Kutoka daraja mbili; lema afanya kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka daraja mbili; lema afanya kweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masingo sharili, Oct 21, 2012.

 1. m

  masingo sharili Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KATIKA HALI YA KUSHANGAZA VIJANA WAWILI WALIVAMIA MKUTANO WA CHADEMA KTK KATA YA DARAJA MBILI ULIOHUDHURIWA NA MAMIA YA WANANCHI KUTOKA MITAA YA SANARE, DARAJANI, JAMUHURI NA MITAA MINGINE YA KATA HIYO. LEMA ALIKUWA JUKWAANI KUMNADI MGOMBEA WA CHADEMA KTK KATA YA DARAJA MBILI BW. PROSPER MSOFE AMBAYE ANAONEKANA KUVUTA UMATI MKUBWA WA WANANCHI KTK MIKUTANO YAKE YOTE NILIOISHUHUDIA KWA MACHO YANGU.

  KTK HALI ISIYO YA KAWAIDA VIJANA HAO WALIANZA KUZOMEA ZOMEA KILA MARA WAKATI LEMA AKIHUTUBIA. KITENDO HICHO KILISABABISHA VIJANA WA RED BRIGADE WA CDM KUWAKAMATA NA KUWAHIFADHI MBELE YA JUKWAA LA MKUTANO ILI KUWAEPUSHA NA KIPIGO KUTOKA KWA WANANCHI WALIOKUWA WAMEFURIKA ENEO HILO. BAADA YA MKUTANO KWISHA, ZOEZI LA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUMWEZESHA DIWANI LILIENDELEA AMBAPO ZAIDI YA SH.1600000 ZILIPATIKANA. BAADA YA HAPO, ZOEZI LA KUVUA GAMBA LILICHUKUA NAFASI AMBAPO MABALOZI WAWILI NA WANACHAMA WENGINE 20 WALIREJESHA KADI ZA CCM NA KUKABIDHIWA ZA CDM.

  MWISHO, mh. lema aliamuru wale vijana wawili wapandishwe jukwaani ambapo alielezea jinsi ambavyo alikuwa akiwasadia ikiwa ni pamoja na kuwanunulia boda boda 2 kama mtaji na akawaagiza wawe wanatoa mrejesho wa sh 30000 kwa wiki ili kutengeneza mtaji wa vijana wengine wa Arusha LKN vijana hao walitokomea na baadaye wakaibuka kwa mbunge wa viti maalum wa cdm hapa arusha wakiomba wasaidiwe mtaji wa kuuza matunda, mbunge huyo aliwapa sh. 400000. BAADA YA MDA walirejea tena kwa lema wakidai sh 1000000 ya kufanya biashara, MH. LEMA ALIWAKATALIA NA ALIWATAKA WAREJESHE KIASI CHA ZILE FEDHA ZA BODA BODA ILI KUSAIDia VIJANA WENGINE WASIO NA AJIRA KTK JIJI LA ARUSHA, CHA KUSHANGAZA VIJANA HAO WALIPONYIMWA PESA WALIZOKUWA WANAHITAJI KTOKA KWA LEMA WALIANZA KUZUNGUKA MITAANI WAKIMCHAFUA NA HATA KTK MITANDAO YA KIJAMII. KAMA HAITOSHI VIJANA HAO WAWILI WLIVAMIA MKUTANO WA CDM DARAJA 2 SIKU YA IJUMAA TAR. 19/10/2012 KWA LENGO LA KUVURUGA.

  Baada ya lema kumaliza maelezo yake pale jukwaani, wananchi walipandwa na jazba na kutaka kuwavamia wale vijana LKN MH. LEMA ALITANGAZA KUWASAMEHE AMBAPO WANANCHI WENYEWE WALIONEKANA KUKATAA MSAMAHA HUO, NDIPO LEMA ALIPOAMURU GARI LAKE KUSOGEZWA KARIBU NA KUWAPAKIZA WALE VIJANA WAWILI ILI KAWAOKOA NA KIPIGO KUTOKA KWA UMATI WA WATU ULIOKUWA UMEPANDWA NA JAZBA KUTOKANA NA KUKERWA NA VIJANA HAO. aidha ktk kuhitimisha msamaha wke kwa vijana hao, LEMA ALIWAPA SH. 20000 KILA MMOJA NA KUWATAKA WAACHE USHAROBARO NA WAJITUME KUFANYA KAZI.

  MY TAKE:
  Huo ndio ukweli kuhusu tukio lililomuhusisha lema na wale vijana wawili ktk kata ya daraja2 tar.19/10/2012, hivyo wana jamii tuepukane na propaganda za kupindisha habari ikiwemo kumchafua mh. lema. bila sababu ya msingi.
   
 2. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  pamoja sana mkuu...
   
 3. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Walianza lema katapeli uwanja wakaibika, wakaja kupewa kichapo lema wameaibika magamba bwana yanangaika na singo mpya kila sku zisizokubalika sokoni. Sjui sasa watakuja na single gani?
   
 4. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Tunashukuru kwa ufafanuzi wako kwani kuna mjinga mwingine ambaye ameleta uzi hapa akidai kuwa Lema amepata kichapo jukwaani. Ngoja ni copy nimuunganishie na upuuzi wake.
   
