BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,792
- 287,994
Credibility ya Ndulu ndiyo inazidi kushuka. Amekubali kubebwa na CCM katika kikao kisicho kichwa wala miguu ili wakaendeleze uwongo wanaowadanganya Watanzania, badala ya kusafisha uozo uliojaa BoT. Labda na yeye ameshakuwa mwajiriwa wa CCM, badala ya kushupalia mafisadi watajwe na yeye kuwataja maofisa waliosimamishwa BoT. Hana kichwa chochote pamoja na kuwa ni PhD holder.
Kufuru ya CCM Kikao cha NEC Butiama
na Kulwa Karedia
DALILI za awali zimeanza kuonyesha kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitakachofanyika kwa siku mbili baadaye wiki hii, Butiama, mkoani Mara.
Gharama hizo ambazo Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba hakuwa tayari kuziweka bayana zitahusisha usafiri wa wajumbe wanaotumia ndege, mabasi na magari mengine madogo, ukarabati wa jumba la mikutano, chakula na malazi kwa ajili ya wajumbe wapatao 210 wa kikao hicho muhimu.
Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinaonyesha kuwa, tayari baadhi ya wajumbe wa mkutano huo na waalikwa wengine walikuwa wameshaanza kusafiri kuelekea Butiama ambako kikao hicho cha NEC kitafanyika siku za Jumamosi na Jumapili.
Pamoja na Makamba na Mweka Hazina wa CCM Taifa, Amos Makalla, kutokuwa tayari kueleza kiasi ambacho kimetengwa kwa ajili ya kikao hicho wakitofautiana na alivyokuwa akifanya aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Philip Mangula, viongozi hao walikiri kukodi ndege za serikali zitakazokuwa zikisafirisha wajumbe hao kwenda mkoani Mara takriban kilomita 1,800 kutoka Dar es Salaam.
Mbali ya hilo, Tanzania Daima jana ilishuhudia baadhi ya wajumbe wakijiandaa kuanza safari yao hiyo ya kwenda Butiama kwa ajili ya kikao hicho kwa kutumia usafiri wa mabasi ya Shabiby yanayomilikiwa na mmoja wa makada maarufu wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba, jijini Dar es Salaam jana, Makamba alisema tayari maandalizi yote kwa ajili ya kikao hicho muhimu yameshakamilika.
Siwezi kuwaambia kiasi cha fedha ambacho kitatumika katika mkutano huu kule Butiama. CCM ni chama kikubwa ambacho kinafanya mambo yake kwa kufuata programu kwani bajeti zake zimepangwa hatukopi popote, alisema Makamba kwa kujiamini.
Licha ya kugoma kutaja kiasi cha fedha hizo, Makamba alitamba kwamba wajumbe wote wa mkutano huo watakaokuwa Butiama kwa muda wote, watakula, watalala na kurudi kwenye makazi yao bila ya tatizo lolote.
Napenda kuwaambia kwamba, wajumbe wote watakaokuwa Butiama kwa siku mbili watakula, watalala na watarudi kwenye makazi yao bila tatizo lolote sisi hatuombi au kukopa fedha kutoka sehemu yoyote kwani hizo ziko kwenye bajeti yetu ya chama, alisema Makamba.
Kwa upande wake Makalla alisema, CCM haina wasiwasi wa fedha za kuendesha mikutano yake kutokana na kujitosheleza.
CCM haina tatizo juu ya suala la fedha, kama alivyosema Katibu Mkuu mambo yetu yote yako kwenye bajeti kwa ajili ya kuendesha mikutano yote, alisema Makalla.
Mbali ya hilo, Makamba alisema kwamba, chama hicho kilikuwa kimemwita Butiama Gavana wa Benki Kuu, (BoT), Profesa Beno Ndullu, kwa ajili ya kile ilichokielezea kuwa ni kutoa mwelekeo wa hali ya uchumi wa taifa.
Napenda kuwaambia kwamba kabla ya kuanza kwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, wajumbe wote watapata semina kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu, lengo likiwa ni kufahamisha wajumbe wetu hali halisi ya uchumi wa taifa letu, alisema Makamba.
Uamuzi huo wa CCM kumuita Profesa Ndullu unakuja wakati taifa likisubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi wa Kashfa ya EPA ambayo ilimlazimisha Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM atengue uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali.
