Kutoka Fursa Sawa kwa Wote hadi WAMA na baada ya hapo nini kitafuata? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka Fursa Sawa kwa Wote hadi WAMA na baada ya hapo nini kitafuata?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shadow, Mar 18, 2010.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nimejaribu kufuatilia hizi NGOs zinazoanzishwa hapo Ikulu baada ya utawala mpya kuingia madarakani. Hapo mwanzo nilijua ya kwama 'Fursa sawa kwa wote" ni mali ya watanzania chini ya usimamizi wa mama wa kwanza wa Wakati huo [Mama Anna Mkapa] lakini baada ya yeye na mumwe kuondoka hapo Magogoni akaibeba na kwenda nayo mtaani ingawa sasa hivi inachechemea kuanzia kwenye utendaji hadi kwenye 'media coverage'.
  Hilo alikuishia hapo, kwani mabadiliko ya kiutawala, mama Salma Kikwete naye kwa kupitia Ikulu akaja na kitu kinaitwa Wanawake na Maendeleo. Kwa mtizamo wa juu juu inaonekana hili wazo la kuanzisha hii NGO ni zuri. Inamaanisha hizi NGO zinakuwa makini kwa kipindi cha miaka kati ya 5-10 kulingana na kama mume mtu yaani rais anakuwa madarakani kwa kipindi gani. Baada ya kusema hayo, basi ipo budi kuwa na official duties ambazo zitabainisha kwa uwazi majukumu ya mke /mme wa rais atakapoingia madarakani kwa manufaa ya umma. Mengi ya haya majukumu yawe zaidi katika kusaidia jamii za kitanzania.
  Hii itasaidia kuondoa mlolongo au 'chain' za haya ma NGO yanayozaliwa kila baada ya Rais mpya kuingia madarakani na kuondoa mashaka kwenye macho ya watanzania kwamba hiz NGOs za magogoni zinatumika ndivyo sivyo.
  My take: mama wa kwanza anzisheni NGOs baada ya kutoka Ikulu ; Serikali tengeni majukumu ya mama wa kwanza, apewe ofisi na wafanyakazi ambao ni civil servant. Hii itasaidia 'continuity' katika shughuli hizi za kinamama /baba wa kwanza.
  Tuhifunza kutoka kwa wenzietu: Bofya hapa:http://letsmove.gov/ na hapa:http://www.whitehouse.gov/administration/first-lady-michelle-obama
   
Loading...