Kutoka Dodoma: Fedha za kuhonga wajumbe wa NEC ya CCM zakamatwa!

Kwani wewe ulikuwa bado hujajua kuwa nchi yetu ilikuwa imekaribia sana kupigwa bei kwa wafanyibiashara wakubwa hapa nchini na wawekezaji wa nchi za nje?

Kutokana na tukio la kukamatwa hizo milioni 700 ndiyo tunaukumbuka wosia muhimu sana aliotuachia Mwalimu Nyerere aliposema Ikulu kuna biashara gani hadi mtu aikimbilie Ikulu kwa nguvu zake zote huku anatumia mabilioni kuhonga wapiga kura?

Aliendelea kusisitiza kuwa mgombea wa namna hiyo ni wa kumuogopa kama ukoma.

Hata hivyo waTz wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunalazimika kuvipongeza vikao vya kamati ya maadili ya CCM, kikao cha CC na kikao cha NEC ya CCM kwa kuirescue nchi yetu 'kupigwa bei' kutokana na kitendo chao cha kishujaa na kizalendo cha kuwakata baadhi ya wagombea 'wazito' ambao kutokana na matumizi yao makubwa sana ya mabilioni ya shilingi wakati wa kutangaza nia, ambapo ilikuwa dhahiri mabilioni hayo ya shilingi walikuwa wamepewa na wafanyibiashara wakubwa hapa nchini, ambapo ni dhahiri pia kulikuwa na makubaliano na wagombea hao ya kurejeshewa mabilioni hayo waliyoyawekeza pamoja na 'riba' kubwa mara tu watu wao hao watakapokuwa wametinga Ikulu!


mkuu we ni mtu wa ajabu sana,ni ccm hiyo hiyo iliyoko madarakani ndo unasema ilikaribia kupiga bei nchi na hiyo hiyo ndo unasema imeokoa jahazi.binafsi nashindwa hata kukuelewa.hii hii ccm iliyoko madarakani ndo imekuwa ikiuza nchi na hii hii ndo unasema imeokoa nchi kuuzwa.mbona unajitekenya na kucheka mwenyewe?
 
Namuonea huruma sana dereva tax aliyembeba mwasibu Wa quality group aliyempeleka hotelini na mabagi ya hela na sasa akapigiwa simu ya kumrudisha
1. Kwa mtu mjanja, msaka noti, angeweza kusoma kampeleka MTU wa aina gani hotelini
2. Wakati anaitwa tena alijengewa mazingira ya kujikwamua akambwela mbwela, very sorry brother, milioni 720 hahah hah hah ,

Hata Mungu angemsifu kwa kuwaokoa watanzania kwa sababu hata huko ziliko sasa watazigawana zote.
 
Nani kasema ni million700,na kwamba zimetolewa na manji?pia ni nani alilenga kuhonga wajumbe hao?ni vema tusubiri uchunguzi wa vyombo vya dola ukamilike ili tuwe na la kusema.

vyombo vya dola vipi?hawa majambazi waliousambaratisha uhai wa mwangosi mchana kweupe mbele ya camera!!!!wa wapi wewe?
 
Hebu tupe picha kamili
yaani ilikuwaje mchongo ukastukiwa na ilikuwaje haswa
dreva texi alibugi wapi?
Tililika mkuu
 
mkuu we ni mtu wa ajabu sana,ni ccm hiyo hiyo iliyoko madarakani ndo unasema ilikaribia kupiga bei nchi na hiyo hiyo ndo unasema imeokoa jahazi.binafsi nashindwa hata kukuelewa.hii hii ccm iliyoko madarakani ndo imekuwa ikiuza nchi na hii hii ndo unasema imeokoa nchi kuuzwa.mbona unajitekenya na kucheka mwenyewe?

Wabongo uelewa wetu unatia mashaka, punde utawaona kwenye foleni za kupokea kanga na kapelo za ccm.
 
