Kutoka Butiama: Exclusive news

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Credibility ya Ndulu ndiyo inazidi kushuka. Amekubali kubebwa na CCM katika kikao kisicho kichwa wala miguu ili wakaendeleze uwongo wanaowadanganya Watanzania, badala ya kusafisha uozo uliojaa BoT. Labda na yeye ameshakuwa mwajiriwa wa CCM, badala ya kushupalia mafisadi watajwe na yeye kuwataja maofisa waliosimamishwa BoT. Hana kichwa chochote pamoja na kuwa ni PhD holder.

Kufuru ya CCM Kikao cha NEC Butiama

na Kulwa Karedia

DALILI za awali zimeanza kuonyesha kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitakachofanyika kwa siku mbili baadaye wiki hii, Butiama, mkoani Mara.

Gharama hizo ambazo Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba hakuwa tayari kuziweka bayana zitahusisha usafiri wa wajumbe wanaotumia ndege, mabasi na magari mengine madogo, ukarabati wa jumba la mikutano, chakula na malazi kwa ajili ya wajumbe wapatao 210 wa kikao hicho muhimu.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinaonyesha kuwa, tayari baadhi ya wajumbe wa mkutano huo na waalikwa wengine walikuwa wameshaanza kusafiri kuelekea Butiama ambako kikao hicho cha NEC kitafanyika siku za Jumamosi na Jumapili.

Pamoja na Makamba na Mweka Hazina wa CCM Taifa, Amos Makalla, kutokuwa tayari kueleza kiasi ambacho kimetengwa kwa ajili ya kikao hicho wakitofautiana na alivyokuwa akifanya aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Philip Mangula, viongozi hao walikiri kukodi ndege za serikali zitakazokuwa zikisafirisha wajumbe hao kwenda mkoani Mara takriban kilomita 1,800 kutoka Dar es Salaam.

Mbali ya hilo, Tanzania Daima jana ilishuhudia baadhi ya wajumbe wakijiandaa kuanza safari yao hiyo ya kwenda Butiama kwa ajili ya kikao hicho kwa kutumia usafiri wa mabasi ya Shabiby yanayomilikiwa na mmoja wa makada maarufu wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba, jijini Dar es Salaam jana, Makamba alisema tayari maandalizi yote kwa ajili ya kikao hicho muhimu yameshakamilika.

“Siwezi kuwaambia kiasi cha fedha ambacho kitatumika katika mkutano huu kule Butiama. CCM ni chama kikubwa ambacho kinafanya mambo yake kwa kufuata programu kwani bajeti zake zimepangwa… hatukopi popote,” alisema Makamba kwa kujiamini.

Licha ya kugoma kutaja kiasi cha fedha hizo, Makamba alitamba kwamba wajumbe wote wa mkutano huo watakaokuwa Butiama kwa muda wote, watakula, watalala na kurudi kwenye makazi yao bila ya tatizo lolote.

“Napenda kuwaambia kwamba, wajumbe wote watakaokuwa Butiama kwa siku mbili watakula, watalala na watarudi kwenye makazi yao bila tatizo lolote… sisi hatuombi au kukopa fedha kutoka sehemu yoyote kwani hizo ziko kwenye bajeti yetu ya chama,” alisema Makamba.

Kwa upande wake Makalla alisema, CCM haina wasiwasi wa fedha za kuendesha mikutano yake kutokana na kujitosheleza.

“CCM haina tatizo juu ya suala la fedha, kama alivyosema Katibu Mkuu mambo yetu yote yako kwenye bajeti kwa ajili ya kuendesha mikutano yote,” alisema Makalla.

Mbali ya hilo, Makamba alisema kwamba, chama hicho kilikuwa kimemwita Butiama Gavana wa Benki Kuu, (BoT), Profesa Beno Ndullu, kwa ajili ya kile ilichokielezea kuwa ni kutoa mwelekeo wa hali ya uchumi wa taifa.

“Napenda kuwaambia kwamba kabla ya kuanza kwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, wajumbe wote watapata semina kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu, lengo likiwa ni kufahamisha wajumbe wetu hali halisi ya uchumi wa taifa letu,” alisema Makamba.

Uamuzi huo wa CCM kumuita Profesa Ndullu unakuja wakati taifa likisubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi wa Kashfa ya EPA ambayo ilimlazimisha Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM atengue uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali.

Makamba alisema katika mkutano huo ambao unaonekana kuvuta hisia za watu kutokana na matukio kadhaa yaliyotokea hivi karibuni, utajadili jumla ya ajenda nne, ikiwa ni pamoja na kutoa hali halisi ya mazungumzo ya kisiasa kati ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF).

Alisema ajenda nyingine itakuwa ni ya hali ya uchumi wa taifa, ambayo kwa siku za karibuni imepata mtikisiko, ikiwemo kashfa ya Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu pamoja na mawaziri, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.

