Kutoka Bungeni: Wabunge wamchagua Dr. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 la JMT

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742

Wabunge Wote 394
Wabunge waliopiga kura 369
Akidi ya wabunge wanaotakiwa 184
Wabunge Waliopo na kupiga kura 351

Kura Zilizoharibika 0
Magdalena Sakaya 101(28%)
Dr Tulia 250(71.2%)


Kinachoendelea kwa sasa na wagombea wanaogombea nafasi ya unaibu spika wanaomba kura na kwa sasa ni Magdalena Sakaya kupitia CUF, amesema ana uzoefu wa uongozi kwa miaka 20, kati ya hio miaka 10 ndani ya bunge. Sakaya akijibu swali la Kairuki kuhusu kufanya kazi na spika asie wa chama chake. Amesema kila mbunge anafanya kazi kwa ajili ya watanzania kuhakikisha matarajio ya watanzania yanafikiwa bila kuangalia chama.

Gekul: Umekuwa mbunge kwa awamu tatu, mawazo katika bunge hili hayatekelezwi na serikali, utatumiaje uzoefu wako kuunganisha bunge na serikali.

Sakaya: Tunatambua na awamu mpya ya awamu ya tano, tuna sura mpya za wabunge wengu, spika na tutakuwa na sura mpya ya naibu spika. Naamini sote tukiwa imara tunaenda kuyafikia matarajio ya wananchi.

Anaefata sasa ni Tulia Ackson kupitia chama cha mapinduzi (CCM)

Tulia: Kwa taaluma mimi ni mwanasheria na nimefanya hiyo kazi kwa miaka 14, nilishiriki kutengeneza kanuni zilizoendesha bunge la katiba. Nagombea nafasi kwa sababu najiamini na nina uwezo.

Matiko: Tunatambua alikuwa naibu mwanasheria mkuu na hakupaswa kuwa mwananchama wa chama chochote, leo unaomba nafasi ya unaibu spika, ukiwa mtendaji lakini tayari unachukua upande wa CCM. Unatuaminisha vipi hautaegemea upande!

Tulia: Nilichukua fomu za kugombania uspika nikiwa naibu mwanasheria, kwa ibara ya 67(ii) na 72, anashikilia nafasi mpaka awe candidate na kuwa candidate ni mpaka upite mchakato.

Katiba nimeisoma, kanuni nimezisoma na yapo makundi matatu matatu yanakatazwa kuwa wanachama wa vyama vya siasa ikiwemo wanajeshi!

Spika anamruhusu akakae baada ya baadhi ya wabunge kumtaka ajibu swali badala ya kuzunguka na kutokea sintofahamu.


 
Kwa siasa za kibongo, uwezo badaye mahaba kwanza!!!! Hata kama kukitokea nafasi yoyote bungeni inayohitaji mwanasheria, si ajabu AIRO/LUSINDE akamshinda tundu lisu, kupitia kura. Siasa za kishamba sana.

wewe unashangaa nini si watu walisema UKAWA wakiweka jiwe walitalipigia si akili zetu watanzania hizo bila kujali itikadi
 
Viherehere vya kutoa maoni aidha kwa kukosoa au kusifia huwa vinatuacha vinywa wazi baadaye. Maneno ya mwanaume siku chache kabla ya ndoa hayafanani na maneno atakayotoa miaka miwili baadaye kuhusu mwanamke yule yule, TULIA kwanza.....ndio kwanza kapatikana. Hapo anaongea taaluma, dhamira za moyo wake hazijakuwa wazi bado
 
Back
Top Bottom