Dereva alipo fika hotelini wakati mhindi anapakia hayo mabegi ya hela mhindi alikuwa anamwambia jamaa akae mbali kidogo na gari! hata jamaa siamin kama angeweza kuchomoka na gari
 
Moderators ondoeni thread kama hizi zenye elements za kibaguzi...ilitosha kuwataja Manji na Rostam na sio kuwahusisha wahindi wote...tunaposema Chenge ni Mwizi basi hatumaanishi kabila lake pia ni wezi
Hatuwabagui kama unavyotaka kuaminisha.Tunawakataa kwa kutufanyia mambo ambayo mtu asiye kuwa Mhindi hawezi kuyafanya India hivyo hatuko tayari kuona wanadharirisha nchi yetu na Watu wake hata kama ni masikini.
 
mkuu hakuna nchi yeyote isipokuwa india ikawaruhusu wahindi kumiliki uchumi ikasalimika hawa majamaa ndo yana run Tanzania kwa sasa mfano rostam yeye ana run East Africa yani wamefikia kutuchagulia nani awe rais karibu tenda zote kubwa kubwa za nchi hii wao ndo wanazichukua
 
Unajua mikoani na hata huko Dar es Salaam kuna watu wanaothamini ubinadamu bado na sio kwamba wote wana roho kama za watawala wetu waliotufikisha hapa tulipo! Kitendo alichofanya outwardly unaweza ukaona ni ujinga kwake lakini kitakuwa na matokeo makubwa sana kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida kama wewe na kufaidisha watu wengi badala ya yeye mmoja.
Kikubwa kabisa kasaidia kumtambulisha rasimi na ushahidi wa wazi huyu fisadi papa ambaye amesumbua sana michezo na siasa za nchi hii kwa muda mrefu. Unadhani ingelichukua muda gani kupata ushahidi wa wazi kwa mtu aliyekopeshwa sh 9b nssf akajengea majengo na akayauza kwa nsff hiyo hiyo kwa 90b kwenye muda usiozidi hata miaka mitatu!!!??
 
Dereva alipo fika hotelini wakati mhindi anapakia hayo mabegi ya hela mhindi alikuwa anamwambia jamaa akae mbali kidogo na gari! hata jamaa siamin kama angeweza kuchomoka na gari
Kwa mtu mtafutaji angeweza kufanya chochote kujikwamua. Hakika atabaki kama alivyo
 
Nani kasema ni million700,na kwamba zimetolewa na manji?pia ni nani alilenga kuhonga wajumbe hao?ni vema tusubiri uchunguzi wa vyombo vya dola ukamilike ili tuwe na la kusema.

team membe kwishaa kwisha kwisha kabisaaa nyang'anyang'a ndembe ndembe na manji wenu
 
Namoonea huruma sana dereva tax aliyembeba mwasibu Wa quality group aliyempeleka hotelini na mabagi ya hela na sasa akapigiwa simu ya kumrudisha
1. Kwa mtu mjanja , msaka not, angeweza kusoma kampeleka MTU Wa aina gani hotelini
2. Wakati anaitwa tena alijrngewa mazingira ya kujikwamua akambwela mbela, very sory brother , milioni 720 hahah hah hah ,
Hata mungu angemsifu kwa kuwaokoa watanzania kwasababu hata huko ziliko sasa watazigawana zote

Ungekuwa ww hungeondoka nazo au? Utakufa kijana kwa tamaa ya pesa! Unafikili wenye ela watakuwaja bure uondoke na ela tu
 
Arooo,arooooo,arooooo,kamanda Nzowa,hebu reta vijana wako wakiwa na difenda kama saba hivi wakuje kumuaresti mtoa mada kwa kuchochea ujambaziii,mwambie na Msangi nae arete vijana wake wa antirobari wampe nakos za kutosha hiri rijamaa,inaerekea ni rijambazi sugu sana,rinatamani hera asizozitorea jashoooo,overrr
 
Kwa hiyo huyo aliyekamatwa anahusika vipi ma Membe?? naona mara yeye ni wa teamlowassa mara membe! SIELEWI! Ebu naomba tufumbue macho " vipofu".

maana yake hapo anatumia vidonge vya kuuwa makali....... So asije sahau kumeza siku moja ikawa shida na hatujawahi kuzika raisi akiwa madarakani
 
Wakati anaelezea huyo dereva tax huo upuuzi wake, nikijiwazia nilivyo na taabu ya hela , nikaona kaupenyo kalivyokuwa wazi , tena hela zilizokuwa zimeandakuwa kuwaunguza watanzania
Kuna chozi zito kama nchirizi Wa asali ulinitoka , loooh jamaa atakuwa masikini nileleeee
 
Back
Top Bottom