Makamba alisema ajenda nyingine ni kutoa taarifa ya uchaguzi mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Kiteto, na kutoa taarifa za sherehe za miaka 31 ya CCM na matembezi ya mshikamano yaliyofanyika Februari mwaka huu.

Alisema pia kikao hicho kitapokea na kujadili taarifa nyingine zinazohusu uhai wa chama na maendeleo yake kwa ujumla.

Kuhusu uvumi kwamba CCM imeamua kufanyia mkutano kijijini Butiama kwamba ni kwenda kutambika kwenye kaburi la hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Makamba alisema si kweli, bali wanakwenda kufanya mkutano huo kutokana na utaratibu waliojipangia kichama.

“Napenda kuwahakikishia kwamba hatuendi Butiama kutambika ndugu zangu, bali huu ni utaratibu wetu tuliojipangia wenyewe ndani ya chama, na pili tuna muenzi kutokana na mchango wake kwa taifa letu alioutoa wakati wa uhai wake,” alisema Makamba.

Alisema hii si mara ya kwanza kwa CCM kufanya mkutano wake kama huu nje ya Dodoma, kwani miaka ya nyuma imekwisha kufanya katika mikoa ya Arusha mwaka 1967, ambako ilipitisha Azimio la Arusha lililohusu Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, mwaka 1972 mkutano kama huo ulifanyika mkoani Iringa ambako ulipitisha Siasa ni Kilimo, na mwaka 1970 kikao kama hicho kilifanyika Musoma na kupitisha Azimio la Musoma lililohusu Elimu ya Msingi kwa Wote.

Alisema sababu kubwa ya kufanya mikutano mikoani ni kuwawezesha viongozi kuwa karibu na wananchi, viongozi kupata nafasi ya kukagua shughuli za chama na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika mkoa ambako kikao kinafanyika.

Makamba alisema hadi jana, tayari uongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ulipokea maombi ya kuandaa Mkutano Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM unatarajiwa kuanza Machi 29 hadi 30 kwenye ukumbi wa Jumba la Maendeleo Butiama, ambako kabla ya kifo chake, Mwalimu Nyerere alikuwa akiutumia kuabudu, kabla ya kujengwa kanisa la kisasa.

Jumba hilo ambalo kabla ya mkutano huo lilikuwa katika hali mbaya, limefanyiwa ukarabati mkubwa unaokadiliwa kufikia sh milioni 300 na CCM Mkoa wa Mara.

Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, alitoa taarifa hiyo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, hivi karibuni alipokwenda kujionea maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo lililojengwa mwaka 1972.

Alisema licha ya CCM kutoa kiasi hicho cha fedha, pia wahisani na watu mbalimbali walichangia kwa lengo la kufanikisha ukarabati huo, akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono.


size=4]
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 8 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
CCM watueleze watanzania ni nani DEEP GREEN, na kwa nini Rostam wa Iran ni mbunge wao wakati hana uraia. Wawavue uanachama Lowassa, mwanyika, Chenge, karamagi, balali, hosea, msabaha na mafisadi wote. Baadaye sasa wamuenzi BABA WA TAIFA. Achen unafiki CCM

na Maria Nyerere, Butiama, Mara, - 26.03.08 @ 09:52 | #3575

Namshukuru sana sana mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mtazamo wake wa mbali wa kuimarisha chama.

Naomba sana wajumbe wote wa Kikao hicho cha NEC watumie uwepo wao ktk kikao hicho kuimarisha chama kwa kueleza wazi wazi bila kulindana matatizo yote ktkt chama na serikali na kutoa mapendekezo kwa Mwenyekiti Taifa ili aweze kuchukua hatua staili.

Hivi sasa wannchi wa nchi hii sio wale wa miaka ya nyuma. Hivyo basi ili tuweze kukijenga chama chetu naomba tutoe mapendekezo kwa mfano mimi nikependekeza kwamba viongozi wote wa chama CCM walioingiza nchi ktkt umaskini mkubwa sana na kusababisha wananchi wa nchi hii kuingia kwenye gharama kubwa ktk matumizi ya kila siku watolewe uanachama kabisa na pia wachukuliwe hatua. Hii italete uhai mkubwa sana ktk chama.

Na ukirudi nyuma, siku Rais wa jamhuri ya Tanzania alivyohutubia bunge kwa mara ya kwanza, maneno yake yamefikia ktk utekelezaji wake kabisaaa.Hivyo naomba Mwenyekiti wa CCM Taifa akamilishe ahadi yake kwa vitendo bila kuona huruma ndio kujenga chama na maendeleo ya nchi hayapatikani bila kujitoa muhanga.
Nakumbuka hotuba za baba wa Taifa alisema halikuwa hana utani na mtu akifanya kosa au uzembe ktk mambo ya msingi ya nchi. Hivyo nkuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa usifanye utani ktk mambo ya msingi ya nchi, tumia mmlaka yako kama mwenyekiti wasambaratishe wote waliofanya mambo ya kuhiujumu nchi kwa maslahi yao binafsi.
Nawatakieni kikao chema chenye uelekeo wa kuimarisha chama chetu na maendeleo ya nchi nyetu.

