Kutoka DarTECH hadi D.I.T (Dar es Salaam Institute Of Technelogy)

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,040
Wadau Kunani JF mbona sijaona thread yoyote inayohusu taasisi au chuo hiki kwa mazuri na mabaya yake? Kama kuna yeyote anajua kisa na mkasa atafanya la maana kama atanijuza kupitia hapa hapa, hivo hivo. Inaniwia ngumu kuamini kuwa DIT haipati au haina wadau wa kuweza kumwaga nyuzi hapa kha! Mi ninazo lakini mmh! Kimya kimezidi juu ya DIT hapa jamvini.
Nijuzeni au nitoeni shaka kwanza kabla sijaachia bureki...!
Nawasilisha Wakuu.
 
Lengo si kusema tu mkuu, ni kuchochea yaliyo mazuri au kukemea mabaya..lazima kuwepo sababu za msingi hadi taasisi au ishu iingie kwenye jamvi
 
Lengo si kusema tu mkuu, ni kuchochea yaliyo mazuri au kukemea mabaya..lazima kuwepo sababu za msingi hadi taasisi au ishu iingie kwenye jamvi
<br />
<br /> Hiki kimya mkuu kinatisha juu ya taasisi kubwa kama DIT kuna mengi pale jamani.
 
Kutoka DarTECH hadi D.I.T (Dar es Salaam Institute Of Technelogy)

sawaaaaaaaa.....
 
1. Mkurugenzi wa Fedha na utawala anakaimu nafasi hiyo kwa miaka zaidi ya minne sasa.
2. Yupo kigogo mmoja ameisababishia hasara ya mamilioni ya fedha taasisi hiyo na mambo yamemalizwa kimyakimya na akaachwa aondoke kiulaini na sasa anakula maisha chuo cha mipango Dodoma. Kigogo huyu ambaye alikuwa mkuu wa idara ya utumishi anatuhuma za kuwapa mikataba ya ovyo baadhi ya wafanyakazi nakupelekea taasisi kushitakiwa mahakamani na kulazimika kulipa fidia kubwa.
3. Kigogo huyo kama haitoshi anatuhumiwa kuwaidhinishia udhamini wa mikopo ya benki kwa wafanyakazi hata walio ktk ajira ya mwaka 1 huku benki (@mil2hadi3)wakati masharti ya mkopo ni makato kwa miezi 36 (miaka 3) hivyo taasisi kulazimika kulipa deni lililobaki baada ya mfanyakazi kumaliza mkataba wake.
4. Mikataba ya ovyo kwa wafanyakazi ni jambo lililogeuka kuwa kawaida, nahii ni kutokana na ubabe wa baadhi ya wakubwa wa taasisi hasa mkuu wa utumishi Bi Alice Mwasyoge na kaimu mkurugenzi wa fedha na utawala Bw. Monie Kiluswa.
5. Ni taasisi pekee ambayo baadhi ya watumishi imekuwa kama shamba lao kwa kuingia na kutoka watakavyo. Mfano ni Bw. H. Rashid na Bi Alice walishawahi kuacha kazi (kwa wakati tofauti) na kurudi kila walipoamua kufanya hivyo.
6.Mkuu wa Chuo ni Prof. Kondoro ana mtandao wa kifisadi alioujenga ndani ya chuo kwa mbinu ya kuweka vilaza ktk idara nyeti hasa Idara ya utawala na fedha, na idara ya mshauri wa wanafunzi (dean of students) ndo imeoza na haina lolote imejaa vilaza wa kutosha kabisa.
7. Afisa uhusiano Bw. Kakana ni mtu ambaye amekosa uadilifu kupindukia. Si ajabu ukimsikia akijinasibu kuwa ye ni mtoto wa mjini na hakuna wa kuweza kufichua maovu juu ya DIT hasa kupitia vyombo vya habari kwani kuna fungu linatengwa kwaajili ya ofisi yake ili kulainisha mambo na yeyote atakayethubutu kupeleka maovu jina lake litamfikia kabla ya habari kuchapishwa au kutolewa. Hii imedhihirika ktk madai mbalimbali na hasa mgomo wa wanafunzi mwaka 2005 (mliokuwapo mtakumbuka) vyombo vya habari havikutoa nafasi sawa kwa wanafunzi na uongozi ipasavyo, pamoja na kuwepo kwa waandishi wa televisheni zaidi ya 2 ni moja tu iliyorusha habari ile japo kwa dk 4 na hakuna sehemu ktk taarifa hiyo ilionyesha au kusikika wanafunzi wakitoa malalamiko yao.
8. Kauli za vitisho kwa wanafunzi hasa wanapoonyesha kushitukia janja ya uongozi ya kuwarubuni viongozi wa serikali ya wanafunzi ili waweze kuwagawanya na kuwa rahisi kuwatawala.
9. Ushahidi ninao mwenyewe kwa yote niliyoyaandika hapa. Kuhusu mtiririko wa uwasilishaji tusameheane na msisahau kuwa mimi ni Mwendabure!
10... DIT kunani pale?
 
Back
Top Bottom