Kutoka dereva wa lori mpaka nahodha wa jahazi; je kule jahazi linapotakiwa kufika pakoje?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,467
"Jahazi hili, upepo uwe mwingi, upepo uwe mdogo, jahazi hili lazima likate mawimbi hili safari ifike." Mhe. Rais Samia.

Dereva wa lori, Mungu amrehemu, nae alisema anatupeleka kwenye nchi ya asali na maziwa, hivyo tulitakiwa kutulia na kuwa kwenye mako wowote ule. Lakini ndio hivyo katutoka.

Sasa tumeshushwa kwenye lori na kuingizwa kwenye jahazi, na tunaambiwa vyovyote vile lazima tufike ila hatujaambiwa mwisho wa safari patakuwaje, na itachukua muda gani.

Je, lilipokuwa linaenda lori ndio jahazi linaelekea?
 
Watanzania hatuna shida bora tufike tu mkuu, hata jahazi lingeendeshwa na dereva toyo🙁!.
 
Back
Top Bottom