Elections 2010 Kutoka Daras la 7 moja kwa moja form one ni kuboresha Elimu au?

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
583
287
Katika harakati zinazoonyesha kutapatapa kwa CCM kutokana na kukaliwa kooni na sera bora za Elimu za CHADEMA, jana Waziri wa Elimu Prof. Jumanne Maghembe alitoa ya mwaka pale same aliposema CCM katika kuboresha elimu inafanya mabadiliko makubwa ifikapo 2012. Katika mabadiliko haya wanafunzi watakaomaliza Darasa la 7 wataendelea moja kwa moja kidato cha Kwanza hadi cha nne bila mchujo( yaani mtihani wa daras la 7 utakuwa aidha haupo au utafanywa tu kama procedure pasipo kuwa kigenzo cha kumchagua mwanafunzi for the next level)

Swali la kujiuliza ni Je hapa tunaboresha elimu au tunaboronga zaidii?
Takwimu za asasi ya TWAWEZA inaonyesha kwamba kuna wanafunzi wengi wanamaliza kidato cha 4 hawajui kusoma na kuandika pamoja na kwamba kuna mtihani wa kuchuja darasa la saba kupata best students wa kwenda form 1. Sasa kama wanafunzi watapita DRS la 7 bila mchujo ni hakika tutakuwa na wahitimu wa kidato cha sita wasiojua kusoma na kuandika.

Lakini kubwa zaidi kinachoonekana hapa ni kwamba waziri amekurupuka ili tu kujibu sera za CHADEMA bila kufanya utafiti kama kawaida ya CCM wakifikiri wananchi watarudisha majeshi nyuma na kuacha kumpigia kura DK Slaa.
Ni vema wananchi wajue kwamba mfumo huu wa CCM bado hautawasaidia kwani badala ya kuwasaidia litakuwa na madhara makuu matatu:

1. Bado elimu itatolewa kwa wazazi kuendelea kuwagharamia watoto wao tofauti na CHADEMA wanaotoa Elimu bure tangu Chekechea hadi Form six

2. Ubora wa elimu utazidi kushuka kwani bila mtihani huwezi kupima kama tuna watanzania Competent na hivyo kujifariji kuwa na wasomi wengi kumbe mbumbumbu

3. Bado miundo mbinu na huduma za kielimu na uwezeshaji wa waalimu utabakia tatitizo kubwa la kudorora kwa elimu nchini Tanzania.

Tunachojifunza hapa ni kwamba bado serikali yetu haitaki kufanya utafiti wa kina na wa dhati ili kujua tatizo la elimu Tanzania na kuweka mkakati wa Dhati wa kuboresha. Kwa ufupi Prof. Maghembe amekurupuka tu ili kumwongezea JK nguvu ya kushinda ila hakuna utafiti uliofanyika kuonyesha mafanikio ya hiyo programme. Ili tuboreshe elimu ni lazima tuepuke kuifanya kisiasa kama Maghembe na JK wanavyotaka kuifanya.

Ila wajue wamezoea kuwachezea kwa ahadi za danganya toto. tumeshtuka na hatudanganyiki SLAA NDIYE RAIS AJAYE
 
Back
Top Bottom