 5. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hao magamba watasumbuka sana Arusha chadema ipo juuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
 6. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kumbe picha yenyewe ndivyo ilivyokuwa? tuko pamoja.
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Hii ndio taarifa kamili na imejitosheleza kabisa, hongera mkuu, kuna mwana JF mmoja maarufu kwa jina la Ngongo(labda ni mmojawapo wanaodaiwa-sina uhakika-just joke) alianzisha thread hapa eti Kamanda Lema alipigwa kwenye mkutano huko daraja mbili!huku Ritz akishabikia sana!!Kamanda Lema Apigwe Arusha Patakalika???nasubiri Ngongo achangie hii thread!
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Daa kuna mtu alileta habari za uzushi humu! Naona sasa kapata haibu ya mwaka!
   
 9. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Ngongo ni mzushi. Uzi wake wa jana ulipaswa kuja April fools.
   
 10. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu ndo ukweli, waliokoewa na Lema kwa kuwaingiza kwenye gari, lake otherwise wananchi wenye hasira wangewamaliza!
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Walioleta habari za lema kutapeli uwanja, ama lema kapewa kichapo ni vijana wa kazi wanaotumwa na mkuu wa wilaya kwa ujira wa buku mbili, ambao wana connection na akina Ngongo na LENGIO.
  Ngongo sote tunamfahamu kwa tabia zake za kumchafua lema hata kabla ya uchaguzi. It is my impression that the same Ngongo has another ID, specifically LENGIO
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mods wa jukwaa hili la siasa. Paw na wenzio, naomba kwa heshima na taadhima Ngongo apewe ban pamoja na kuondoa thread yake ili akajifunze adabu na kuacha porojo. Hii ni kwa heshima ya JF. Alileta habari ya uchochezi ambayo ilihusu kupigwa kwa Lema na kutaka kumdhalilisha. Naomba Mods muwe waungwana katika hili.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Afadhali umetusaidia kutupa ufafanuzi. Tumekuwa tukifatilia habari ya Ngongo huko Soko kuu mjini kati ila tumepata taarifa zinazofanana na zako. Nimekuwa nikimuheshimu sana Mzee Ngongo, ila amejiharibia sana credibility yake. Namshauri awe anajaribu kufatilia taarifa zake vizuri kabla hajazirusha hewani, alichofanya ni ukiukwaji wa taratibu za JF zinazostahili BAN.
   
 14. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  niliposoma habari ya ngongo nilijua kuna ajenda imejificha,lakini ninapopata kuisoma habari hii ndo napata picha kamili.wabaya wa lema wanajitesa kwa kila namna ili kumchafua lakini wapi,hongera mkuu kwa kuleta facts,ntakupa like badae nw natumia mchina simu.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Alitakiwa apigwe ban kwa uzushi na uwongo
   
 16. s

  sokoinei JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,835
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nilikutana na uzi huo yani nilishang'aa sana jinsi ukweli ulivyo geuzwa,lakini sishangai kwani kunasiku lipumba alikuja arusha na wapambe wake kutoka dar aliwakodishia magari yenye sura ya kidaleslamu,kesho yake ikaandikwa hivii cuf yaiteka arusha.nilicheka sanaa juzi watu walifanya mkutano daraja2 Hawakupata hata watu 20,hayo ndo mazadhara ya kupika habar mwisho ni kuumbuka.eti lema apigwe mbele ya wafuasi wake kwenye mji wake!i!haimuingii akilini hatakama nikichaa ukimsimlia.cdm arusha tuko makin sana na kuna habari ya mgombea wa ccm daraja2 nikiiweka hapa mtacheka sana lakini haina haja hatuwez jadili udhaifu atapanda chat ya kujadiliwa na the greats.alisalitiwa na mtu alie zani ni ccm alikua nae ndani ya gari lake wakapita mahali yule jamaa akasema hebu shushe hapa nikachukue fegi ile ameshuka tu akanyoosha vidole viwili akasema peopleoo watu wakgjibu pawaaa.akageuka akamwambia we gamba ondoka minishafika asante kwa lift lakin njo cdm ukombolewe aliona aibuu.na kunamengi sana hatuwez mjadili
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  @Ngongo atakuwakiongozi wa kile chama chenye jogoo alimaizwa na lema hivyo mpaka leo ana hasira nae..
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. s

  sokoinei JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,835
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hatushangai sana lema wameshindwa kummaliza kisiasa.kwasababu anagusa mioyo ya watu na huwezi kubadili mchele uwe mawe labda kama mwanamazingaombwe,nyeupe naiwe nyeupe nyekundu naiwe nyekundu soda isiwe bia plz jifunzeni kuusema ukeli hata mungu atawasimamia muongo rafikiyake shetan na hatashinda anajiliwaza tu.arusha cdm lema.mkohapo?
   
 20. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Huyu ****** nyaji anatejiita ngongo jana alikuja hapa na mipasho yake tukamzodoa sana,mkuu heshima kwako kwa kuweka bayana ukweli wa kilichojiri....mods naomba huyu ngongo ale ban kwa uongo na maslahi yake binafsi ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hii.
   
Loading...