Kutoka "elimu elimu elimu" mpaka "ajira ajira ajira"

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,552
44,708
Ajenda kuu mwaka huu iwe ni suala la ajira watanzania tujiulize nani ana sera nzuri za kuwapa watoto wa wenye Nchi ajira ili nao wafike mahali pazuri kama ambavyo na wenyewe walipata ajira wakafikia hizo nafasi kubwa kubwa.

Tuache Kwanza habari za nyongeza ya mshahara kwa watumishi tujue inakuaje kuaje vijana wanazidi kumaliza chuo kilio kikiwa ni ajira ili waache kuwa wategemezi.
 
kuna wakati nilisoma kwenye shirika letu la takwimu waliandika ajira rasmi ni asilimia 8 tu ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini maana yake 92% ya wabongo wako ajira isiyo rasmi ambayo kwasasa imekumbwa na msukosuko , ukata na kupoteza ajira za mamilioni ya watu nchini kwa sababu zifuatazo

1. miundombinu mikubwa ya nchi kama SGR na Stieglers imezoa pesa iliyokuwepo kwenye mzunguko na kuipeleka nje ya nchi kupitia kuwalipa makandarasi wa nje japo angalau vibarua wanalipwa

2. ununuzi wa ndege nyingi umeondoa pesa nyingi kwenye mzunguko kwa mkupuo

3.mikakati ya kuua NGOs kwa kuzifunga ovyo nchi imepoteza fedha nyingi za wazungu na watu wengi kupoteza ajira

4.Kodi kubwa za biashara zinazoua mitaji ya wafanyabiashara ambao wengi wamerudi kwenye umaskini na kushindwa kukuza mitaji ambapo wangeweza kuajiri zaidi

5.Masharti magumu ya mikopo taasisi za fedha watu maskini hawana dhamana

6. Gharama kubwa ya mawasiliano ya simu na internet , bei ya umeme na petroleum zinapunguza faida za biashara na kukata mitaji ya biashara

7.Elimu duni zinazofundishwa mashuleni kwa kutumia ideology ya kipumbavu ya ujamaa inayofanya wananchi kushindwa kufaidika na globalization kwa kuwa wajinga washamba na kushindwa kuongea English na hivyo kukosa masoko na mitaji ya nje

8. matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa kwa wapinzani yamekimbiza wafadhili na wawekezaji wanaoamini kwenye human rights

9. kukua kwa deni la taifa nilisikia Mkulu akisema kila mwezi nchi inalipa madeni billion 700!ina maana nchi inaondoa pesa nyingi kwenye mzunguko kila mwezi. Pia hii ina maana sirikali hupeleka bajeti ndogo isiyozidi hata 50% kwenye serikali za mitaa tunapoishi!

10. watanzania wengi ni wavivu na matapeli wanaochagua kazi za kufanya hasa wenye elimu ya juu kidogo!!

11.mfumo mbaya wa elimu unaoandaa watu kufanya kazi za ofisi badala ya kujiajiri, wahitimu hutafuta kazi miaka hata mitano ndipo hushtuka na kujiajiri!

12. kukosekana utashi wa serikali kuanzisha masomo ya ujasiriamali kuanzia chekechea wakati serikali inajua haina ajira za kuwapa wahitimu!

13. sirikali kushindwa kuwa na political will na mikakati ya kuondoa tatizo la ajira! akili yote iko kwenye miundombinu tu!!

14. wananchi kushindwa kupaza sauti kuwa wanakufa na njaa kwa ukosefu wa ajira kwakuwa wanaogopa kukamatwa, kupotezwa, kufungwa jela , marungu na mabuti ya FFU!

15. raia wengi kukosa elimu ya uraia na hivyo kushindwa kutumia sanduku la kura kujitetea!!
 
