kutoka dodoma, maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kutoka dodoma, maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kagosha, Feb 10, 2011.

 1. k

  kagosha Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kuhusu swala la arusha, waziri mkuu alidanganya taifa na bunge, mbuge lema aomba mwongozo kuhusu upotoshwaji huo, mama kawa mbogo
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nami nimemsikia Mama Makinda akilizima swali la Mbunge huyo. Sio hilo tu, WM pia amejibu ki-Makamba maswali mazuri ya KUB Mbowe.
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Endelea kutujuza mkuu maana wengine tupo katika mihangaiko ya kila siku, hakuna access ya kuangalia tv
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ajali ya Maspika Bungeni Dodoma Kuteleza Jukumu la Kutetea
  'Sauti za Wachache' (Minority Voices) Na Hatari yake

  Kukuza Mbegu ya Siasa za Chuki kwa Taifa letu
  [​IMG]

  Je, tunapozungumza Kidemokrasia na kwa kuzingatia misingi yote ya UTAWALA BORA hapa nchini kwetu, serikali yetu kweli inafahamu maana halisi na tafsiri ya SAUTI YA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE (Minority Voices) WANAPOCHUKUA HATUA YA KUTUMIA SILAHA YA KIDEMOKRASIA KUTOKA NJE YA BUNGE pindi wanapopinga jambo wasiloliafiki kimsingi??

  Silaha hii ya kutoka nje ya bunge, kwa wale wanaoelewa vema demkrasia katika vitendo halisi, ni silaha hatari sana ambayo hutumika na waunguana badala ya kupigana ngumi kufuatia mijadala fulani. Silaha hii hutumika hasa pale ambapo KIKUNDI FULANI CHA WATU WENGI KINAPOTUMIA WINGI WAO VIBAYA (Majority Force) kulazimisha jambo BILA KUZINGATI MANTIKI INAYOTAWALA JAMBO HUSIKA NA AU SHERIA, TARATIBU NA KANUNI zilizopo.

  Endapo itabainika kwamba serikali yetu chini ya CCM hujionea tu jambo hili kama kiji-sinema wabunge wa chama chochote wanapotibuliwa kupita kiasi na kujiamulia tu kutumia hii salaha kama hatua ya mwisho kabisa kuonyesha KUTOKUAFIKI JAMBA FULANI na pengine serikali hata ikaendelea tu kujifariji kwamba kimataifa LUGHA HII YA MWILI KIDEMOKRASIA haina gharama yake kwa taifa letu, basi watakua wanajidanganya sana mchana mchana. Lakini naamini kwamba watu wengi sana tu wenye upeo mkubwa ndani ya taifa hili wanaelewa fika tafsiri ya lugha hii.

  Hakika, utawala bora ni pamoja na KULINDA VILIVYO MINORITY VOICES na pale tunaposhindwa kufanya hivyo basi mjue ya kwamba dereva wa gari lililobeba wale watu wengi huenda asifike salama; atawamwaga njiani abiria wake kabla safari haijakamilika kimatarajio. Kipimo halisia wa utawala bora katika nchi hupimika zaidi kutokama na ujumbe usiokua wa maneno tunaoupata usoni mwake mnyonge.

  Mfano mzuri nchini ni kwamba bila Mwalimu Nyerere kutambua ukweli huu leo hii nchini mwetu tusingekua na huu Mfumo wa vyama vingi kamwe.

  Dunia inatuangalia sana tunavyoenenda katika kujitawala huku na pengine hata kutucheka jino-pembe kama taifa lililosheheni wanadiplomasia mahiri sana kwa viwango vya kimataifa LAKINI WASIOKUA NA MAANA YOYOTE KWA SEHEMU MUHIMU YA JAMII YAKE YENYE SAUTI DHAIFU!!!

  Mhesimiwa Spika, Mama Anna Makinda, kama referee kwenye jumba letu la mijadala Dodoma, wala hatuhija mtu kutukumbusha kwamba wajibu wako namba moja bungeni humo ni KUHAKIKISHA WAKATI WOTE KWAMBA SAUTI DHAIFU INAPEWA SANA UZITO, HULINDWA NA HUPEWA MOYO WA USHIRIKI SALAMA. Mimi naamini sana kwamba hali hii inaweza kabisa ikazuiliwa kwa kupendelea zaidi kutenda haki wakati wote uwapo kazini hapo.

  Kinyume cha hapo mama yetu utakapoponyokwa miiko ya usimamizi wa mijadala kwa kulinda HAKI na kuanza KUTIA TIMU kwenye kile kikundi cha 'wasakata kabumbu ya nyumbani' basi hapo ndipo utakapofanikiwa sana kupanda mbegu mbaya sana (Political Animorsity) ya chuki ndani ya taifa letu. Hata kule Pemba na Unguja ile sura mbaya ya vipindi vilivyopita haikunyesha tu kama mvua; tuliilea sisi wenyewe kwa kutovutiwa sana kutenda haki!!!

  Na uzoefu unaonyesha kwamba kwa hali ya aina hiyo wewe mwenyewe utakua unasaidia kwa kiasi kikubwa sana kukiangamizi hicho kikundi kipenzi au kiwakilishi chake na wananchi nao kusubiri kukirudishia KURA ZA CHUKI hivo hivo kama ishara ya kutaka kumtetea mnyonge aliyeonekana kunyongwa hadi na HAKI YAKE bungeni - Ndugu Ndugai, hebu litafakari kidogo hili ninalolisema hapa kwa faida ya mijadala ijayo!!!

  Taifa lisiloweza kulinda vilivyo sauti dhaifu katika ngazi yoyote ya jamii haina tofauti sana na wanaukoo wanaogombania mali ya marehemu na kuwaacha solemba wajane na yatima huku wakijipongeza kama zuzu na tonge linalobana kwenye koo!!!!
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hebu nunueni visimu vyenye redio. 92.3 ya TBC wanatangaza laivu sasa hivi.
   
 6. Kagwina

  Kagwina Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli ukipenda Penye pengo utaita mwanya! Tuwe objective badala ya kujadili hoja kimajungu na kwa upande mmoja! Ipo siku chadema itachukua dola, tutawapima kwa uchambuzi mnaoufanya kama leo, tuache ushabiki!
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  WM wetu, mtu aliyebobea kwa maswala ya USALAMA wa TAIFA, amemjibu KUB Mbowe utadhani hakuwepo hapa nchini wakati yale yaliyotokea Arusha yanafanyika!
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Simbachawene naye anajaribu kujikomba kwa WM. Ana Makinda amemkatalia.
   
 9. r

  rmb JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hizo simu za radio hazitatatua hili tatizo, dawa yake waweke radio zao na Tv zao online tutazipata tu kiurahisi kuliko hizo simu!
   
Loading...