Kidumu chama cha mapinduzi.

na jozee, Irg, - 26.03.08 @ 10:11 | #3576

hii ni kawaida ya ccm kufanya kufuru katika vikao vyake mbalimbali kwa pesa za mafisadi.naomba m/kiti wa ccmJK atutajie mafisadi wa EPA na waache unafiki kwa hili ***** hawezi kurudisha mali alafu unakataa kumtaja.huo ni unafiki na kutufanya watz kuwa wajinga na mambumbumbu.haya JK kazi kwako umeamua kuwapeleka mafisadi kwa hayati Nyerere,naona kama wanaenda kumkashifu mzee wetu ngoje afufuke sijui hizo sura zenu mtazipeleka wapi na ufisadi.asante

na fredy Godwin, Tumaini-iringa university, - 26.03.08 @ 10:38 | #3579

Ikiwezekana pia wakodi helikopta ya Mbowe kuwapeleka wajumbe wa NEC butiama

na kk - 26.03.08 @ 10:40 | #3581


Makamba na wenzake watambue kwamba wakati wa kujidai na kujigamba umepita, wawape wananchi haki zao.

Kuendelea kutamba kwamba CCM hawana tatizo na pesa wakati tunajua kwamba ni pesa zinazotokana na ufisadi ni kuendelea kutuumiza roho. Huku ni kuonyesha kwamba watu hawa hawana adabu na heshima kwa wananchi katika wakati huu mgumu wa ufisadi.

Kutambia hela ni ufedhuli na ujeuri usio na maelezo, ni kielelezo cha upeo mdogo wa uelewa wa viongozi wa chama kikongwe, CCM.

Maelezo ya kumuenzi Baba wa Taifa ni matusi kwa mzee huyo, kwani huwezi kumuenzi mtu kwa kupinga aliyoyasimamia.

Mungu awajalie viongozi wa CCM wafunguke macho na kuona ukweli na haki.

na Amk, Dar, - 26.03.08 @ 10:48 | #3583

Ni kikao cha kiini macho kama vikao vingine vya chama cha majambazi,hivyo wadanganyika wasitegemee kuwa kuna lolote jipya litapatikana labda wasubiri kusikia mbinu mpya zitakazotumika kulinda wafadhili wa ccm,yaani wakina epa,uchumond,ticks,songas,ubinafsishaji na kuendelea.........wasiguswe na mkono wa sheria.

na kadogoo, mbarara, - 26.03.08 @ 10:59 | #3585

sijui kwanini makamba ni katibu mkuu wa ccm?!
ningekuwa mimi jk katibu mkuu wa ccm ningeteua mtu mwenye uwezo mkubwa wa kazi,elimu,fikra na uzoefu kama Abdulharaman kinana,Salim Ahmed Salim au hata jaka mwambi au aggrey mwanri nk.
makamba anapwaya sana ktk nafasi nyeti kama hiyo!

na jingo - 26.03.08 @ 11:07 | #3587

Kama ccm haina tatizo na pesa, tunaomba maisha bora kwa watanzania wote na siyo kula na kulala ka wajumbe huko mkutanoni na hatimaye kurudi kwao salama. Makamba acha upuuzi, unaongea upupu sana, hufai hata kuwa katibu wa kata!!!

na Tyson, Butiama, - 26.03.08 @ 11:11 | #3588[/size]
 
Bubu Ataka Kusema,

Kwanini unaona CCM kumualika Prof. Ndullu ni jambo lisilofaa.

Niliposoma kichwa cha habari hata mimi nilishutuka lakini kwenda kusoma
ndani nikagundua huenda ni jambo jema kwa CCM na vyama vingine kupigwa somo la uchumi na prof. wa BOT.

Boss wa BOT anaweza kuitwa na kutoa semina sehemu mbalimbali na hata kuhojiwa juu ya mwenendo wa uchumi wa nchi.

Bila ya kusahau yale ya EPA, mimi binafsi naona hii ni move nzuri ambayo CCM wamefanya. Kule CCM kuna watu wanafikiri, tatizo tu hawatumii hizo fikra kwa kuendeleza nchi.

Muhimu sasa ni kusubiri Pro. Ndullu atasema nini.
 
Bubu Ataka Kusema,

Kwanini unaona CCM kumualika Prof. Ndullu ni jambo lisilofaa.

Niliposoma kichwa cha habari hata mimi nilishutuka lakini kwenda kusoma
ndani nikagundua huenda ni jambo jema kwa CCM na vyama vingine kupigwa somo la uchumi na prof. wa BOT.

Boss wa BOT anaweza kuitwa na kutoa semina sehemu mbalimbali na hata kuhojiwa juu ya mwenendo wa uchumi wa nchi.

