JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
..kama ni kutaka kujua kinachoendelea ndani ya BOT basi CCM-NEC inapaswa kumhoji Waziri wa Fedha. Huyo anajulikana kwamba ni mwanachama wa CCM.
..katika mataifa mengi yaliyoendelea Benki Kuu ni chombo kilicho huru. Mtendaji wake huachwa afanye maamuzi kwa maslahi ya nchi bila kuingiliwa na wanasiasa.
..hata kama katiba yetu inatoa mwanya kwa Raisi na CCM kumuingilia gavana ktk maamuzi yake ya kitaalamu, itakuwa vizuri kama CCM[au chama kilichoko madarakani]watajiepusha na kutumia mwanya huo.
..CCM ndiye mid-wife wa demokrasia yetu changa. sasa wakianza ku-behave vibaya wakati wako madarakani wanaweza kusababisha vyama vingine navyo kufuata mkondo ikiwa vitafanikiwa kushika dola.
..leo tukilazimisha gavana wa BOT ahojiwe na CCM-NEC nini kitazuia Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai, Mwanasheria Mkuu wa serikali, etc etc...kuingiliwa ktk majukumu yao na wanasiasa?
..hekima, busara, na uzalendo, vinapaswa kutuongoza hapa.