Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 588
- 1,698
Habari wanajamvi,
Kama tujuavyo siku ya Jumamosi, Rais John Magufuli alifanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri akiwahamisha baadhi, wengine wakiondoka na wapya wakikanyaga barazani. Leo ambao watapenda kushika nafasi walizotajwa wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam. Kuwa nami nikujuze yatakayojiri Ikulu.
=======
Shughuli imeanza kwa kuimba wimbo wa Taifa, waziri wa madini, Angellah Kairuki anaanza kwa kula kiapo cha kutumikia wizara yake mpya baada ya kutolewa Utumishi. Aliemfatia ni Charles Tizeba ameapa kuwa waziri wa Kilimo baada ya wizara yake kugawanywa.
Kwa sasa anaapa Kapteni Mkuchika kuwa waziri wa Utumishi akirithi mikoba ya Angellah Kairuki.
Mawaziri na Manaibu waziri wanaendelea kuapa akiwemo Dkt. Faustine Ndugulile, Kangi Lugola na Subira Mgaru. Pia ameapa naibu waziri wa habari, sanaa utamaduni na michezo, Juliana Shonza pia katibu wa bunge, Stephen Kigaigai.
Jaji Mkuu: Nawapongeeza na kuwatakia kila laheri katka kuitumikia nchi yetu, kwa upande wa mahakama tunawaomba mfate taratibu na kanuni na hakutakuwa na mgongano.