Bila ya kusahau yale ya EPA, mimi binafsi naona hii ni move nzuri ambayo CCM wamefanya. Kule CCM kuna watu wanafikiri, tatizo tu hawatumii hizo fikra kwa kuendeleza nchi.

Muhimu sasa ni kusubiri Pro. Ndullu atasema nini.

Seriously!! Deep down u actually believe kuna kitu kipya Ndulu atasema?? He is going to tell them what they want to hear that is Uchumi umeyumba kidogo but due to their strategies mwakani yote yatakaa sawa, na pia atawaambia secta ya kilimo inakuwa kwa kasi na hela za madini sasa zinatumika katika maendeleo bila kusahau kwamba hela za EPA zinarudi kwa kiasi kikubwa sana!! na atamaliza speech kwa kusema BOT sasa ni swafi kabisa!!

Makamba kama MC wa CCM ataanzapiga makofi atamsifu raisi na kamati zake, atamsifu Ndulu kwa kazi nzuri BOT , watachinja mbuzi na kunywa beer..wakati watapofika Dar hakuna umeme majumbani kwao!!

Shit kwa mwendo huu mbona naona hata mimi kazi ya u gavana BOT naiweza!! LOL...
 
Seriously!! Deep down u actually believe kuna kitu kipya Ndulu atasema?? He is going to tell them what they want to hear that is Uchumi umeyumba kidogo but due to their strategies mwakani yote yatakaa sawa, na pia atawaambia secta ya kilimo inakuwa kwa kasi na hela za madini sasa zinatumika katika maendeleo bila kusahau kwamba hela za EPA zinarudi kwa kiasi kikubwa sana!! na atamaliza speech kwa kusema BOT sasa ni swafi kabisa!!

Makamba kama MC wa CCM ataanzapiga makofi atamsifu raisi na kamati zake, atamsifu Ndulu kwa kazi nzuri BOT , watachinja mbuzi na kunywa beer..wakati watapofika Dar hakuna umeme majumbani kwao!!

Shit kwa mwendo huu mbona naona hata mimi kazi ya u gavana BOT naiweza!! LOL...



teh teh...hata mimi ni governor Killuminati, CCM chama cha Clowns for sure!
 
Well, Mtanzania you may be right! but try to picture this, Mwenyekiti wa chama cha Democratic(DP), Mch. Christopher Mtikila, amemwita Professor B. Ndulu, ktk kikao cha chama chake kule Bagamoyo,ili kuwaeleza wanachama hali ya uchumi wa nchi?? What do u think Mtanzania, atakuja??....



...na kuhusiana na kuwa atasema nini(Ndulu)he wont be saying shit, umeishasikia msemo au maneno NIDHAMU YA WOGA??..right now he'll be wetting himself, on what will become of him, if he doesn't go(which is the right thing to do, according to me)....CCM your are so full of time, Chief of the clowns akiwa Mh. Makamba.
 
Bubu Ataka Kusema,

Kwanini unaona CCM kumualika Prof. Ndullu ni jambo lisilofaa.

Niliposoma kichwa cha habari hata mimi nilishutuka lakini kwenda kusoma
ndani nikagundua huenda ni jambo jema kwa CCM na vyama vingine kupigwa somo la uchumi na prof. wa BOT.

Boss wa BOT anaweza kuitwa na kutoa semina sehemu mbalimbali na hata kuhojiwa juu ya mwenendo wa uchumi wa nchi.

Bila ya kusahau yale ya EPA, mimi binafsi naona hii ni move nzuri ambayo CCM wamefanya. Kule CCM kuna watu wanafikiri, tatizo tu hawatumii hizo fikra kwa kuendeleza nchi.

Muhimu sasa ni kusubiri Pro. Ndullu atasema nini.

CHADEMA nao wamuite katika vikao vyao ili wamuhoji basi, vyote si vyama vya siasa?
 
Well, Mtanzania you may be right! but try to picture this, Mwenyekiti wa chama cha Democratic(DP), Mch. Christopher Mtikila, amemwita Professor B. Ndulu, ktk kikao cha chama chake kule Bagamoyo,ili kuwaeleza wanachama hali ya uchumi wa nchi?? What do u think Mtanzania, atakuja??....



...na kuhusiana na kuwa atasema nini(Ndulu)he wont be saying shit, umeishasikia msemo au maneno NIDHAMU YA WOGA??..right now he'll be wetting himself, on what will become of him, if he doesn't go(which is the right thing to do, according to me)....CCM your are so full of time, Chief of the clowns akiwa Mh. Makamba.


Killuminati,

Tatizo hapa ni watu kuwa na wasiwasi na kila jambo ambalo CCM wanafanya.

Idea yenyewe sio mbaya, hao NEC ndio wanapango mipango ambayo serikali ya CCM inatekeleza, kupigwa lecture na prof. Ndullu linaweza kuwa jambo zuri, of course kama wako tayari kusikiliza.