Sio waache kuwa tegemezi wapate elimu ya kujua hakuna kiongozi atakae watilia pesa mfukoni na kuwapelekea vibaba majumbani!
 
kuna wakati nilisoma kwenye shirika letu la takwimu waliandika ajira rasmi ni asilimia 8 tu ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini maana yake 92% ya wabongo wako ajira isiyo rasmi ambayo kwasasa imekumbwa na msukosuko , ukata na kupoteza ajira za mamilioni ya watu nchini kwa sababu zifuatazo

1. miundombinu mikubwa ya nchi kama SGR na Stieglers imezoa pesa iliyokuwepo kwenye mzunguko na kuipeleka nje ya nchi kupitia kuwalipa makandarasi wa nje japo angalau vibarua wanalipwa

2. ununuzi wa ndege nyingi umeondoa pesa nyingi kwenye mzunguko kwa mkupuo

3.mikakati ya kuua NGOs kwa kuzifunga ovyo nchi imepoteza fedha nyingi za wazungu na watu wengi kupoteza ajira

4.Kodi kubwa za biashara zinazoua mitaji ya wafanyabiashara ambao wengi wamerudi kwenye umaskini na kushindwa kukuza mitaji ambapo wangeweza kuajiri zaidi

5.Masharti magumu ya mikopo taasisi za fedha watu maskini hawana dhamana

6. Gharama kubwa ya mawasiliano ya simu na internet , bei ya umeme na petroleum zinapunguza faida za biashara na kukata mitaji ya biashara

7.Elimu duni zinazofundishwa mashuleni kwa kutumia ideology ya kipumbavu ya ujamaa inayofanya wananchi kushindwa kufaidika na globalization kwa kuwa wajinga washamba na kushindwa kuongea English na hivyo kukosa masoko na mitaji ya nje

8. matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa kwa wapinzani yamekimbiza wafadhili na wawekezaji wanaoamini kwenye human rights

9. kukua kwa deni la taifa nilisikia Mkulu akisema kila mwezi nchi inalipa madeni billion 700!ina maana nchi inaondoa pesa nyingi kwenye mzunguko kila mwezi. Pia hii ina maana sirikali hupeleka bajeti ndogo isiyozidi hata 50% kwenye serikali za mitaa tunapoishi!

10. watanzania wengi ni wavivu na matapeli wanaochagua kazi za kufanya hasa wenye elimu ya juu kidogo!!

11.mfumo mbaya wa elimu unaoandaa watu kufanya kazi za ofisi badala ya kujiajiri, wahitimu hutafuta kazi miaka hata mitano ndipo hushtuka na kujiajiri!

12. kukosekana masomo ya ujasiriamali kuanzia chekechea wakati serikali inajua haina ajira za kuwapa wahitimu!

13. sirikali kushindwa kuwa na political will na mikakati ya kuondoa tatizo la ajira! akili yote iko kwenye miundombinu tu!!

14. wananchi kushindwa kupaza sauti kuwa wanakufa na njaa kwa ukosefu wa ajira

15. raia kushindwa kutumia sanduku la kura kujitetea!!
Uchambuzi mzuri sana
 
Sio waache kuwa tegemezi wapate elimu ya kujua hakuna kiongozi atakae watilia pesa mfukoni na kuwapelekea vibaba majumbani!
Hao viongozi wenyewe wa Serikalini from Magu to nani huko wote walianza kwa kuajiriwa hakuna hata mmoja kati yao aliyekua na uthubutu wa kujiajiri lkn leo ndio wa kwanza kuwaambia vijana wajiajiri.
 
Ajenda kuu mwaka huu iwe ni suala la ajira watanzania tujiulize nani ana sera nzuri za kuwapa watoto wa wenye Nchi ajira ili nao wafike mahali pazuri kama ambavyo na wenyewe walipata ajira wakafikia hizo nafasi kubwa kubwa.

Tuache Kwanza habari za nyongeza ya mshahara kwa watumishi tujue inakuaje kuaje vijana wanazidi kumaliza chuo kilio kikiwa ni ajira ili waache kuwa wategemezi.
Hakuna serikali yoyote dunianj inayoweza kuajiri graduate wote mkuu jukumu la serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa kuweka Sera nzuri za uwekezaji,Kodi rafiki kwa wajasiliamali pamoja na mambo mengine yanayofanana na hayo...ajira kwenye sekta rasmi huwa ni kwa wachache
 
Back
Top Bottom