Makamba alisema katika mkutano huo ambao unaonekana kuvuta hisia za watu kutokana na matukio kadhaa yaliyotokea hivi karibuni, utajadili jumla ya ajenda nne, ikiwa ni pamoja na kutoa hali halisi ya mazungumzo ya kisiasa kati ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF).
Alisema ajenda nyingine itakuwa ni ya hali ya uchumi wa taifa, ambayo kwa siku za karibuni imepata mtikisiko, ikiwemo kashfa ya Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu pamoja na mawaziri, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.
Makamba alisema ajenda nyingine ni kutoa taarifa ya uchaguzi mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Kiteto, na kutoa taarifa za sherehe za miaka 31 ya CCM na matembezi ya mshikamano yaliyofanyika Februari mwaka huu.
Alisema pia kikao hicho kitapokea na kujadili taarifa nyingine zinazohusu uhai wa chama na maendeleo yake kwa ujumla.
Kuhusu uvumi kwamba CCM imeamua kufanyia mkutano kijijini Butiama kwamba ni kwenda kutambika kwenye kaburi la hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Makamba alisema si kweli, bali wanakwenda kufanya mkutano huo kutokana na utaratibu waliojipangia kichama.
Napenda kuwahakikishia kwamba hatuendi Butiama kutambika ndugu zangu, bali huu ni utaratibu wetu tuliojipangia wenyewe ndani ya chama, na pili tuna muenzi kutokana na mchango wake kwa taifa letu alioutoa wakati wa uhai wake, alisema Makamba.
Alisema hii si mara ya kwanza kwa CCM kufanya mkutano wake kama huu nje ya Dodoma, kwani miaka ya nyuma imekwisha kufanya katika mikoa ya Arusha mwaka 1967, ambako ilipitisha Azimio la Arusha lililohusu Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, mwaka 1972 mkutano kama huo ulifanyika mkoani Iringa ambako ulipitisha Siasa ni Kilimo, na mwaka 1970 kikao kama hicho kilifanyika Musoma na kupitisha Azimio la Musoma lililohusu Elimu ya Msingi kwa Wote.
Alisema sababu kubwa ya kufanya mikutano mikoani ni kuwawezesha viongozi kuwa karibu na wananchi, viongozi kupata nafasi ya kukagua shughuli za chama na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika mkoa ambako kikao kinafanyika.
Makamba alisema hadi jana, tayari uongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ulipokea maombi ya kuandaa Mkutano Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM unatarajiwa kuanza Machi 29 hadi 30 kwenye ukumbi wa Jumba la Maendeleo Butiama, ambako kabla ya kifo chake, Mwalimu Nyerere alikuwa akiutumia kuabudu, kabla ya kujengwa kanisa la kisasa.
Jumba hilo ambalo kabla ya mkutano huo lilikuwa katika hali mbaya, limefanyiwa ukarabati mkubwa unaokadiliwa kufikia sh milioni 300 na CCM Mkoa wa Mara.
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, alitoa taarifa hiyo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, hivi karibuni alipokwenda kujionea maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo lililojengwa mwaka 1972.
Alisema licha ya CCM kutoa kiasi hicho cha fedha, pia wahisani na watu mbalimbali walichangia kwa lengo la kufanikisha ukarabati huo, akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono.
size=4]
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 8 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
CCM watueleze watanzania ni nani DEEP GREEN, na kwa nini Rostam wa Iran ni mbunge wao wakati hana uraia. Wawavue uanachama Lowassa, mwanyika, Chenge, karamagi, balali, hosea, msabaha na mafisadi wote. Baadaye sasa wamuenzi BABA WA TAIFA. Achen unafiki CCM
na Maria Nyerere, Butiama, Mara, - 26.03.08 @ 09:52 | #3575
Namshukuru sana sana mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mtazamo wake wa mbali wa kuimarisha chama.
Naomba sana wajumbe wote wa Kikao hicho cha NEC watumie uwepo wao ktk kikao hicho kuimarisha chama kwa kueleza wazi wazi bila kulindana matatizo yote ktkt chama na serikali na kutoa mapendekezo kwa Mwenyekiti Taifa ili aweze kuchukua hatua staili.
Hivi sasa wannchi wa nchi hii sio wale wa miaka ya nyuma. Hivyo basi ili tuweze kukijenga chama chetu naomba tutoe mapendekezo kwa mfano mimi nikependekeza kwamba viongozi wote wa chama CCM walioingiza nchi ktkt umaskini mkubwa sana na kusababisha wananchi wa nchi hii kuingia kwenye gharama kubwa ktk matumizi ya kila siku watolewe uanachama kabisa na pia wachukuliwe hatua. Hii italete uhai mkubwa sana ktk chama.