Hivyo hivyo hata CHADEMA au chama kingine wanaweza kumwita kwenye mkutano wao kama wanataka kujua hali ya uchumi na kumwuliza maswali juu ya mwenendo wa uchumi wetu.

Wenzetu walioendelea wana mikutano na gavana mingi tu kuanzia wasomi, wafanyabiashara, wabunge mpaka wanasiasa wengine.

Idea sio mbaya, labda tupinge kwasababu hatuamini CCM wataitumia vizuri hiyo
taarifa.

Labda sasa CHADEMA au chama kingine nao kama wanataka lecture ya prof. wafanye hivyo na kama atakataa bila sababu, hapo tunaweza kuifanya kuwa issue, vinginevyo tunachopinga ni kama CCM walivyopinga innovation ya Mbowe ya kukampeni kwa helikopta, baada ya muda na wao wakajiona wajinga na kuanza kutumia helikopta.
 
CCM kukaangana Butiama

Waandishi Wetu Machi 26, 2008

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wiki hii kinakutana kijijini Butiama huku kikiwa katika shinikizo la ndani na nje, la kutaka kifanye mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa siasa nchini.

Hiyo inatokana na tukio la karibuni la Bunge kuchukua hatua za kujisafisha kwa kushughulikia tuhuma za ufisadi, ambazo zilijitokeza zaidi katika kashfa ya kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.

Vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), vitakutana Butiama ikiwa ni ishara ya kuvuta hisia za wajumbe kwa yale aliyoyasimamia Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake. Mwalimu alizaliwa Butiama na amezikwa hapohapo.

Habari ndani ya CCM zinaeleza kwamba, kwa hali ya mambo ilivyo, mgawanyiko unakinyemelea chama hicho tawala huko Butiama, kutokana na kuibuka makundi yanayoandaa mikakati tofauti, moja likijipanga kuwasafisha watu waliotuhumiwa kwa ufisadi na jingine likijenga hoja ya kutaka CCM kuchukua hatua kali dhidi yao.

Vyombo kadhaa vya habari na vyanzo mbalimbali, bila kutaja majina, wiki hii vimesema kwamba CCM inajiandaa katika moja ya matukio ya Butiama, kuwachukulia hatua watendaji wa juu wa Serikali waliohusishwa na lile sakata la mradi wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni ya Richmond Delevelopment LLC.

Japo majina hayatajwi, lakini wanaorejewa katika hatua hiyo, kubwa ya aina yake, ni pamoja na wale waliojiuzulu kutokana na kutajwa katika kashfa hiyo: aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha. Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Afrika Mashariki, Dk. Msabaha alikuwa Nishati na Madini.

Kwa mujibu wa habari hizo zinazohitimisha taarifa zilizozagaa miongoni mwa wana CCM, ni wazi kwamba , kuna wana CCM ambao wanataka hata wale ambao si watendaji serikalini nao washughulikiwe na chama kutokana na kutajwa kwao na kashfa zilizoibuka.

Kashfa ya Richmond, iliibua mambo bungeni chini ya usimamizi wa Spika Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati Dk. Harrison Mwakyembe. Kashfa nyingine iliyotikisa Serikali na CCM ni ile ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), angalau kwa sasa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambako zaidi ya shilingi bilioni 133 zimetajwa kupotea huku chama hicho tawala na makada ama wafadhili wake wakihusishwa kwa karibu mno na ubadhirifu huo.

Pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kudai kwamba ajenda za vikao vya Butiama bado ni siri, tayari watendaji na viongozi wa chama hicho, wamekwisha kugusia baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuibuka katika vikao hivyo na bila kumung'unya maneno wote wamezungumzia ufisadi na kashfa zilizotikisa nchi katika siku za hivi karibuni.

Wakati kiongozi mmoja wa CCM aliliambia Raia Mwema kwamba suala la BoT, litazungumzwa, mtendaji mmoja alisema suala la kutenganisha biashara na siasa ni moja ya ajenda za vikao vya Butiama lakini wote hawakubainisha undani wa ajenda hizo.

Hata hivyo, taarifa ya CCM iliyosainiwa na Makamba, na kusambazwa kwa vyombo vya habari jana Jumanne, ajenda za Butiama zinatajwa kwa ujumla, bila kuingia kwa undani wa kitakachotokea.

Kipengele ambacho kinaficha ajenda nyingine zitakazojadiliwa kipo kwenye ajenda ya nne, kikisema kwamba, "kikao pia kitapokea na kujadili taarifa nyingine zinazohusu uhai na maendeleo ya Chama chetu kwa ujumla."

Katika taarifa hiyo ya Makamba, kunatajwa ajenda nne tu, ikiwamo ya taarifa kuhusu hali ya kisiasa na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo ya CUF na CCM.

Ajenda nyingine zinazotajwa ni taarifa ya hali ya uchumi nchini, taarifa ya uchaguzi mdogo wa Bunge katika Jimbo la Kiteto na taarifa ya sherehe za CCM kutimiza miaka 31 na matembezi ya mshikamano yaliyofanyika Februari 2, mwaka huu.

