Kutoka CHADEMA: Updates juu ya msiba wa Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka CHADEMA: Updates juu ya msiba wa Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Jan 14, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]TANZIA[/FONT]


  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepatwa na majonzi makubwa na kinasikitika sana kwa kifo cha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa, Mheshimiwa Regia Mtema ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Mheshimiwa Regia Mtema amefariki leo tarehe 14 Januari 2011 kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu darajani.

  Katika uhai wake marehemu Regia Mtema amefanya kazi mbalimbali za kisiasa na kijamii katika taifa. Marehemu Regia Mtema amezaliwa tarehe 21 mwezi Aprili mwaka 1980 na kusoma shule za sekondari kidato cha kwanza mpaka cha sita katika shule ya sekondari ya Forodhani na Shule ya Wasichana ya Sekondari ya Machame. Marehemu Regia Mtema alipata shahada yake ya kwanza (Bsc Home Economics and Human Nutrition) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

  Mara baada ya kuhitimu masomo yake marehemu Regia Mtema alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na CHADEMA na kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA na baadaye kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya CHADEMA nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum.

  Viongozi wakuu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa, wajumbe wa kamati kuu, wakurugenzi wa chama makao makuu na wabunge wamejumuika hivi sasa na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.

  CHADEMA inatoa pole kwa familia ya marehemu Regia Mtema, wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Jimbo la Kilombero, wanachama wote wa CHADEMA, jamii ya watu wenye ulemavuTanzania na Watanzania wote kwa ujumla, kutokana na msiba huu wa ghafla katika wakati ambapo mchango wake ukihitajika kwa chama na kwa taifa.

  Taarifa zaidi kuhusu taratibu za maziko, itatolewa mara baada ya kukamilisha majadiliano baina ya familia ya marehemu, chama na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mipango ya mazishi ya marehemu inapangwa nyumbani kwa Baba wa Marehemu Regia Mtema, Ndugu Estelatus Mtema, Tabata Chang'ombe. Ratiba ya maziko itatolewa baada ya kukamilika kwa taratibu zinazopangwa na familia ya marehemu, Ofisi ya Bunge na chama.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu Regia Mtema, mahali pema peponi. Amina.

  Imetolewa na:

  John Mnyika(Mb)
  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni majonzi makubwa sana.Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.Jina la bwana lihimidiwe.
   
 3. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 412
  Trophy Points: 180
  asante sana kwa taarifa na poleni kwa msiba mzito.
   
 4. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  So sad.!
   
 5. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Inna lillahi wainnah ilayhi raajiuun!!
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Raha ya milele umpe ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani Amina!
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  RIP Regia. Thats all we can say.
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Lakini kwa nini mapema hivi dada Regia?kapumzike kwa amani mpendwa wetu!tuko nyuma yako
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Poleni sana CHADEMA na familia ya marehemu. RIP Regia Mtema!
   
 10. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Poleni sana wanaChadema. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,, Amen
   
 11. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Dificult 2blv on this sad news! Kichwa knaniuma coz of ths! Duh, my God z t true that, ma sisy Regy z no longer wit us! W ril nid ua mecy and comfort kwa kpnd hk kgumu! CDM, Mungu ka2nyanganya jembe! R.I.P our lvly sister, 2taonana tena paradiso! Bye, bye byee. Oooh my GOD!
   
 12. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Lala salama Mpendwa...
   
 13. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  My heart is bleeding today
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina lake libarikiwe.
   
 15. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  poleni sana cdm lakini hasa familia, tunaungana nanyi ktk kipindi hk kgm kwa kuomboleza, cha muhimu ni kuendeleza mshikamano wa vyama vyote kuifariji familia ya mh, Regina mtema, bwana alitoa na bwana ametwaa jila bwana libarikiwe Aamen.
   
 16. rasmanyara

  rasmanyara Senior Member

  #16
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tulikupenda sana lakini Mungu kakupenda zaidi.Mungu amlaze pema peponi mpambanaji Regia Mtema
   
 17. vengu

  vengu JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  Raha ya milele umpe eeh bwana na mwanga wa milele umuangazie..apumzike kwa amani!
   
 18. M

  MUHOJA-VENTURE Member

  #18
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni msiba mkubwa kwa taifa.Mungu amlaze pahali pema peponi.Amen.
   
 19. H

  Handsome Member

  #19
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jaman poleni sana ndugu zangu,Mungu mwema awatie Nguv sana,jaman ril ver ver sor Chadema,Mh.Mbowe na wote.
   
 20. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  May the good lord rest her soul in eternal peace
   
Loading...