Na ukirudi nyuma, siku Rais wa jamhuri ya Tanzania alivyohutubia bunge kwa mara ya kwanza, maneno yake yamefikia ktk utekelezaji wake kabisaaa.Hivyo naomba Mwenyekiti wa CCM Taifa akamilishe ahadi yake kwa vitendo bila kuona huruma ndio kujenga chama na maendeleo ya nchi hayapatikani bila kujitoa muhanga.
Nakumbuka hotuba za baba wa Taifa alisema halikuwa hana utani na mtu akifanya kosa au uzembe ktk mambo ya msingi ya nchi. Hivyo nkuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa usifanye utani ktk mambo ya msingi ya nchi, tumia mmlaka yako kama mwenyekiti wasambaratishe wote waliofanya mambo ya kuhiujumu nchi kwa maslahi yao binafsi.
Nawatakieni kikao chema chenye uelekeo wa kuimarisha chama chetu na maendeleo ya nchi nyetu.
Kidumu chama cha mapinduzi.
na jozee, Irg, - 26.03.08 @ 10:11 | #3576
hii ni kawaida ya ccm kufanya kufuru katika vikao vyake mbalimbali kwa pesa za mafisadi.naomba m/kiti wa ccmJK atutajie mafisadi wa EPA na waache unafiki kwa hili ***** hawezi kurudisha mali alafu unakataa kumtaja.huo ni unafiki na kutufanya watz kuwa wajinga na mambumbumbu.haya JK kazi kwako umeamua kuwapeleka mafisadi kwa hayati Nyerere,naona kama wanaenda kumkashifu mzee wetu ngoje afufuke sijui hizo sura zenu mtazipeleka wapi na ufisadi.asante
na fredy Godwin, Tumaini-iringa university, - 26.03.08 @ 10:38 | #3579
Ikiwezekana pia wakodi helikopta ya Mbowe kuwapeleka wajumbe wa NEC butiama
na kk - 26.03.08 @ 10:40 | #3581
Makamba na wenzake watambue kwamba wakati wa kujidai na kujigamba umepita, wawape wananchi haki zao.
Kuendelea kutamba kwamba CCM hawana tatizo na pesa wakati tunajua kwamba ni pesa zinazotokana na ufisadi ni kuendelea kutuumiza roho. Huku ni kuonyesha kwamba watu hawa hawana adabu na heshima kwa wananchi katika wakati huu mgumu wa ufisadi.
Kutambia hela ni ufedhuli na ujeuri usio na maelezo, ni kielelezo cha upeo mdogo wa uelewa wa viongozi wa chama kikongwe, CCM.
Maelezo ya kumuenzi Baba wa Taifa ni matusi kwa mzee huyo, kwani huwezi kumuenzi mtu kwa kupinga aliyoyasimamia.
Mungu awajalie viongozi wa CCM wafunguke macho na kuona ukweli na haki.
na Amk, Dar, - 26.03.08 @ 10:48 | #3583
Ni kikao cha kiini macho kama vikao vingine vya chama cha majambazi,hivyo wadanganyika wasitegemee kuwa kuna lolote jipya litapatikana labda wasubiri kusikia mbinu mpya zitakazotumika kulinda wafadhili wa ccm,yaani wakina epa,uchumond,ticks,songas,ubinafsishaji na kuendelea.........wasiguswe na mkono wa sheria.
na kadogoo, mbarara, - 26.03.08 @ 10:59 | #3585
sijui kwanini makamba ni katibu mkuu wa ccm?!
ningekuwa mimi jk katibu mkuu wa ccm ningeteua mtu mwenye uwezo mkubwa wa kazi,elimu,fikra na uzoefu kama Abdulharaman kinana,Salim Ahmed Salim au hata jaka mwambi au aggrey mwanri nk.
makamba anapwaya sana ktk nafasi nyeti kama hiyo!
na jingo - 26.03.08 @ 11:07 | #3587
Kama ccm haina tatizo na pesa, tunaomba maisha bora kwa watanzania wote na siyo kula na kulala ka wajumbe huko mkutanoni na hatimaye kurudi kwao salama. Makamba acha upuuzi, unaongea upupu sana, hufai hata kuwa katibu wa kata!!!
na Tyson, Butiama, - 26.03.08 @ 11:11 | #3588[/size]