Katibu Mwenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, alipoulizwa kuhusu ajenda nyingine, alikataa kuzungumzia undani wake, hasa alipoulizwa kuhusu ajenda kama vile kashfa ya Richmond, Azimio la Zanzibar, kashfa ya EPA, mikataba mibovu ya madini na kuchanganya siasa na biashara.

Kabla hata ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, kuwasilisha ripoti yake bungeni, Rais Jakaya Kikwete, aligusia suala la kutenganisha siasa na biashara, hoja ambayo ilikuwamo katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Kushabihiana kwa mawazo ya Rais Kikwete na yale ya Kamati Teule ya Bunge, tena kwa kushabihiana hata kwa muundo wa sentesi kwa kiwango kikubwa, kunayapa uzito mkubwa maneno hayo na hivyo kuwaweka katika mazingira magumu zaidi wanasiasa waliotajwa katika ripoti ya Richmond.

Miongoni mwa wanasiasa waliotajwa katika ripoti hiyo lakini hawamo ndani ya serikali, yumo mjumbe wa NEC, na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambaye pamoja na kukiri kufanya biashara na makampuni ya umeme, amekanusha kuhusika katika kashfa ya kandarasi ya mradi wa Richmond.

Rostam ambaye ni mwanasiasa mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani na nje ya serikali na CCM, amenukuliwa akisema kwamba yanayotokea ni vita ya kisiasa ambayo hana shaka kwamba atakabiliana nayo kwa kuwa anajiamini yeye ni mtu safi katika biashara zake na katika siasa.

Hata hivyo, Rostam amenukuliwa na gazeti moja la kila siku akisema kwamba anamuunga mkono Kikwete katika nia yake ya kutenganisha biashara na siasa, kauli ambayo inaashiria kutokuwapo upinzani mkubwa katika hoja hiyo, ambayo inaweza kutolewa uamuzi na azimio kijijini Butiama.

Kauli hiyo ya Rostam inaashiria pia maandalizi yake ya kutoa maelezo katika vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kufanyika mjini Dodoma mapema mwezi ujao, baada ya kutakiwa kufanya hivyo kufuatia kauli zake za kuituhumu Kamati Teule ya Bunge kuwa haikumtendea haki kwa pamoja na mambo mengine, kuwa haikumhoji.

Mjumbe mmoja wa NEC ambaye tayari yuko njiani kuelekea mkoani Mara, ameliambia Raia Mwema kwamba kama kweli CCM inakusudia kumuenzi Baba wa Taifa, kuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba inakirudisha chama kwa wananchi badala ya sasa kuwa zaidi mikononi mwa "wateule wachache".

"Hivi sasa watu wamesahau kabisa suala la alama za CCM za jembe na nyundo na maana yake halisi na wako ambao nahisi wanataka kufikiria hata kuweka noti katika katika bendera ya chama, kwa hiyo huko Butiama lazima tuamue kurudisha imani ya wananchi, chama chetu ni chama cha wakulima na wafanyakazi na wengine hatuwakatai lakini watusaidie si kututumia," alisema mwana CCM huyo ambaye ana madaraka ndani ya chama hicho.

Pamoja na kuwapo ajenda rasmi za mkutano huo, imeelezwa kwamba baadhi ya mambo yataibuliwa ndani ya kikao kwa nia ya kuwashitukiza wale ambao wana nia ya kuvuruga nia njema ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete ya kukisafisha chama.

Katika hotuba zake zote tokea ile ya kwanza alipokabidhiwa uenyekiti na mtangulizi wake, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Kikwete amekuwa akibainisha nia yake ya kukisafisha chama, ambacho alisema kimekuwa kikiendelea kupoteza baadhi ya sifa zake za kuwa chama cha kutetea wanyonge.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kuna kundi linalojiandaa kutumia mkutano huo kuzuia mkakati wowote unaoweza kuwavurugia mipango yao ya baadaye kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa taratibu na kanuni za CCM na badala yake kuhakisha mkutano huo unatumika kuwajenga zaidi kisiasa.

"Vikao vya Butiama vina malengo ya kuwaengua baadhi ya watu katika siasa na hofu hiyo inazingatia kwamba Nyerere amekuwa akidaiwa kuwachukia kabla ya kifo chake na hivyo kwenda Butiama ni kuwakumbusha wajumbe kwamba waliwahi kukataliwa na Mwalimu. Kwa kweli Mwalimu aliwajenga Watanzania kuwachukia matajiri hata wale ambao hawana hatia," alisema mmoja wa watu walio karibu na wanasiasa wanaotuhumiwa.

Lakini kauli hiyo imepingwa na mwana CCM mwingine ambaye yuko karibu na familia ya Mwalimu Nyerere, akisema kwamba kuna matajiri wengi ambao walishiriki kwa uadilifu mkubwa katika ujenzi na ustawi wa Tanzania kabla na baada ya uhuru na baadhi yao walishiriki hata kuunda serikali.

