Kutoka Ikulu: Rais Magufuli awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri kutokana na mabadiliko ya Baraza

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
564
1,000
Habari wanajamvi,

Kama tujuavyo siku ya Jumamosi, Rais John Magufuli alifanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri akiwahamisha baadhi, wengine wakiondoka na wapya wakikanyaga barazani. Leo ambao watapenda kushika nafasi walizotajwa wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam. Kuwa nami nikujuze yatakayojiri Ikulu.


=======

Shughuli imeanza kwa kuimba wimbo wa Taifa, waziri wa madini, Angellah Kairuki anaanza kwa kula kiapo cha kutumikia wizara yake mpya baada ya kutolewa Utumishi. Aliemfatia ni Charles Tizeba ameapa kuwa waziri wa Kilimo baada ya wizara yake kugawanywa.

Kwa sasa anaapa Kapteni Mkuchika kuwa waziri wa Utumishi akirithi mikoba ya Angellah Kairuki.

Mawaziri na Manaibu waziri wanaendelea kuapa akiwemo Dkt. Faustine Ndugulile, Kangi Lugola na Subira Mgaru. Pia ameapa naibu waziri wa habari, sanaa utamaduni na michezo, Juliana Shonza pia katibu wa bunge, Stephen Kigaigai.

Jaji Mkuu: Nawapongeeza na kuwatakia kila laheri katka kuitumikia nchi yetu, kwa upande wa mahakama tunawaomba mfate taratibu na kanuni na hakutakuwa na mgongano.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,975
2,000
sidhani nchi yetu inahitaji serikali kubwa kama tuliyokuwa nayo,elewa hii inatugharimu sisi walipa kodi ,hili sio jambo la kufurahia,wananchi wanahitaji huduma sio kubadilishiwa baraza kila kukicha,kuna nchi hapahapa SADC mabadiliko hawa ni ya nadra sana maana wanaelewa cost zinazokuja nazo na mabadiliko haya,nitafurahi nikiamka asubuhi our no 1anatangaza wizara 15 tu ambazo ndizo tunazohitaji.
 

Obuma

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
2,731
2,000
Tunachapa kazi hayo mengine yanakuhusu wewe. Tuliambiwa Bunge live linazui watu kufanya kazi na mimi nasema hizi sherehe live zinazuia watu kuchapa kazi kwa hiyo wao wamalizane wenyewe na sisi tuendelee na kazi zetu.
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,785
2,000
Habari wanajamvi,

Kama tujuavyo siku ya Jumamosi, Rais John Magufuli alifanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri akiwahamisha baadhi, wengine wakiondoka na wapya wakikanyaga barazani. Leo ambao watapenda kushika nafasi walizotajwa wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam. Kuwa nami nikujuze yatakayojiri Ikulu.
=======
Saa ngapi??
 

Nathan Jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
1,435
2,000
Si Baraza jipya, ni watu wapya ndani ya Baraza ambao hawataleta mabadiriko yeyote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom