiongozi wenu aliye madarakani

-Mzee Mwinyi alilaghaiwa mwaka 1992 na wanaong'ang'ania kutuongoza sasa ambao utajiri wao hauna maelezo.

Mdau: Rasimu ya II ya Katiba Mpya ilikuwa inarejesha Miiko na Maadili ya Uongozi; tusisitize Katiba ipatikane ikiwa na hili.

Wakiliki wa Vyombo vya habari: Tanzania ni nchi kama nchi nyingine, ni jukumu letu sote kuilinda na kutunza amani.

- Wanasiasa, Viongozi na Vyanzo vingine vya Habari viwe na Ucha Mungu na kuzingania utunzaji amani.

-Vyombo vya Habari vizingatie Maadili/Miiko ya Kazi katika kufikisha ujumbe kutunza Amani na Umoja wa Kitaifa

Dr. Reginald Mengi: Viongozi wa Dini onyesheni umoja wenu sasa, Matamko yakitoka yasimame kwa umoja kuhimiza Umoja na Amani

-Tuna wajibu wa kufanya yaliyo mema kuhakikisha Tanzania haiwi na machafuko kabla na baada ya Uchaguzi
 
Ni jukumu letu sote kwa maana ya serikali, vyama vya siasa, wanaharakati, wananchi, vyombo vyote vya ulinzi, waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje na wadau wote. Kwa hiyo tusiwaachie wadau wa habari peke yao.
 
Back
Top Bottom