"Unakumbuka tulikuwa na akina Amir Jamal, Al-Noor Kassum na kina Jaffar Sabodo, ambao hadi leo wanaheshimika na hawajachukiwa na Watanzania kwa kuwa walikuwa waadilifu, sasa leo ukisema Mwalimu alichukia matajiri unakuwa unakosea," alisema mwana CCM huyo, ambaye yuko karibu mno na familia ya Mwalimu Nyerere.

Ajenda ya mwafaka kati ya CCM na CUF, ambao unaelezwa kuwa unapingwa na baadhi ya wana CCM wenye msimamo mkali Visiwani Zanzibar, wakisema utapunguza nguvu ya chama hicho Visiwani.

Kwa mujibu wa habari hizo, kipengele kinachowakera wana CCM wenye msimamo mkali Zanzibar ni kile cha kushirikiana katika Serikali na CUF, jambo ambalo wanaliona litawapunguzia nguvu ya kisiasa na kuwapa nguvu wapinzani.

Hitimisho la vikao vya Butiama linatarajiwa kuibua mambo ambayo yatatoa mwelekeo wa CCM ama kuendelea kuwa imara ama kugawanyika na pengine "Azimio la Butiama" litakuwa azimio la tatu la chama tawala baada ya Azimio la Arusha la mwaka 1967 ‘lililovurugwa' na "Azimio la Zanzibar" la mwaka 1992.

Tayari wanasiasa machachari wa upinzani, akiwamo Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk.Wilbroad Slaa, wamehoji usafi wa CCM kufanya kikao Butiama mahali alikozikwa Baba wa Taifa, ambaye ameaga dunia akiwa hana doa, kauli ambayo imezungumzwa pia na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Wakati hayo yakijiri, viongozi wa dini, wakiwamo mashehe wakati wa sherehe za Maulidi wiki iliyopita na Maaskofu wakati wa ibada za Pasaka, wamezungumzia wazi kuhusu watuhumiwa wa ufisadi wakitaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi yao ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao.
 
kama CCM watarudi na MIFISADI(maana ni mingi) itabidi tusioneane aibu ni kutangaza rasmi kuwa CCM wote ni MAFISADI.

Hii haina maana kuwa tutakuwa tunawachukia hila ni kuwasaidia. Maana ukikuta mtoto wako anatembea na wavuta bangi ipo siku naye antavuta bangi. na ukikaa na wezi nawe kuna siku utakuwa Mwizi. Hivyo CCM wakikaa na Mafisadi na wakaona sawa itabidi wote tuwaite MAFISADI.

CCM ogepeni jina FISADI ni udhalilishaji wa hali ya juu.
 
hakaangwi mtu wala nini, nyie subirini muone watu wakipongezana kwa kazi nzuri ya kushughulikia ufisadi. Na baadaye maandamano ya kuungana mkono.

Thanks.
 
Nakuunga mkono kabisa Senti
CCM ni wasanii completely jamani, hakuna lolote la kutokea huko Butihama, unategemea kumwajibisha Lowassa kama Fisadi uku ukimwacha Mkapa ambaye ni Fisadi mkuu?
Kamwe hiyo haiwezekani kwa chama kama kile cha mafisadi watupu, maana wote wameoza kabisa, na hata Kikwete naye ni Fisadi tu jamani, nyie ngojeni tu ukweli utajulikana hapa hapa tu
Usanii kama kawaida ndo ngao ya Viongozi wa Tanzania

Nasubiri kuona spin watakayokuja nayo this time. Makamba ameruhusiwa kuongea na vyombo vya habari sasa ina maana hakuna chochote kitakachofanyika.........
 
Vikao vya chama na Gavana wapi na wapi?

Halafu cha kuelewa CCM hawana historia nzuri na Magavana.

Ni juzi tu kuna tuhuma za Deepgreen na CCM, labda kama wanaenda kumuliza hayo. Inawezekana wanamfunda jinsi ya kujibu maswali kisiasa.
 
Wanamuweka sawa huyo, anapewa dili kabisa la 2010 kuwa mchezo ni ule ule tu, ukisikia kelele za kisiasa hapa ni danganyatoto tu lakini 2009-2010 tutakuja na gia ileile ya National Security, kwa hiyo kaa tayari.

Ama sivyo tunakubebesha mzigo wa Balali, si ulikuwa number two wake plae.

Atasema nini zaidi ya kuwashukuru wazee kwa kumpa ulaji.

We unafikiri kwa nini vikao vinakuwa closed doors?
 
..............SASA gavana anataka kuleta hisia kuwa anaendwa kuwekwa sawa na ccm ili awasafishe kwenye tuhuma za benki kuu...na pia si unajua uchaguzi utakuja tena na ccm watahitaji tena kuchota pesa benki kuu..sasa lazima wakamweke prof nduru sawa ili asiwaangushe watakapohitaji kuchota mapesa ya kutumia ccm...

sasa hatutamchukulia tena prof ndullu kama proffessional..tutamuona kama dr balali..very soon!!!
 
teh teh...hata mimi ni governor Killuminati, CCM chama cha Clowns for sure!

Mkuu Heshima mbele, mimi ni mwanachama mkereketwa wa CCM, lakini no way kwamba I am a clown, vipi next time ukirekebisha hii lugha ambayo kwa kweli siyo ya kistaarabu, kutumiwa tena kwenye jamii kama hii, mimi nilifikiri tunaikataa hii lugha kwa waliotuvamia, sasa na wewe wa muda mrefu ukiitumia tutawaambia nini waliotuvamia?.

SASA gavana anataka kuleta hisia kuwa anaendwa kuwekwa sawa na ccm ili awasafishe kwenye tuhuma za benki kuu...

1. CCM ni chama kinachotawala Tanzania, kwa ridhaa ya wananchi waliokikubali kwa kuwapigia kura kutokana na kukubali sera zao, moja ya sera za CCM kwa taifa, ambazo waliziahidi kwenye kampeni za uchaguzi, ni pamoja na uchumi wetu ambao nguvu yake kubwa hutokea BOT, sasa CCM watafanya vipi mkutano mzito bila ya gavana? I mean regardless ya how our uchumi si doing, which as usual ni a debatable ishu, lakini ni haki not only kwa CCM, bali hata vyama vya upinzani kumuita vinapokuwa na mikutano yao mikubwa.

2. Mkuu ninaamini kwamba ungekuwa na hoja nzito sana, iwapo gavana wetu wa BOT, angekuwa in the past amewahi kuitwa kwenye mikutano mizito ya vyama vya upinzani, akakataa au CCM ikamkatalia aisende,

Otherwise, naona kama sio a weak argument, basi hakuna argument kabisaa, gavana ni lazima aende kule kwenye kikao kikubwa cha CCM, yaaani chama tawala, ili aweke mambo wazi exactly yalipo na pia wajumbe wa NEC, wapate nafasi ya kumuuliza maswali muhimu huku waziri wa hazina akiwepo, kuepuka kutupiana lawama, kama alivyofanya Mama Meghji, this time wote watakuwepo yaani waziri na gavana, I thought CCM ought to be louded kwa hiki kitendo kuliko kushambuliwa. To me the move sounds good, na ni matumaini yangu kuwa opposition wata-follow the idea in the future, wakikataliwa then tutamkoma nyani.

Ahsante Wakuu.
 
Bubu Ataka Kusema,

Kwanini unaona CCM kumualika Prof. Ndullu ni jambo lisilofaa.

Niliposoma kichwa cha habari hata mimi nilishutuka lakini kwenda kusoma
ndani nikagundua huenda ni jambo jema kwa CCM na vyama vingine kupigwa somo la uchumi na prof. wa BOT.

Boss wa BOT anaweza kuitwa na kutoa semina sehemu mbalimbali na hata kuhojiwa juu ya mwenendo wa uchumi wa nchi.

Bila ya kusahau yale ya EPA, mimi binafsi naona hii ni move nzuri ambayo CCM wamefanya. Kule CCM kuna watu wanafikiri, tatizo tu hawatumii hizo fikra kwa kuendeleza nchi.

Muhimu sasa ni kusubiri Pro. Ndullu atasema nini.

Anaalikwa ili akafanye nini wakati mafisadi hata kutajwa wanaogopwa? Tunaambiwa mafisadi wamerudisha bilioni 60 tunauliza zimewekwa katika bank ipi na account namba ni ipi, hakuna anayejibu. Tunauliza, wekeni majina hayo ya waliorudisha hizo bilioni 60 na kiasi walichorudisha, wanang'aa macho!. Nduku katutangazia kwamba kuna maofisa waliohusika na EPA pale BoT wamesimamishwa kazi, tumemuomba majina ya maafisa hao, nyadhifa zao na kutaka kujua kama bado wanalipwa mishahara, kanyamaza kimya.

Sasa huko Butiama atasema nini cha kuwaridhisha Watanzania? Kwani pesa zilizokupuliwa na mafisadi ni za wanachama wa CCM tu na siyo za Watanzania wote. Kipi atakachokisema Butiama ambacho anashindwa kukisema akiwa Dar!? :confused:
Usanii kama kazi!
 
hakaangwi mtu wala nini, nyie subirini muone watu wakipongezana kwa kazi nzuri ya kushughulikia ufisadi. Na baadaye maandamano ya kuungana mkono.

Thanks.

Chama Cha Mafisadi, tangu lini mwizi akamkamata mwizi mwenziye!? Hakuna jipya lakini hapa JF tutaendelea kuwalima tu kama kazi

1.jpg

Fisadi nambari one
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom